Heri ya Jumatano ya Majivu na kipindi cha Kwaresma

barafu

JF-Expert Member
Apr 28, 2013
6,739
32,866
image.jpeg
image.jpeg


Kesho wakristo wa baadhi ya madhehebu Tanzania,wataungana na wakristo wenginekote duniani kuadhimisha Jumatano ya majivu na kuanza kipindi cha siku 40 cha toba na kufunga cha kwaresima.Ni kipindi cha majitoleo,zaka,sadaka na kujinyima kwa wale watakaokuwa katika mfungo huo mtakatifu.Kipindi hiki ni kwa kuona wagonjwa,yatima na kusaidia wale walio ktk uhitaji.
Hapa kwetu Tanzania tutumie kipindi hiki cha siku 40 kama wakristo,kuombea Taifa letu amani na kuondoa mtanziko wa kisiasa kwa dugu zetu wa Zanzibar.Kwetu wakristo Kwaresma haimbatani sanaaa na kufunga kwa "kujulikana" bali funga yetu na utowaji wetu wa sadaka huwa ni wa "kimyakimya" maana hata maandiko yanatuasa kuwa tufungapo si lazima jirani ajue kuwa umefunga,wala utowapo sadaka kwa mkono wa kuume mkono wako wa kulia usijue hata kiasi cha sadaka ulichotoa.Ili toba yetu iwe sawa na yenye kukidhi,basi tusiwe kama wale mafarisayo na walimu wa sheria,ambao hujutapa huko na huko ili waonekane na watu wa mataifa,bali sisi tufanye mambo yetu sirini,na Mungu aliye sirini atatujazi.
Wakati tukiingia kipindi hiki cha Kwaresma,wale wa kanisa katoliki ni mwaka wa kuliombea kanisa la dunia,katika kipindi cha toka mwaka 1054 toka kanisa ligawanyike na kuwa "Kanisa la Mashariki la Orthodox" na "Kanisa la Magharibi la Roma",Wakuu wa makanisa haya kwa maana ya Patriach na Papa walikutana mara ya mwisho.Safari hii watakutana nchini Cuba wakati Papa akielekea Mexico kwa huduma ya kichungaji.Tuliombee kanisa la Mashariki na hili la Mgaharibi ili kuwe na umoja wa kikanisa wenye tija ya amani,upendo na ushirikiano wa kidunia.Nawatakia mfungo mwema wa kwaresma.
"MWANADAMU KUMBUKA KUWA U MAVUMBI NA MAVUMBINI UTARUDI....TUBUNI NA KUIAMINI INJILI"
 
Back
Top Bottom