Heri ya mwaka mpya 2012 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Heri ya mwaka mpya 2012

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by kasimba123, Dec 29, 2011.

 1. k

  kasimba123 JF-Expert Member

  #1
  Dec 29, 2011
  Joined: Apr 18, 2010
  Messages: 1,318
  Likes Received: 188
  Trophy Points: 160
  Amani ya M.Mweenyezi Mungu iwe nawe na msamaha wake na baraka sake ziwe Juu yako.
  Heri ya mwaka mpya kwa wale ambao M.Mungu atawajaalia kuuufikisha.
  Nimatumaini yangu kuwa utakuwa Mwaka wa mafanikio kwako wewe na familia yako ndugu na jamaa zako kwa Ujumla. Nimeona nizitume salaam hizi kwani sina uhakika kuwa nitaufikisha Mwaka kama ilivyoada kuwa ni Mungu mwenyewe ndiye ajuaye Saa yang ya Mwisho kuishi Katika Dunia hii

  Hakika Mungu ni Mwema na ni katika wema wake, Huruma na utukufu wake atatujaalia kutuondolea madhila na kutujaalia kwa lolote tufiirialo kulifanya kwenye mwaka MPYA 2012.

  Kumbuka Kumuomba wakati wa dhiki, na mshukuru wakati wa furaha. Ufanye mwaka 2012 kuwa wa furaha, Amani na faraja kwa kmtegemea yeye na kumuweka karibu yake.

  M.Mungu akujaalie riziki akufanyie wepesi kwa kila jambo, akuepusha na mitihani migumu ya maisha, Akujaalie afya njema upendo na faraja. Akujaalie chakula Bora cha Roho na sio Bora chakula.

  M.Mungu aipushe familia yako na mabaya yoote na akujaalie uvumilivu ili uweze kumuweka Shetani mbali nawe kwani kukosa uvumilivu humkaribisha shetani

  M.Mungu akujaalie nuru na mwanga katika kila unalolifanya na kukuongoza kwa kila jambo lolote upangalo. Akuepushe na mahasidi na mafisadi wawezao kufisadi na kuhasidi maisha yako kwa ujumla.

  M.Mungu akuzidishie kwa jamb lolote jema ufanyalo.M.Mungu

  EEh M.Mungu tujalie waja wako na utuepushe na Magonjwa, tujalie afya njema yenye baraka tele. tujalie heri na fanaka. M.Mungu wasamehe madhambi yao wazazi,watoto wetu na ndugu zetu waliotangulia mbele haki waepushe na adhabu ya kaburini na wafufue wakiwa miongoni mwa walio wema.

  EEh M.Mungu ifanye JF izidi kuwa chem chem ya mijadala moto moto na izidi kuwa sehemu ya kuliwazana na kudumisha undugu wetu wa mtandao. Iepushe na made za kipumbavu majungu na wajaalie MODS na wore wachangiao upeo na uwelewa wa mambo ili izidi kuwa msaada wa kizazi chetu na kizazi kijacho. Wapo moyo wale wanaotukanwa iliwasijibu matusi bali busara iwatangulie. wape busara wale walio ghadhibika na waongoze wale waliotetereka

  EEH M.Mungu tusaidie
  Amina
  Heri ya Mwaka Mpya 2012
  Ni mimi nikukumbukaye Daima Dumu kwa kuwa wewe ni sehemu ya kunifanya mimi niwe na furaha 2012
   
Loading...