Heri ya Christmass wana JF wote.

bonjov

Senior Member
Mar 16, 2015
122
250
Naamin kila mtu ameamka salama siku ya leo. Nachukua nafasi hii kumshukuru Mungu kutupa uzima na afya tele katika maisha yetu ya kila siku pamoja na changamoto zote tunazokutana nazo kila uchwao. Wana JF wenzangu mwaka umeisha tayari na 2017 ipo kwenye kona, hatuna budi kuishi maisha yampendezayo Mungu katika maisha yetu ya kila siku.

Kwa waliofanikiwa kimaisha hamna budi kumuomba Mungu/Mola kutunza mlicho nacho na kikue zaidi zaidi katika njia impendezayo, na ambao mambo hayajaenda vizuri hakuna kukata tamaa endelea kupigana sababu siku yako ipo yawezezekana 2017 kuna mafanikio yako na yatakuja pale tu jitahada utakapoziongeza zaidi kutunza kipato ulichonacho.

Wale wenye ndoa zao Halali mzidi kumuomba Mungu awazidishie UPENDO, AMANI, HESHIMA KWA MWENZAKO,UVUMILIVU na KUMTUMAINI yeye katika ndoa, familia yako kwa ujumla na ailinde katika kila hali, zingatieni Maombi ndio njia pekee ya kufanya ndoa yako idumu na si michepuko au kwenda kwa waganga.

Wale watufatao Mke/Mume, kumbuka kila jambo na wakati wake na uishi kwa kumtumainia Mungu katika hilo kuliko akili zenu, kumbuka ndoa ni jukumu zito sana lililo na changamoto nyingi sana. Usilazimishe mahusiano au ndoa kwa sababu ya hofu yeyote ya kimwili au kiakili maana matokeo yake mara nyingi huwa si mazuri huko mbeleni. Anza 2017 ukiwa na tumaini kubwa kwa Mungu katika juhudi zako za kutafuta mwenzi na Mungu atakupatia wa kufanana nawe.

Wanafunzi, 2017 mzidishe bidii katika masomo yenu huku mkimweka Mungu mbele, katika maneno ya vitabu vitakatifu amesema "atawafanya kuwa vichwa na si mkia", ila hayo yote yawezakana ukisali, kusoma kwa bidii na mwaka 2017 utakuwa wa kheri kwako.

Jumamosi njema, Kheri ya Christmass na Mwaka Mpya
Mungu awabariki sana
Bonjov
 

ndege JOHN

JF-Expert Member
Aug 31, 2016
7,730
2,000
Nawakumbusha tu pia kuomba Kwa ajili ya kufunguliwa vibali Kwa mwaka ujao.. Ni marufuku Kubaki maskini 2017
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar threads

Top Bottom