Hela zote hizi Za kubana matumizi zimekwenda wapi

lidoda

JF-Expert Member
Apr 27, 2008
641
574
Hela zote hizi zimekwenda wapi?
1.Kama alivyodai kuwa "amepunguza" ukubwa wa Baraza la Mawaziri kubana matumizi.
2. Kafuta safari za nje
3.Kafyeka wafanyakazi hewa
4. Kafyeka wanafunzi hewa
5. Kakataza ajira mpya
Na tunaambiwa mabilioni na huenda matrilioni yameokolewa, sasa hizi hela zote zinakwenda wapi?

Wale waliopokea au kutoa mishahara hewa mbona mpaka leo hawajashitakiwa??? Wale waliofukuzwa kazi na tuliambiwa kuna watu wanapokea mishahara zaidi ya 10 mbona hatuwaoni mahakamani??

Mbona hizo mahakama za mafisadi mlizotuahaidi mngewaweka mafisadi na mlipata kura za Watanzania wengi mbona hatuzioni?
 
broo alishajibu amepunguza/Kulipa madeni mengi ambayo serikali ilikuwa inadaiwa ,ikiwemo ya walimu
 
*kafuta posho kadhaa
*kazuia bilioni 900 za malimbikizo ya madeni ya watumishi
*kapandisha kodi
*anakamua bilioni 2.5 kila mwaka kutoka kwa wanafunzi wa vyuo aliowanyima mikopo
*kazuia za wahanga kagera

tunachonufaika ni njaa, hakuna kingine..
ziko wapi ?
 
Sauti ya umma ni sauti ya Mungu haya yanayotekea sasa hivi hapa tz ni matokeo ya dhambi ya wizi wa kura.
 
Jinsi unavyoshangaa ndivyo na wengine wanashangaa vivyo hivyo.. Kundi pekee ambalo halishangai ni ... Sina buku 7ningelitaja

Bora wa buku saba kuliko wa viroba,hadi mmegeuza wabodaboda wawe walevi .
 
Hela zote hizi zimekwenda wapi?
1.Kama alivyodai kuwa "amepunguza" ukubwa wa Baraza la Mawaziri kubana matumizi.
2. Kafuta safari za nje
3.Kafyeka wafanyakazi hewa
4. Kafyeka wanafunzi hewa
5. Kakataza ajira mpya
Na tunaambiwa mabilioni na huenda matrilioni yameokolewa, sasa hizi hela zote zinakwenda wapi?

Wale waliopokea au kutoa mishahara hewa mbona mpaka leo hawajashitakiwa??? Wale waliofukuzwa kazi na tuliambiwa kuna watu wanapokea mishahara zaidi ya 10 mbona hatuwaoni mahakamani??

Mbona hizo mahakama za mafisadi mlizotuahaidi mngewaweka mafisadi na mlipata kura za Watanzania wengi mbona hatuzioni?
Hujui budget ya maendeleo imeongezwa kutoka 26℅ hadi 40℅ ya budget yote?Hujui kua elimu ya msingi kwa sasa inatolewa Bure? Hayo ni baadhi ya mambo machache tu.
 
Back
Top Bottom