Heri ya Miaka 95 ya Kuliangaza Taifa!

Heri ya Miaka 95 ya Kuliangaza Taifa!

TANESCO

Official Account
Joined
Jul 12, 2014
Posts
5,676
Reaction score
3,451
picha.jpeg

Habari Tanzaniaaaaa!

Leo tunayo furaha kubwa sana ya kusherehekea miaka 95 tangu kuanzishwa kwa shirika lako pendwa la TANESCO!

Yeeeees! Miaka 95 ya safari ya uthubutu, uvumilivu, ubunifu na mafanikio makubwa!

Kutoka kuunganisha mamilioni ya Watanzania na huduma ya umeme, kutekeleza miradi mikubwa kama Julius Nyerere Hydropower Project na Kishapu, hadi kuendeleza nishati safi ya kupikia na kuboresha utoaji huduma kwa wateja wetu!

Hakika, tumepitia mengi, tumefanya makubwa na tuna mengi zaidi ya kufanya!

TANESCO imeendelea kuliangaza Taifa, kuchochea uchumi na kuleta maendeleo katika maisha ya Watanzania!

Katika safari hii ya miaka 95, tunatoa shukrani za dhati kwa Marais wote waliopita katika awamu mbalimbali, kwa mchango wao katika kuweka misingi na kuendeleza mafanikio ya TANESCO.

Na kipekee, tunampongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa uongozi wake, maono na dhamira ya kuendelea kuhakikisha nishati ya umeme inawafikia Watanzania wote!

Hongera pia kwa Wizara ya Nishati, Bodi ya Wakurugenzi, Menejimenti na wafanyakazi wote wa TANESCO mashujaa wanaoliangaza Taifa letu kila siku!

Wow! Miaka 95! Ni mbali tumetoka, ni mengi tumefanya, na hapa tulipofika ni mafanikio ya kujivunia kweli!Lakini safari bado inaendelea!

Hongera TANESCO kwa miaka 95 ya mafanikio!

TANESCO the One Giant Institution!
 
Washukuriwe sana wakoloni wa Uingereza walianzisha shirika hili kwa kutumia sheria za India. Na walaaniwe ccm ambao wakati fulani miaka ya 90 hadi 2000 mwanzoni walitaka kuuza shirika hili na zaidi kuliletea wezi kina DOWANS, Aggreko, Symbions, IPTL, Songas, Pan Africa energy, Net Group Solutions ambao walilinyonya/wamekuwa wakilinyonya hadi kukaribia kufilisika.

Kwenye hii taarifa yenu ya miaka 95 mnatakiwa ku acknowledge huu ukweli kuwa Tanesco ni shirika lililoanzishwa na wakoloni na siyo hawa wakoloni wa baada ya 9, Dec 1961.
 
SSH amekuwa na maono gani mkuu TANESCO, acha unafiki!

Punguzeni bei ya unit, ni ghali mno, mliahidi JNHPP ikikamilika mtaboresha bei zenu ziwe rafiki kwa mtanzania wa kawaida.
Habari ndugu mteja,

tunapenda kukufahamisha kuwa ni kweli Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amekua na maono na dhamira ya kweli kuendelea kuhakikisha nishati ya umeme inawafikia Watanzania wote.

Jitihada na uwekezaji unaofanyika ni mkubwa ili kuhakikisha huduma ya umeme inapatikana kwa ubora na uhakika.^HN
 
Washukuriwe sana wakoloni wa Uingereza walianzisha shirika hili kwa kutumia sheria za India. Na walaaniwe ccm ambao wakati fulani miaka ya 90 hadi 2000 mwanzoni walitaka kuuza shirika hili na zaidi kuliletea wezi kina DOWANS, Aggreko, Symbions, IPTL, Songas, Pan Africa energy, Net Group Solutions ambao walilinyonya/wamekuwa wakilinyonya hadi kukaribia kufilisika.

Kwenye hii taarifa yenu ya miaka 95 mnatakiwa ku acknowledge huu ukweli kuwa Tanesco ni shirika lililoanzishwa na wakoloni na siyo hawa wakoloni wa baada ya 9, Dec 1961.
Mkuu umeyataja madude yote yaliyolitesa taifa hili kwa nyakati It's very unfortunate kwamba tulikuwa na viongozi walioliingiza taifa katika mikataba mibovu ya kinyonyaji,na sasa wapo wanakula pension na kuitwa waheshimiwa bila kuwajibishwa.IPTL,SYMBION,net group solutions na madude mengine kama hayo yalileta aibu kubwa katika taifa hili.Ni vile tu tumeshaona wizi na mikataba mibovu kama sehemu ya utamaduni wetu,vinginevyo waliohusika walistahili kufungwa.

Kwenu TANESCO,
Mnaposherehekea miaka 95 ya kutoa huduma kumbukeni bado kuna matatizo makubwa mawili,umeme kukatika hovyo na bei kubwa kwa wateja.Yatatueni hayo.
 
Back
Top Bottom