Heko za Sikukuu 🎄 kwa Wadada na Wamama....

Heko za Sikukuu 🎄 kwa Wadada na Wamama....

Kasie

Platinum Member
Joined
Dec 29, 2013
Posts
22,801
Reaction score
43,177
Habari za mchana wadau...


Shukrani nyingi zimuendee Maulana kwa kunipa kibali cha kuiona siku ya leo nikiwa mzima na mwenye afya tele 🙏.

Najua kila mtu ana namna yake ya kusherehekea Sikukuu ya Krismasi. Kwa upande wangu, huwa napenda kupika pilau la viungo vizima vizima. Shurti pilau isindikizwe na kachumberi, shurbati na rosti la 🐗 lililotupiwa mbogamboga na ndizi mzuzu zilizokatwakatwa mithili ya kiepe 😋😋😋😋😋 taaaaamuuuuuu😋😋

Salamu za pekee ziwaendee wadada na wamama walioingia jikoni kupika chochote kwa ajili ya Sikukuu.

Karibuni mle kwa picha 😉.

C2FDD8D4-831A-40C5-9651-0249D220965C.jpeg


Pilau

B8BC05F0-E16A-4D66-9663-3AA0A23381EF.jpeg


Rosti 🐗 + mambogamboga.

Skukuu njema 😍.
 
Kinywajiii cha kulainisha koo hujakiweka wakati kilikuwepo
Heri ya xmass
 
Habari za mchana wadau...


Shukrani nyingi zimuendee Maulana kwa kunipa kibali cha kuiona siku ya leo nikiwa mzima na mwenye afya tele .

Najua kila mtu ana namna yake ya kusherehekea Sikukuu ya Krismasi. Kwa upande wangu, huwa napenda kupika pilau la viungo vizima vizima. Shurti pilau isindikizwe na kachumberi, shurbati na rosti la lililotupiwa mbogamboga na ndizi mzuzu zilizokatwakatwa mithili ya kiepe taaaaamuuuuuu

Salamu za pekee ziwaendee wadada na wamama walioingia jikoni kupika chochote kwa ajili ya Sikukuu.

Karibuni mle kwa picha .

View attachment 2057136

Pilau

View attachment 2057135

Rosti + mambogamboga.

Skukuu njema .

Mimi ndo wamegoma kula mchana ndo naingia sasa kujipikilisha wanachokitaka sijui nitamaliza saa ngapiila ntaleta picha
 
Mimi ndo wamegoma kula mchana ndo naingia sasa kujipikilisha wanachokitaka sijui nitamaliza saa ngapiila ntaleta picha

Weka ufundi wako wote mdada, wenyewe wanasema cooking is an art.

Wabarikiwe wataokula chakula chako.

Twasubiria picha.
 
Asante sana, kwa wote tulionhia jikoni.

Nami nimepika pilau na kitimoto safi kabisaa.
 
Kasinde mpenda vitamu.....

Nashushia chokoleti 😋😋😋😋

Ya kuvuta Mahabaaa...
3397EC91-C92D-4D0D-9F88-B3F5CC4E7782.jpeg
 
  • Thanks
Reactions: Lee
Back
Top Bottom