GE2025 Hemed Suleiman: Wananchi chagueni CCM kwa maendeleo

GE2025 Hemed Suleiman: Wananchi chagueni CCM kwa maendeleo

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

PAYE

JF-Expert Member
Joined
Jun 19, 2025
Posts
354
Reaction score
395
Mgombea wa Uwakilishi Jimbo la Kiwani, Hemed Suleiman Abdulla, amesema wakati umefika kwa wananchi wa Kiwani kuchagua viongozi wanaoweza kuwatumikia na kuwaletea maendeleo jimboni humo.

Mgombea wa Uwakilishi Jimbo la Kiwani ndugu Hemed Suleiman Abdulla amesema wakati umefika kwa wa.jpg
Ameyasema hayo kwa nyakati tofauti alipozungumza na kuomba kura kwa wananchi wa vijiji vya Kendwa, Kirimdomo,Vizuke, Kichaka na Chwaka.

Amesema amekusudia kuimarisha zaidi huduma za kijamii katika jimbo la kiwani ikiwa ni pamoja na ujenzi wa hospitali kubwa ya kisasa na vituo vya Afya vitakavyotoa huduma zote za matibabu na vipimo bure pamoja na kusimamia suala zima la nidhamu kwa madaktari na wahudumu wa Afya ili wananchi waweze kupata huduma za matibabu kwa uangalizi kwa nidhamu ya hali ya juu.

Amesema azma yake ni kuhakikisha wajasiriamali na wenye vikundi vya ushirika watapatiwa mitaji, elimu ya ujasiriamali na mikopo isiyo na riba ili kukuza biashara zao pamoja kutafutiwa masoko ya uhakika ndani na nje ya nchi ili kuwa na uhaki wa kuuza biashara zao.

Sambamba na hayo Hemed amesema akichaguliwa kuwa Mwakilishi wa Jimbo la kiwani atajenga soko kubwa la kisasa katika kijiji cha Kendwa ambalo litatoa fursa kwa wafanyabisha wa kijiji hicho na vijiji jirani kufanya biashara zao katika mazingira mazuri na salama.
 
CCM na maendeleo wapi na wapi.

CCM wanachojua ni ufisadi kuteka na kuua wapinzani wao kisiasa na wanaowakosoa.

Yani tangia uhuru mpaka leo maji ni shida umeme sio wa uhakika halafu mjinga mmoja anakwambia chagua CCM kwa maendeleo!

Ushindwe kuleta tija kwa miaka zaidi ya 60 uje uweze kwa miaka mitano.

Ni kichaa tu ndo atawapa kura CCM.
 
Back
Top Bottom