Heko kili lager:yanga hata mlewe mpaka kuzimia mgao wa pesa za mtani jembe utakuwa hivi


Jospina

Jospina

JF-Expert Member
Joined
Apr 19, 2013
Messages
2,420
Likes
253
Points
180
Jospina

Jospina

JF-Expert Member
Joined Apr 19, 2013
2,420 253 180
Dar es Salaam: Bia ya Kilimanjaro Premium Lager imeleta msisimko mpya katika utani wa jadi kati ya mashabiki wa Simba na Yanga nchi nzima kupitia kampeni yake mpya ijulikanayo kama NANI MTANI JEMBE iliyozinduliwa leo jijini Dar es salaam na itadumu kwa muda wa miezi miwili.
Akiongea kwenye uzinduzi, George Kavishe, Meneja wa bia ya Kilimanjaro Premium Lageramesema NANI MTANI JEMBE itawapa fursa ya aina yake mashabiki wa Simba na Yanga kuonyesha mapenzi yao kwa Simba na Yanga kupitia kampeni hiyo itakayoendeshwa kwa sms ambapo Shilingi milioni 100 zitagawanywa kati ya Simba na Yanga halafu fedha hizo zitawekwa katika benki maalum mtandaoni.
• Kilimanjaro Premium Lager imetenga kiasi cha shilingi milioni 100 ambazo zitashindaniwa Simba na Yanga kupitia mashabiki wake.
• Kampeni itakapoanza kila klabu itatengewa kiasi cha shilingi milioni 50.
• Katika kipindi hicho chote mteja ambaye ni Mtani Jembe akibandua ganda la kizibo cha bia ya Kilimanjaro Premium Lager ataona namba. Ataandika jina la timu yake (SIMBA au YANGA) ikifuatiwa na namba hiyo ya kwenye kizibo kasha atatuma kwenda namba 15440 na kuipa shavu timu yake. Baada ya hapo atapata ujumbe wa kuthibitisha kwamba meseji yake imepokelewa. Kwa kufanya hivyo atakuwa amepunguza kiasi cha shilingi 1,000 kwenye akaunti ya klabu pinzani na kuiongezea klabu yake kiasi hicho cha sh. 1,000.

• Mwisho wa kampeni kama mashabiki wa Simba walipiga kura zaidi na kuichangia zaidi basi Simba itapata milioni 60 na Yanga itapata milioni 40. Na vilevile mwisho wa kampeni kama mashabiki wa Yanga walipiga kura zaidi na kuichangia zaidi basi Yanga itapata milioni 60 na Simba itapata milioni 40.

• Mteja anayetuma SMS atachajiwa kiwango cha kawaida cha kutuma sms na baada ya kutuma sms atapata sms ya uthibitisho kwamba ameipigia kura timu yake na kufanikiwa kuichangia kiasi cha shilingi 1,000. Kutokana na upigaji kura wa mashabiki, akiba ya timu wanayoshabikia itakuwa ikiongezeka au kupungua kulingana upigaji kura.
Mwisho wa kampeni fedha hizo zitakabidhiwa kwa uongozi wa kila timu kulingana na matokeo ya kura na klabu zitajiamulia namna ya kutumia fedha hizo.

Kampeni hii inatarajiwa kuongeza chachu ya ushindani kati ya mashabiki wa Simba na Yanga kwa kuwapa fursa kuonyesha mapenzi yao kwa timu zao. Mbali na kampeni ya SMS, kutakuwepo na shilingi milioni 2 ambazo mashabiki watajishindia kila wiki kwa wiki kumi kwa mashabiki watakaoshiriki zaidi. Vilevile Nani Mtani Jembe itawaburudisha mashabiki wa Simba na Yanga kupitia matukio mbalimbali mabonanza, promosheni zitakazofanyika barabarani, kwenye bar na kwenye matawi ya Simba na Yanga. Kampeni hii itafika kileleni tarehe 21 Disemba 2013 ambapo mechi mechi ya hisani itachezwa kati ya klabu hizo mbili kwenye Uwanja wa Taifa mbele ya maelfu ya mashabiki wa timu hizo.

'Mwisho wa Kampeni Kama Simba ilipiga kura zaidi itaondoka na mil 60 na Yanga 40, au Kama Yanga ilipiga kura zaidi basi itaondoka na mil 60 na Simba 40'

Angalizo;

Hii inamaana Hata Yanga mulewe mpaka mgalegale basi Simba Lazima iondoke na mil 40!

Safi sana Kilimanjaro Waache waendelee kujitoa ufahamu kwa kunywa pombe wakijua wanamkomoa simba isipate kitu
 
M

Masuke

JF-Expert Member
Joined
Feb 28, 2008
Messages
4,610
Likes
144
Points
160
M

Masuke

JF-Expert Member
Joined Feb 28, 2008
4,610 144 160
Hiyo inaitwa Vigezo na masharti kuzingatiwa.
 
kitwala

kitwala

JF-Expert Member
Joined
Aug 31, 2012
Messages
1,466
Likes
268
Points
180
kitwala

kitwala

JF-Expert Member
Joined Aug 31, 2012
1,466 268 180
Umekuja kidaku kweli baada ya kuona unapigwa mweleka.
 
Vegetarian

Vegetarian

JF-Expert Member
Joined
Apr 7, 2012
Messages
614
Likes
292
Points
80
Vegetarian

Vegetarian

JF-Expert Member
Joined Apr 7, 2012
614 292 80
Mnyama lazima atoke kapa msimu huu. We pwayanga tu,tehe tehe...
 
WABHEJASANA

WABHEJASANA

JF-Expert Member
Joined
Jun 22, 2011
Messages
4,225
Likes
8
Points
135
Age
40
WABHEJASANA

WABHEJASANA

JF-Expert Member
Joined Jun 22, 2011
4,225 8 135
Kashaga kumbe na wewe huwa unatokwa na ufahamu hivi?!,ndio maana Rage anawaendesha!!
 
Rogie

Rogie

JF-Expert Member
Joined
Nov 22, 2010
Messages
7,241
Likes
4,641
Points
280
Rogie

Rogie

JF-Expert Member
Joined Nov 22, 2010
7,241 4,641 280
Katika matangazo yao wanasema kiasi kitakachopatikana ndicho timu itapewa,hao Kilimanjaro Lager waambie walete hizo mambo zao za 60 kwa 40 ndipo watawajua mashabiki wa Yanga.
 
N

ndomyana

JF-Expert Member
Joined
Jan 24, 2012
Messages
4,748
Likes
78
Points
145
Age
39
N

ndomyana

JF-Expert Member
Joined Jan 24, 2012
4,748 78 145
Huo utani wapeleke pale kwa maharage yanga huo utanu hatuuendekezi tunachojua sisi hadi sasa tuna milioni96 mkia wana m4
 
Jospina

Jospina

JF-Expert Member
Joined
Apr 19, 2013
Messages
2,420
Likes
253
Points
180
Jospina

Jospina

JF-Expert Member
Joined Apr 19, 2013
2,420 253 180
Katika matangazo yao wanasema kiasi kitakachopatikana ndicho timu itapewa,hao Kilimanjaro Lager waambie walete hizo mambo zao za 60 kwa 40 ndipo watawajua mashabiki wa Yanga.
vigezo na masharti kuzingatiwa, we unashiriki mchezo hata hujui vigezo na masharti
 
Mphamvu

Mphamvu

JF-Expert Member
Joined
Jan 28, 2011
Messages
10,711
Likes
1,024
Points
280
Mphamvu

Mphamvu

JF-Expert Member
Joined Jan 28, 2011
10,711 1,024 280
Nasikitika kusema kuwa Kilimanjaro, au TBL wanaharibu soka la nchi hii kwa kupeleka pesa za walipakodi kule kule ambako zinafujwa kila siku na kufanyiwa mzaha.
Airtel wanawekeza pesa katika soka la watoto, wakati hawa TBL wanapeleka pesa Simba na Yanga ambako kwa vibweka vyao tangu udhamini huu uanze vinatosha kabisa kuwapokonya haki za kudhaminiwa kama kanuni za masoko na unadi wa bidhaa zinavyotaka.
 

Forum statistics

Threads 1,272,323
Members 489,918
Posts 30,447,420