Heri ya Mwaka Mpya!!!

Heri ya Mwaka Mpya!!!

MwanaFalsafa1

JF-Expert Member
Joined
Feb 26, 2008
Posts
5,564
Reaction score
850
Kwanza nitangulize heri ya mwaka mpya kwa wanaJF wote na watembeleaje wote wa tovuti hii. Mungu ametuepushia mengi na tunaomba azidi kutuepushia. Pamoja na kusherekea na ndugu, jamaa, marafiki inabidi tutambue kwamba kusherekea huku hakudumu sana kwa maana bado kuna kero zile zile na matatizo yale yale yaliyo kuepo mwaka jana ambayo yame tufuata mwaka huu.

Katika 2013 tunaelekea katika miaka nane (8) ya utawala wa Mh. Jakaya Kikwete na serikali ya awamu ya pili. Kwa mawazo yangu huu ndiyo mwaka wa mwisho haswa kwa serikali hii kutimiza azma zake mbali mbali maana taratibu kuanzia mwakani akili za viongozi na wananchi zitaanza kuelekea kwenye kutafuta mrithi wa JK. Kwa wenzetu wazungu hii wanaita "lame duck" period, kipindi ambacho nguvu (angalau za kiushawishi) za raisi zina pungua kwa sababu watu washajua muda si mrefu ataondoka. Kwa hiyo basi ukiacha jambo lolote kubwa linalo weza tokea 2014 au 2015, huu ndiyo utakua mwaka ambao jina la JK litakua lisha andikwa kwenye mawe.

Ushauri kwa Mh. Raisi:
1. Tumia mwaka huu kujenga jina lako zaidi ili Watanzania wakukumbuke kwa mazuri zaidi. Bado kuna mambo ambao yanaweza yaka fanyika kwa kipindi hiki kifupi kicho baki kujiongezea heshima kwa wananchi wako.

2. Simamia uandikaji wa katiba mpya ili katiba mpya itumike kwenye uchaguzi mkuu ujao. Naamini kama ukifanikiwa kwa hili na kama katiba ikitimiza matarajiwa ya wananchi basi hiki ndicho kitakua kitu kikubwa zaidi utakacho kumbukiwa.

3. Ongoza chama chako kwa hekima zaidi. Tamaa za uogozi ya baadhi ya wanachama wenzako unaweza ukadhoofisha serikali yako na hakika kupunguzia heshima serikali yako mbele ya wananchi. Hakikisha maslahi ya kichama haya tafuni yale ya taifa.

4. Dumisha amani na demokrasia. Mwaka 2012 umekua mwaka wa maadamano kuzuiwa pasipo sababu muhimu, wananchi kuuliwa kwa ajili ya itikadi zao za kisiasa, jeshi la polisi kutumia ubabe kwa wananchi wake, na viongozi halali kushtakiwa mahakamani kuvuliwa vyeo kupitia nyundo ya hakimu badala ya kura za wananchi.

Ushauri kwa upinzani (haswa Chadema):
1. Simamieni swala la katiba mpya
2. Endeleeni kuibua mijadala yenye manufaa kwa taifa
3. Zuieni mambo ambayo yata haribu sifa yenu mbele ya wananchi katika muda huu mfupi uliojaa.

Ushauri kwa wananchi:
1. Tuendelee kuelimisha jamii kuhusu haki zao za kikatiba, wajibu wao kwenye kuhoji na kuwajibisha viongozi wao na umuhimu wa kushiriki siasa za nchi. Naamini kila mmoja anaweza kwa nafasi yake akamuelimisha mtu iwe majumbani kwao, mitaani kwao, maofisini nk.

2. Tuendelee kuipigia kelele serikali itimize ahadi zake maana ahadi ni deni.

3. Tusi waachie viongozi tu bali na sisi tuweke maslahi ya taifa mbele. Pale kiongozi yoyote au chama chochote kinapo fanya vizuri tusifie halkadhalika wakifanya vibaya tukemee bila kuangalia mapenzi yetu binafsi.


Ni hayo tu kwa sasa. HERI YA MWAKA MPYA WANANCHI WENZANGU!
 
Back
Top Bottom