Heko kwa basi la Kidia One Dar es Salaam - Arusha

idaz

JF-Expert Member
Sep 1, 2013
1,099
982
Nianze kwa kumshukuru Mungu kwa kunfikisha Arusha salama,pia niweke wazi tu,hili sio tangazo la biashara ila ni experince yangu leo nilipopanda hili bus.

Mi ni msafiri wa mikoani mara nyingi sana, na huwa nikisafiri nakuwa na bus specific ambalo hupanda, pia lodge sipendi sana kubadilisha badilisha.

Mi ni mteja naweza sema regular wa KLM, basing on qualities ambazo nadhani ni za juu kuliko mabus mengi ya kwenda kaskazini. Kuna siku nilikosa nafasi KLM ilabidi nipande BM linaloenda Arusha pia, kwa kweli nilivutiwa nalo sana, kwa kujali muda ma nilifika Moshi mapema sana, so ikawa ni mteja wa both KLM na BM kulingana na uharaka na uhitaji wangu.

Leo nimefika kituoni nipande Bm, naona jamaa kapiga sim naona kaambiwa limejaa,akaniambia niende na Kidia one lililokuwa lina nafasi, sikuwa na choice. Lilipokuja, kweli ni jipya na zuri sana, nikafurahi.

Niliamka na dalili za koromeo kuwasha na kuwa kavu,nikawa nimeshapata maji moto home but nikawa naomba Mungu nifike Arusha au Ms mapema ili niweze nunua zile dawa pendekezwa,ukizingatia AC inapuliza kweeli, lazima uingie uwoga. Mungu alivyo mwema, jamaa anatangaza kati ya huduma wanazotoa kwenye bus ni pamoja na vimiminika vya moto kama kahawa, chai na tangawizi, yaani!

Nilimshkuru Mungu na nikawa nasubir huduma ianze,kweli nimepiga tangawizi moto za kutosha, na konda yule kijana nilimwambia tu ukweli siko poa so anifanyie wepesi, basi kwa weled wake alinielewa na ikawa nikumuomba tangawizi ananiletea.

Mara ya mwisho kuomba ni pale Same, aliniambia hii mashine ni ya kuwasha na kuzima so ngoja nikaiwashe, nikaona nakuwa kero mathalani nshakaribia ms, nawiwa kutoa heko kwa huu ubunifu unaoendana na hali ya sasa, wengine pia waige mfano huu.
 
Nilizoea KLM sana, mdogo wangu akanambia jaribu Kidia one ni zuri nikamwambia 'hapana litakuwa baya kama stand yake silitaki😆

Siku natakiwa kugeuka Arusha, napiga Simu KLM, BM, Esther coach wote wamejaza mpaka siku mbili mbele sikuwa na opt nyingine nikawacheck Kidia wao siku moja mbele nikakata.

Nilifika Shekilango sina hata furaha na safari maana najua naenda kupanda bora gari nifike A town..... Kuingia kwenye gari zuri, linaondoka huduma nini mambo yakawa bien. Nikachagua huduma ya chai ya maziwa......Kidia one is the best then ndio aje KLM
 
Ofisi zao ziko wapi? First class fare yao ngapi? Sikujua eti ni lazima nilitest maana nna kisafari hivi karibuni....
Kwa Arusha ni Pale Dar Express, Kw Dar ni Shekilango kama hawajahama Baada ya Stand Kuhamia Mbezi
 
Nilizoea KLM sana, mdogo wangu akanambia jaribu Kidia one ni zuri nikamwambia 'hapana litakuwa baya kama stand yake silitaki😆

Siku natakiwa kugeuka Arusha, napiga Simu KLM, BM, Esther coach wote wamejaza mpaka siku mbili mbele sikuwa na opt nyingine nikawacheck Kidia wao siku moja mbele nikakata. Nilifika Shekilango sina hata furaha na safari maana najua naenda kupanda bora gari nifike A town..... Kuingia kwenye gari zuri, linaondoka huduma nini mambo yakawa bien. Nikachagua huduma ya chai ya maziwa......Kidia one is the best then ndio aje KLM
Ulivyokosa usafiri kwanini hukunicheki PM

Nikubebe mgongoni bure kabisa??
 
Hivi kuna watu bado mnapanda KLM na mnaisifia kutoa huduma bora kweli?.

Bado mpo nyuma sana, yaani mpo nyuma sanaa. Mazoea yanakufanya usijue au kupata huduma bora 'zaidi'
Akina Mama kwa KLM huwambii Kitu.. ila Gentleman kupanda KLM ni Kuihujumu Nafsi Yako Gari inaondoka Saa 12:00 Asubuhi Dar inafika Arusha Saa 01+Jioni hata kama ni Luxury du inachosha
 
Nianze kwa kumshukuru Mungu kwa kunfikisha Arusha salama,pia niweke wazi tu,hili sio tangazo la biashara ila ni experince yangu leo nilipopanda hili bus.

Mi ni msafiri wa mikoani mara nyingi sana, na huwa nikisafiri nakuwa na bus specific ambalo hupanda,pia lodge,sipendi sana kubadilisha badilisha.

Mi ni mteja naweza sema regular wa KLM,basing on qualities ambazo nadhani ni za juu kuliko mabus mengi ya kwenda kaskazini, kuna siku nilikosa nafasi KLM ilabidi nipande BM linaloenda Ars pia,kwa kweeli nilivutiwa nalo sana,kwa kujali muda ma nilifika Ms mapema sana,so ikawa ni mteja wa both Klm na Bm kulingana na uharaka na uhitaji wangu.

Leo nimefika kituoni nipande Bm, naona jamaa kapiga sim naona kaambiwa limejaa,akaniambia niende na Kidia one lililokuwa lina nafasi,sikuwa na choice.
Lilipokuja,kweli ni jipya na zuri sana,nikafurahi.

Niliamka na dalili za koromeo kuwasha na kuwa kavu,nikawa nimeshapata maji moto home but nikawa naomba Mungu nifike Arusha au Ms mapema ili niweze nunua zile dawa pendekezwa,ukizingatia Ac inapuliza kweeli,lazma uingie uwoga.
Mungu alivyo mwema,jamaa anatangaza kati ya huduma wanazotoa kwenye bus ni pamoja na vimiminika vya moto kama kahawa,chai na tangawizi,yaani!

Nilimshkuru Mungu na nikawa nasubir huduma ianze,kweli nimepiga tangawiz moto za kutosha,na konda yule kijana,nilimwambia tu ukweli siko poa so anifanyie wepesi,basi kwa weled wake alinielewa na ikawa nikumuomba tangawizi ananiletea.

Mara ya mwisho kuomba ni pale same,aliniambia,hii mashine ni ya kuwasha na kuzima so ngoja nikaiwashe,nikaona nakuwa kero mathalani nshakaribia ms,nawiwa kutoa heko kwa huu ubunifu unaoendana na hali ya sasa,wengine pia waige mfano huu.
Hii kitu inatua Chuga saa ngapi ikinyanyuka Dar saa 12:00 asubuhi?

Mimi pamoja na huduma huwa napenda sana gari lilalofika mapema.

Mwaka 2016, nilipanda SKY LINE kutoka Chuga kwenda Dar, ilinifikisha mapema sana, ilinishusha Mbezi saa tisa mchana. Sijui kwa sasa kama bado inajali muda
 
Akina Mama kwa KLM huwambii Kitu.. ila Gentleman kupanda KLM ni Kuihujumu Nafsi Yako Gari inaondoka Saa 12:00 Asubuhi Dar inafika Arusha Saa 01+Jioni hata kama ni Luxury du inachosha
Okay.

Na unakuta kuna chombo mathalani, Tahmeed, Esta, BM nk saa 1530hrs unashuka zako na kuingia XL Longue kunywa supu.
 
Back
Top Bottom