Bazazi
JF-Expert Member
- Aug 18, 2008
- 2,806
- 3,524
Waungwana!
Mwezi ulopita nalikuwa Majita, Halmashauri ya Wilaya Musoma. Huko nalikutana na kisa ambacho kidogo kilinishangaza na kujisemea tu TEMBEA UONE na dunia haijaisha na maajabu yake.
Nikiwa Majita nilihudhuria msiba na kijana aliyefika kwao kwa ajili ya kumzika nduguye naye mauti kumkuta ghafla baada ya kuzika. Kijana alikuwa anaishi na mwanamke bila ndoa na walibarikiwa watoto.
Kwa kuwa hawakuwa na ndoa, FAMILIA HALISI (Nucleus Family) ilimkataa mkamwana wao. Hoja kuu ni hawamtambui kwani hawakuwahi kutoa mahari. Hali hiyo ilisababisha mtafaruku msibani kwani ilibainika familia kwa kuwa kijana wao alikuwa mtumishi, lengo ni kuhakikisha mafao yake wanayachukua na si yaende kwa familia yake.
Baada ya vikao kadhaa baina ya familia ya kijana na mkamwana walifanikiwa kusuluhisha mgogoro.
Kwa UFAHAMU wangu, iwapo kijana hajatoa MAHARI, familia ya mkamwana ndio huwa inadai kutomtambua kijana hadi wapewe Mahari. Fedha ni MWANAHARAMU!
BAZAZI NI BAZAZI na si bazazi.