Heri ya Siku ya Wajane Duniani 23 Juni, 2024

Dkt. Gwajima D

Minister
Joined
Nov 28, 2015
Posts
1,706
Reaction score
8,657
Wasaalam wanajukwaa.
Kuelekea Siku ya Wajane Duniani tarehe 23 Juni 2024, fahamu machache tafadhali 👇🇹🇿

HISTORIA; Siku ya Wajane Duniani huadhimishwa tarehe 23 Juni kila mwaka ambapo, iliasisiwa na Bw. Lord Loomba aliyeanzisha Taasisi ya Loomba mwaka 2005 baada ya baba yake kufariki tarehe 23 Juni mwaka 1954.

UMUHIMU WA SIKU HII: Wajane ni kundi kubwa ambalo, hukabiliwa na changamoto nyingi baada ya kufiwa na wenza wao ikiwemo, wengine kuachwa katika umaskini, kunyimwa haki zao za mirathi kama ardhi, haki za kuwalea watoto na kudhulumiwa mali nyinginezo walizochuma kwa pamoja na wenza wao. Aidha, wajane wengine hufukuzwa nyumbani mwao, hutengwa na kunyanyaswa na ndugu wa mume pamoja na jamii na wengine hulazimishwa kuolewa na ndugu wa marehemu pasipo ridhaa yao huku wengine wakikosa huduma ya utetezi pale wanapotafuta haki zao.

Maadhimisho ya siku ya wajane nchini Tanzania hulenga pia, kukuza hamasa, mshikamano na uelewa ndani ya jamii ili kuacha ukiukwaji wa haki za binadamu kwa wajane. Aidha, maadhimisho haya hutoa fursa ya pamoja kwenye kutambua changamoto za wajane na namna ya kukabiliana nazo. Katika maadhimisho haya, wajane pia hutengeneza kwa upya mtandao unaowapa nafasi ya kupata taarifa mbalimbali zinazohusu fursa za kiuchumi, kijamii na uongozi kwa maendeleo na ustawi. Halikadhalika, siku hii ni muhimu katika kuongeza uhamasishaji wa kupinga ukiukwaji wa haki za binadamu kwa wajane.

KAULIMBIU 2024. “Imarisha Mifumo ya upatikanaji wa Nishati: Kukuza Uchumi wa Wajane na Familia”.

MAADHIMISHO YANAFANYIKA WAPI? Kila mkoa na wilaya zake kuadhimisha.
_________________

ZIADA YA TAARIFA 👇

Duniani inakadiriwa Wajane ni takriban millioni 258 na kati ya hao, Wajane 115 millioni wanadhulumiwa, wanafanyiwa ukatili, wanakabiliwa na umaskini na kutengwa na jamii.

Tanzania, idadi ya wajane ni 1,396,262 sawa na asilimia 4.5 ya wanawake wote nchini, kwa sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2022.

Kaulimbiu ya Mwaka huu hapo juu, inaendana na agenda ya Kitaifa inayosisitiza matumizi ya Nishati Safi na Salama ya Kupikia ambapo, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni Kinara wa Upatikanaji wa Nishati hii Duniani kwa lengo la kupunguza mzigo wa kazi za malezi (unpaid care work) (zisizo na malipo) kwa Wanawake wakiwemo Wajane.

Aidha, Mwongozo wa Benki ya Dunia kuhusu Nishati safi na salama ya kupikia wa mwaka 2020 unasisitiza matumizi ya Nishati Safi na Salama ya kupikia.

Faida za juhudi zote hizi kuwa, hazilengi tu kupunguza mzigo wa kazi kwa wanawake wakiwemo wajane bali pia, kuwapa nafasi ya kujihusisha na shughuli za uzalishaji mali na hivyo kuingiza kipato katika ngazi ya jamii na Taifa na kupunguza uharibifu wa mazingira pamoja na athari za kiafya.
MWISHO.

Sikuwahi kujua kama kuna siku ya wajane Duniani, nashukuru mama yangu amefikiwa, ni miaka zaidi ya kumi tangu awe mjane, asante Dkt Gwajima
 
Maskini mama yangu, ni miaka 30 sasa akiwa mjane! Wanawake wa zamani walikuwa na uvumilivu sana.
Salamu ziwaendee wamama wote, akiwemo mama yangu, waliofiwa na waume zao, wakalea watoto wao walio achiwa bila kuolewa tena.

Leo ndo nimejua kuna siku ya wajane, jf bana!
 
Mungu aendelea kumpa nguvu mama yangu pamoja na wajane wote duniani!!! Kusema ukweli kuwa mjane na kusimama na familia so Jambo jepesi....walio lelewa na mjane Hili wanalielewa Sana...passion yangu siku moja niwe na NGO inayotetea kundi hili la wajane wanapitia mazito mnooo.
 
Asante sana kwa taarifa Mh.Waziri, Wizara unayoiongoza ina majukumu mazito sana katika kukuza Ustawi wa Jamii yetu na kutatua matatizo mbalimbali yanayoendelea kutokea katika jamii zetu hizi. Ubarikiwe sana
 
Nakushukuru wewe na wengine wote kwa muda wako kusoma taarifa hii. Nina Imani utawapa na wengine wajue na waendelee kufuatilia taarifa hizi kwenye kurasa mbalimbali za wizara ya Jamii.
 
Sikuwahi kujua kama kuna siku ya wajane Duniani, nashukuru mama yangu amefikiwa, ni miaka zaidi ya kumi tangu awe mjane, asante Dkt Gwajima
Shukrani kwa muda wako, siku hii ipo na ni msaada Sana kwenye kujenga uelewa wa pamoja kuhusu kundi hili na wanandoa wakubali kuandika Wosia mapema Ili mmoja ikitokea ametangulia, mwingine aendeleze familia. Aidha, inawakumbusha wanaume kuwapa wanawake Haki za elimu na kiuchumi maana huwezi jua nani anamwacha mwingine. Tuelimishe wengine tafadhali
 
Maskini mama yangu, ni miaka 30 sasa akiwa mjane! Wanawake wa zamani walikuwa na uvumilivu sana.
Salamu ziwaendee wamama wote, akiwemo mama yangu, waliofiwa na waume zao, wakalea watoto wao walio achiwa bila kuolewa tena.

Leo ndo nimejua kuna siku ya wajane, jf bana!
Poleni sana, hongera kwa mama huyu aliyesimama kwa nafasi yake🙏🏽, Mungu ampe heri na baraka zake. Tuendelee kuwapa taarifa wengine 🤝
 
Mungu aendelea kumpa nguvu mama yangu pamoja na wajane wote duniani!!! Kusema ukweli kuwa mjane na kusimama na familia so Jambo jepesi....walio lelewa na mjane Hili wanalielewa Sana...passion yangu siku moja niwe na NGO inayotetea kundi hili la wajane wanapitia mazito mnooo.
Mungu akubariki kwa maono yako, nakuombea ufanikishe🙏🏽
 
Wasaalam wanajukwaa.
Kuelekea Siku ya Wajane Duniani tarehe 23 Juni 2024, fahamu machache tafadhali 👇🇹🇿

HISTORIA; Siku ya Wajane Duniani huadhimishwa tarehe 23 Juni kila mwaka ambapo, iliasisiwa na Bw. Lord Loomba aliyeanzisha Taasisi ya Loomba mwaka 2005 baada ya baba yake kufariki tarehe 23 Juni mwaka 1954.

UMUHIMU WA SIKU HII: Wajane ni kundi kubwa ambalo, hukabiliwa na changamoto nyingi baada ya kufiwa na wenza wao ikiwemo, wengine kuachwa katika umaskini, kunyimwa haki zao za mirathi kama ardhi, haki za kuwalea watoto na kudhulumiwa mali nyinginezo walizochuma kwa pamoja na wenza wao. Aidha, wajane wengine hufukuzwa nyumbani mwao, hutengwa na kunyanyaswa na ndugu wa mume pamoja na jamii na wengine hulazimishwa kuolewa na ndugu wa marehemu pasipo ridhaa yao huku wengine wakikosa huduma ya utetezi pale wanapotafuta haki zao.

Maadhimisho ya siku ya wajane nchini Tanzania hulenga pia, kukuza hamasa, mshikamano na uelewa ndani ya jamii ili kuacha ukiukwaji wa haki za binadamu kwa wajane. Aidha, maadhimisho haya hutoa fursa ya pamoja kwenye kutambua changamoto za wajane na namna ya kukabiliana nazo. Katika maadhimisho haya, wajane pia hutengeneza kwa upya mtandao unaowapa nafasi ya kupata taarifa mbalimbali zinazohusu fursa za kiuchumi, kijamii na uongozi kwa maendeleo na ustawi. Halikadhalika, siku hii ni muhimu katika kuongeza uhamasishaji wa kupinga ukiukwaji wa haki za binadamu kwa wajane.

KAULIMBIU 2024. “Imarisha Mifumo ya upatikanaji wa Nishati: Kukuza Uchumi wa Wajane na Familia”.

MAADHIMISHO YANAFANYIKA WAPI? Kila mkoa na wilaya zake kuadhimisha.

View attachment 3022790
Maskini Mke wa Nzunda, aliyekuwa RAS wa Kilimanjaro ambaye kapoteza uhai akiwa kazini. Mke wake sasa ni mjane
 
Asante sana kwa taarifa Mh.Waziri, Wizara unayoiongoza ina majukumu mazito sana katika kukuza Ustawi wa Jamii yetu na kutatua matatizo mbalimbali yanayoendelea kutokea katika jamii zetu hizi. Ubarikiwe sana
Hii wizara ni kubwa na Pana na kama mnavyojua jamii ni watu na mambo ya watu ni mapya Kila Leo. Hivyo, inahitaji jamii wenyewe waimiliki wizara yao Ili twende sawa kwa haraka🤝🙏🏽
 
Mungu awatie nguvu wajane wote 🙏🏾
 
Back
Top Bottom