Hence proved. Mbeya ni kijiji kikubwa

Hence proved. Mbeya ni kijiji kikubwa

Sawyer123

Member
Joined
Jun 11, 2017
Posts
15
Reaction score
81
Nimekaa Mbeya miezi miwili sasa, ila nimenyoosha mikono. Mbeya ni likijiji likubwa, picha linaanza kila mtu kajaa vumbi kuanzia usoni hadi miguuni. Huwezi kutembea Mbeya kwa raha, bajaji zina fujo, highway hakuna sheria zinafuatwa, vumbi kama lote. Utapata mtu kapendeza town, ila chini ana soksi, jinsi vumbi linakera!

Ukija kwenye biashara, hawa watu hawana habari na customer service, utachoka wewe mteja....wahehe wanasema 'sindimgaya sida'...vifungashio vyao utalia. Yaani wanafanyia biashara kimaskini, imagine mfuko ulioisha diapers, mama muuza matunda anakupa ndo uwekee matunda. Usiponunua mfuko wako, utalishwa uchafu ufurahi.

Mbeya panasifika Kwa vyakula vingi, ila nimechoka mwili na roho kwasababu menu zao ni ugali na wali kila siku, hapo utawekewa na chainizi, maharage na nyama(nilitafuta mtori, nikaambiwa huku ukipika mtori hakuna wa kununua, ndizi za kupikwa pia siyo kitu utakikuta sana sehemu za vyakula). Au uende sehemu za kitimoto, manake huku mdudu amejaa kila Kona au ule chips na zile nyama choma zao. Kupata matunda yaliyokatwa ni shidaaaaa, nasema ni shida. Ukitaka kula varieties lazima jasho likutoke. Nikaja kuelewa kwanini wakazi wengi wa hili likijiji wanamaumbo ambayo huwezi jua kiuno Kiko wapi, matumbo yao yamejaa wanga hatari, swala la balance diet kwao ni ndoto. Ukionwa unakula matunda laZima uulizwe kama wafanya diet au. Wako na ushamba fulani hivi wakazi wa huku, kwanini Mbeya ni Jiji? Aibu naona mimi.

Mbeya katikati ya mji Ile mitaa ya Mwanjelwa Kuna watu wanapika chips kwa kutumia kuni, basi Moshi unasambaa maduka ya jirani hadi siyo poa, na Watanzania tunajua kuvumiliana, basi majirani wanavumilia. Sehemu imejaa Moshi, unakaaje hata ule chakula? Na kwamba hakuna kiongozi anayeona hiyo shida? Katikati ya mji kabisa?

Hapo sijagusia miundombinu, mipango ya mitaa, majengo yao, ni fujo TU. Halafu vijana wengi wa rika fulani hawaogi, wote wananuka harufu hiyo hiyo....wanaogopa maji hatari. Wakija kupata huduma ofisini unatamani umwambie Kaa kwanza pembeni nitakuhudumia ukiwa umekaa ili Ile harufu yake isijae kwenye dirisha lako.

Kuna mtaa street lights zinawaka kwa sensor, Kuna muda sensor zinafanya kazi, Kuna muda hazifanyi. Usiku wa Giza kabisa taa inawaka sekunde mbili inajizima. Kweli aliyefunga hizi taa ni mzima kabisa?

Baada ya kusema haya, na kwa mpangilio mbovu, niseme TU, Watanzania tunasafari ndefu ya kuishi kwa ustaarabu kwenye miji yetu. Uchafu kila sehemu, noise pollution ndo usiseme, hard waste zimetapakaa kila sehemu. Hatuoni shida?
Am out.
 
Hahhaa hotel zao nyingi za kulala chafu hapafu wahudumu wanakushangaa wewe unaeshangaa.
Kuna hotel ile ya Sokoni mwanjelwa ile gorofa na za pembeni mwake. Kidoogo GR Hotel.
Mbeya kila mwanamke baunsa 😀
 
Nimekaa Mbeya miezi miwili sasa, ila nimenyoosha mikono. Mbeya ni likijiji likubwa, picha linaanza kila mtu kajaa vumbi kuanzia usoni hadi miguuni. Huwezi kutembea Mbeya kwa raha, bajaji zina fujo, highway hakuna sheria zinafuatwa, vumbi kama lote.

Ukija kwenye biashara, hawa watu hawana habari na customer service, utachoka wewe mteja....wahehe wanasema 'sindimgaya sida'...vifungashio vyao utalia. Yaani wanafanyia biashara kimaskini, imagine mfuko ulioisha diapers, mama muuza matunda anakupa ndo uwekee matunda. Usiponunua mfuko wako, utalishwa uchafu ufurahi.

Mbeya panasifika Kwa vyakula vingi, ila nimechoka mwili na roho kwasababu menu zao ni ugali na wali kila siku, hapo utawekewa na chainizi, maharage na nyama(nilitafuta mtori, nikaambiwa huku ukipika mtori hakuna wa kununua, ndizi za kupikwa pia siyo kitu utakikuta sana sehemu za vyakula). Au uende sehemu za kitimoto, manake huku mdudu amejaa kila Kona au ule chips na zile nyama choma zao. Kupata matunda yaliyokatwa ni shidaaaaa, nasema ni shida. Ukitaka kula varieties lazima jasho likutoke. Nikaja kuelewa kwanini wakazi wengi wa hili likijiji wanamaumbo ambayo huwezi jua kiuno Kiko wapi, matumbo yao yamejaa wanga hatari, swala la balance diet kwao ni ndoto. Ukionwa unakula matunda laZima uulizwe kama wafanya diet au. Wako na ushamba fulani hivi wakazi wa huku, kwanini Mbeya ni Jiji? Aibu naona mimi.

Mbeya katikati ya mji Ile mitaa ya Mwanjelwa Kuna watu wanapika chips kwa kutumia kuni, basi Moshi unasambaa maduka ya jirani hadi siyo poa, na Watanzania tunajua kuvumiliana, basi majirani wanavumilia. Sehemu imejaa Moshi, unakaaje hata ule chakula? Na kwamba hakuna kiongozi anayeona hiyo shida? Katikati ya mji kabisa?

Hapo sijagusia miundombinu, mipango ya mitaa, majengo yao, ni fujo TU. Halafu vijana wengi wa rika fulani hawaogi, wote wananuka harufu hiyo hiyo....wanaogopa maji hatari. Wakija kupata huduma ofisini unatamani umwambie Kaa kwanza pembeni nitakuhudumia ukiwa umekaa ili Ile harufu yake isijae kwenye dirisha lako.

Kuna mtaa street lights zinawaka kwa sensor, Kuna muda sensor zinafanya kazi, Kuna muda hazifanyi. Usiku wa Giza kabisa taa inawaka sekunde mbili inajizima. Kweli aliyefunga hizi taa ni mzima kabisa?

Baada ya kusema haya, na kwa mpangilio mbovu, niseme TU, Watanzania tunasafari ndefu ya kuishi kwa ustaarabu kwenye miji yetu. Uchafu kila sehemu, noise pollution ndo usiseme, hard waste zimetapakaa kila sehemu. Hatuoni shida?
Am out.
Nenda kanywe sumu ujiue. Mbeya litaendelea kuwa Jiji lililojuu nchini hapa. Kama hujui vigezo vya TAMISEMI wanavyo promote kutoka kitongoji kuja mji mdogo, mji, manispaaa hadi Jiji basi huna hadhi ya kushiriki huu mjadala
 
Mkoa wowote ukienda kama umetokea Dar, utapaona pa ajabu sana ila ukishapazoea. Tabu za Dar, zitakufanya usipakumbuke.

Kuna mwingine aliisema vibaya sana mwanza wiki ya kwanza kufika ila kwa sasa miaka inakatika yupo huko na hata mpango wa kuhama hana.
 
Songwe Airport ipo mkoa wa Songwe.
Songwe Airport iko Mbeya. Mkoa wa Songwe hauna Airport bali wanatumia Airport iliyoko Mbeya.

Asili ya jina Songwe ni mto unaoanzia bonde la Songwe lililoko wilaya ya Chunya, mto unapita mpakani mwa Mbeya na wilaya ya Mbozi kisha unakwenda wilaya ya Ileje na kumwaga maji ziwa Nyassa
 
Hahhaa hotel zao nyingi za kulala chafu hapafu wahudumu wanakushangaa wewe unaeshangaa.
Kuna hotel ile ya Sokoni mwanjelwa ile gorofa na za pembeni mwake. Kidoogo GR Hotel.
Mbeya kila mwanamke baunsa 😀
Huu ni uongo labda unazolalaga wewe kulingana na kipato chako ila hotel na guest nyingi za Mbeya ni nzuri.

Kuhusu madem, hapa unaniandikoa kufurahisha genge bro ila kiukweli Mbeya kuna pisi kali sana bro.

Tujitahidi kuwa wakweli kwenye baadhi ya issue bro sio kukandia tu.
 
Mbeya is overrated.
Umekaa Tandale kwa Mtogole Buguruni Kwa Mnyamani, halafu unaiponda Mbeya.

Kila mtu wa Dar anajifanya anaishi Posta au Masaki!! Acheni ujinga wenu. Kwanza hamjui ni vigezo gani vinatumika kufanya mahali paitwe Jiji.

Mbeya inajengwa na wananchi wenyewe tofauti na majiji mengine ambayo yanajengwa na Serikali. Mbeya iko kwenye halmashauri 5 zenye uchumi ulio juu hapa nchini, halafu mtu wa Kazuramimba unataka kuiponda Mbeya
 
Mkoa wowote ukienda kama umetokea Dar, utapaona pa ajabu sana ila ukishapazoea. Tabu za Dar, zitakufanya usipakumbuke.

Kuna mwingine aliisema vibaya sana mwanza wiki ya kwanza kufika ila kwa sasa miaka inakatika yupo huko na hata mpango wa kuhama hana.
Kwamba Dar uswekeni ni bora zaidi ya maeneo yote nchini?
 
Huu ni uongo labda unazolalaga wewe kulingana na kipato chako ila hotel na guest nyingi za Mbeya ni nzuri.

Kuhusu madem, hapa unaniandikoa kufurahisha genge bro ila kiukweli Mbeya kuna pisi kali sana bro.

Tujitahidi kuwa wakweli kwenye baadhi ya issue bro sio kukandia tu.
Pisi Mbeya...hahahahaaa.....zote Zina rangi mbili hadi 4. Uso rangi yake, vidole rangi yake, miguu rangi yake ....ukiona pisi, ni mgeni.
 
Songwe Airport iko Mbeya. Mkoa wa Songwe hauna Airport bali wanatumia Airport iliyoko Mbeya.

Asili ya jina Songwe ni mto unaoanzia bonde la Songwe lililoko wilaya ya Chunya, mto unapita mpakani mwa Mbeya na mkoa wilaya ya Mbozi kisha unakwenda wilaya ya Ileje na kumwaga maji ziwa Nyassa
Wadanganye wasiojua.
 
Back
Top Bottom