Hela ya mwekezaji Simba itarudi kwa kuuza mechi Yanga, Azam

Sema waswahili tunagubu sana,hivi mo kuchukua timu ama kutochukua sisi mashabiki tunafaidika na ama tuna hasara na nini!?unakuta shabiki wa yanga anabeza mabadiliko kisa tu yamefanywa na simba muulize yeye ni kitu gani anafaidi huko yanga,atakwambia ubingwa Mara tatu!!!so what!?ubingwa unakusaidia nini kama msimu tu unaofaata baada ya ubingwa wako unashindwa hata kuwalipa mishahara wachezaji!!simba imeshakuwa kampuni that's all
Hasara utakayoipata wewe shabiki wa kawaida uliyekuwa umezoea kuingia uwanjani kiujanjaujanja, kununua jezi zilizotandazwa chini kwa 2000, uliyezoea kuaona Ndanda lazima ifungwe na Simba, uliyezoea kusikiliza mechi za Simba kwenye redio, uliyekuwa umezoea kupata ticket kwa njia za ajabuajabu, uliyekuwa unaendesha maisha yako kwenye mgongo wa Simba (majengo ya klabu, mabaunza, wauza vifaa feki vya Simba) sasa hivi ndiyo mwisho wenu. Viongozi walikuwa wanaongelea yale mazuri tu ya mfumo huu lakini hawakuwaambia mashabiki nini wategemee kutoka kwenye mfumo huu mpya wa uendeshaji mpira ambao wacheza kamali na watafuta faida ni kikwazo kikubwa kwa furaha za mashabiki.
 
Bahati mbaya sijui kutukana kama wewe usiye na breki ya maneno.
Kuwa makini siku nyingine, jifunze kuwasilisha ujumbe bila kuvunja heshima ya mtu.
Pili usidandie hoja kama hujailewa vizuri, mimi nahoji kwa mtu makini alipaswa kuhoji kipindi kile watu wanafanya ufadhili, sio kipindi hiki watu wanawekeza. Huu ni mfumo ulio wazi mtu anatoa sh 10 anategemea kupata sh 15, usichokielewa ni nini?
sorry
 
Waeleze ili uwatoe hofu wanachama wa Simba wenzio sio mimi. Mimi ninafahamu ninachokiongea.

Wamiliki wa timu siku zote hawana tabia ya kuwasikiliza mashabiki, bali wanachoangalia ni faida na hasara tu hata kama timu ikifanya vibaya. Pale Arsenal kama mashabiki wangekuwa na thamani basi mmiliki wa timu angeshamfukuza Arsene Wenger. Lakini ni kati ya timu ambazo hazina madeni na zinazotengeneza faida Ulaya kuliko timu nyingine. Kama kwa Simba kufungwa na Lipuli kutasababisha mapato mengi kwa mliki wa club basi Simba lazima ifungwe na Lipuli ikibidi (mikeka itachanika siku hiyo). Hivyo mfumo huu una uzuri lakini una ubaya wake hasa kwa mashabiki wa club.
Umeongea vizuri
 
Shabiki yeyote duniani unachotakiwa kuhoji ni performance mbaya ya team peke yake.Vitu vingine huna haki ya kuhoji.Period.
 
Ni sensa ipi ilifanyika kuonyesha simba inawashabiki wachache halaf yanga ni wengi.Au ni mambo yako ya kichoko
 
Mahaba tu hayo, kwa skili yako ni biashara gani ndani ya Simba inayoweza kugharamia yale yote aliyoyaahidi MO Simba? Mashiki wangapi Simba wanaweza Kununua jezi original ya Simba? Viingilio uwanjani washabiki wanasubiri mechi ya Simba na Yanga tu, kwa mechi nyingine wanaangalia kwenye luninga.
Ndiyo maana kuna tofauti kati yako, na MO, usipopaona wewe yeye hupaona, ndiyo maana yupo pale. Lazima tukubali mabadiliko ingawa ni magumu mwanzoni.
 
Umeongea kweli ila jambo kubwa ninalo kiulizA ni jinsi gani MO atapata Faida au kurudisha Pesa yake aliyo wekeza.....

Kama atafanikiwa kufanya vizuri kwenye michuano ya Afrika..Mazingira Ya nchi yetu kwa sasa sio rafiki katika uwekezaji kwenye soka...

Kwa mimi ilikuwa kama sisi wadau wa mpira tungepiga kelele kwanza miondo mbinu iwe mizuri hata mwekezaji akiwekeza kwenye timu ajue anakuja kupata Faida...!
Sasa Leo Mishahara ya wachezaji ya miezi miwili ni sawa na zawadi ya mshindi VPL + FA.....

Bidhaa za Simba walizo nazo sidhani kama zinafika mauzo ya 200milioni...

N:B Pia kwenye hili clubs zingine zinatakiwa zijifu ze kupitia Simba
 
Kutoruhusu asinunue 100% ni incase mmiliki kafirisika. Unaesema hawez rudisha faida unajidanganya. Simba ina mashabiki wengi sana si Tanzania tu hata nchi jirani. Amini usiamini hiyo billion 20 atairudisha in one year. Akiuza jezi Million 5 kila jezi elfu 15,00 mara miaka 5 ni sh ngapi? Get collection mechi zote nje na ndani na nje ya nchi. Akatangaza biashara yake kupitia jezi ya simba. Naona hata hiyo billion 20 kapewa tu zawadi
Mkuu una uwakika Simba anaweza kuuza Jezi Milion 5 kwa msimu mmoja?
 
Umeongea kweli ila jambo kubwa ninalo kiulizA ni jinsi gani MO atapata Faida au kurudisha Pesa yake aliyo wekeza.....

Kama atafanikiwa kufanya vizuri kwenye michuano ya Afrika..Mazingira Ya nchi yetu kwa sasa sio rafiki katika uwekezaji kwenye soka...

Kwa mimi ilikuwa kama sisi wadau wa mpira tungepiga kelele kwanza miondo mbinu iwe mizuri hata mwekezaji akiwekeza kwenye timu ajue anakuja kupata Faida...!
Sasa Leo Mishahara ya wachezaji ya miezi miwili ni sawa na zawadi ya mshindi VPL + FA.....

Bidhaa za Simba walizo nazo sidhani kama zinafika mauzo ya 200milioni...

N:B Pia kwenye hili clubs zingine zinatakiwa zijifu ze kupitia Simba
Kaka hata purchasing power ya watanzania ni ndogo sana kuweza kununua huduma za mpira. Watanzania wengi bado wanahangaika kupata chakula, maji, matibabu, malazi, na Usafiri. Wanamudu kununua bidhaa kuukuu zilizokwishatumika mahala pengine na vile bandia kutoka Asia. Ukosefu wa ajira, ujira mdogo, na kilimo, ufugaji na uvuvi duni ni chanzo cha tatizo. Kuuza mechi kunaweza kuwa chanzo muhimu cha mapato kwa muwekezaji wa mpira Tanzania hasa katika kipindi hiki ambacho kodi ni lazima ulipwe na madawa ya kulenya hakuna.
 
Biashara gani ipo Simba yenye mashabiki kidogo sana Tanzania kuliko Yanga itakayoweza kurudisha fedha za muwekezaji zaidi ya kupanga matokeo ya mechi za Simba ndani na nje ya nchi?

Kamali inaweza kuwa chanzo kikuu cha mapato ya muwekezaji wa Simba.

Tusishangilie sana kwa sasa ni mapema mno.
Nimeumia sana roho .
 
Mahaba tu hayo, kwa skili yako ni biashara gani ndani ya Simba inayoweza kugharamia yale yote aliyoyaahidi MO Simba? Mashiki wangapi Simba wanaweza Kununua jezi original ya Simba? Viingilio uwanjani washabiki wanasubiri mechi ya Simba na Yanga tu, kwa mechi nyingine wanaangalia kwenye luninga.
Usilolijua acha kuchangia, watu watang'amua uwezo wako na kukuacha kama ulivyo - Mo ni mfanyabiashara kupitia Simba atatangaza biashara zake na zitamlipa maradufu jinsi club inavyopata umaarufu ndani na nje ya nchi we unadhani Heineken wanavyoidhamini UCL wanalipwa? Wao ndio wanalipa kwani umaarufu wa Uefa Champion ni Duniani kote kupitia ilo Heineken imetambulisha na kufahamika kweli kweli ulimwenguni na imefungua branch nchi mbali mbali ikiwemo Tanzania na wanafanya biashara kweli kweli hii ndio siri ya wafanyabiashara wengi kununua bilabu mkuu
 
Ninapenda Heineken na Windhock lakini sio kutokana na UCL bali kutokana ubora wao na promotion wanazofanya kwenye mabaa mbalimbali, sidhani kama wewe unakunywa Heineken kwakuwa umeiona UCL. Watanzania wengi hawana choice bali wanaongozwa na uwezo wao wa kununua. Man U inadhaminiwa na kampuni la magari la Kimarekani la Chevrolet, wako Watanzania wanaipenda Man U lakini hawana magari ya Chevrolet.
 
Kujenga viwanja viwili vya kisasa, kufanya usajili wa wachezaji wa kisasa kabisa wanaoweza kuifunga Yanga wakati wowote, kulipa mishahara ya wachezaji hao kila mwezi, kujenga gym, kujenga hostels za kisasa, kulisha wachezaji, kutibu wachezaji na kusafirsha timu wewe unadhani inaweza kuwa hela ngapi? Purchasing power ya mashabiki wa simba unaijua? wenye uwezo wa kununua zitakazokuwa bidhaa bora original za club wanaweza kuwa wangapi?. Watakaoacha kutumia/kununua bidhaa nyingine na kuvutika kutumia bidhaa za MO (juice, sabuni, na bidhaa nyingine za MO Limited) kwasababu tu MO ndiye mdhamini wa club yao na kuacha biadhaa nyingine zinazofanana au kuzidi kwa ubora bidhaa za MO ni wangapi?
Jibu: Ni wengi wenye uwezo wa kufanya hivyo
 
Ninapenda Heineken na Windhock lakini sio kutokana na UCL bali kutokana ubora wao na promotion wanazofanya kwenye mabaa mbalimbali, sidhani kama wewe unakunywa Heineken kwakuwa umeiona UCL. Watanzania wengi hawana choice bali wanaongozwa na uwezo wao wa kununua. Man U inadhaminiwa na kampuni la magari la Kimarekani la Chevrolet, wako Watanzania wanaipenda Man U lakini hawana magari ya Chevrolet.
Biashara matangazo, leo hii mtu aliyeko kijiji angeweza kuelewa kama man u wadhamini wake wakuu ni watengeneza magari kama sio kujitangaza?
 
Hivi Nyinyi [HASHTAG]#Ndala[/HASHTAG] Kwanini Munawashwa na Mambo Ya Simba?
Wacheni Wivu Huo Kwa Kuona Simba imepiga Hatua....
Muekezaji Ni Mfanya Biashara! Kwahiyo Pakuzipata Pesa anapajua Yeye... Wewe Hayakuhusu...
 
Back
Top Bottom