mrsleo
JF-Expert Member
- Jan 13, 2014
- 2,587
- 3,886
Ngoja nikiwambia mpendwa wangu, wala sio tatizo ila hapa duniani watu tumeumbwa tofauti tofuati, na wa jinsi hiyo yako tupo, mimi niko kama wewe ni mtu wa peke yangu peke yangu tu hata marafiki huwa sipendi kuwa nao zaidi ya wawili manake sipendi kuwa na mzunguko wa watu weeengi huwa nahisi kero, na mtu kunizoea mimi ni lazma anielewe kwanza usiponielewa utasema najisikia, sina ukaribu hata na ndugu zangu labda wale wa tumbo moja tu, hapa ofisini kila siku nipo kama mgeni huko mtaani ndo kabisaaa sema tu nashukuru mtaa nnaoishi ni kila mtu ndani ya geti lake kwahiyo hakuna wa kuni jaji, hata huyu mume nilienae ni Mungu tu aliniletea manake kwa nnavyoishi ingekuwa ngumu, hata huko kwa ndugu wa mume nako kila siku nipo kama mgeni ila nashukuru wamenielewa na wananichulia kama nilivyo, kwahiyo jikubali, jipende na acha wengine pia wakukubali the way ulivyo, zamani nilikuwa nahisi kama wewe kwamba labda nna tatizo lakini kadri nikijaribu kuwa kama watu wengine nashindwa vibaya mno nakuwa kama najitesa, mwisho wa siku nikasema hivi ndivyo nilivyo cha msingi simchukii mtu wala simdharau mtu