kalulukalunde
JF-Expert Member
- May 27, 2016
- 1,056
- 1,083
HATIMAYE wakuu wa mikoa na wilaya wamefanikiwa kwa kiasi kikubwa kutimiza agizo la Rais John Magufuli la kukabiliana na upungufu wa madawati katika shule za msingi na sekondari ili kuhakikisha wanafunzi wanasomea katika mazingira bora.
Mapema mwaka huu, Rais Magufuli aliteua wakuu wapya wa mikoa na baada ya kuapishwa aliwaambia vigezo atakavyotumia kuwapima ni pamoja na kushughulikia tatizo la upungufu wa madawati katika shule za msingi na sekondari ili kuimarisha mazingira ya shule na kufanikisha sera ya kutoa elimu bure kuanzia elimu ya awali hadi kidato cha nne.
Rais aliwataka wakuu wa mikoa kuhakikisha kuwa hadi kufikia Juni 30 mwaka huu wawe wamefuata tatizo la madawati katika shule zote.
Kwa mujibu wa hotuba ya Waziri Mkuu wakati wa kuahirisha Bunge la 11, takwimu zinaonesha, hadi kufikia Juni 17 mwaka huu tayari kulikuwa na madawati mapya 552,630 ambayo yamepatikana kwa njia ya michango mbalimbali na hivyo kufanya shule za msingi kuwa na madawati 2,632,392 sawa na asilimia 77 ya mahitaji na sekondari zikifikisha madawati 1,395,138 sawa na asilimia 93.
Takwimu hizo zinaonesha kuwa katika shule za msingi bado yanahitajika madawati 792,949 sawa na asilimia 23 na sekondari madawati 112,785 sawa na asilimia saba. Taarifa ya Waziri Mkuu inasema kuwa halmashauri 25 kutoka mikoa 13 zimeripotiwa rasmi kukamilisha mahitaji ya madawati ya shule za msingi na halmashauri 46 kutoka mikoa 19 zimekamilisha madawati kwa shule za sekondari.
Katika hotuba hiyo ya kuahirisha Bunge iliyotolewa siku 13 kabla ya Juni 30, mwaka huu, ni wazi kuwa mikoa mingine imefanikiwa kukamilisha mradi huo kabla ya tarehe iliyopangwa na Rais.
Wakuu wa mikoa na wilaya ambao wamefanikiwa kukamilisha mradi wa madawati Juni 30 wanapaswa kupongezwa kwa kutimiza agizo la Rais kwa wakati huku tukiamini kwamba ambao walikuwa hawajamaliza nao waliongeza kasi.
Mfano ilipofika tarehe 30 Juni mikoa mbalimbali ikaripoti kukalimisha mradi wa madawati kwa shule za msingi na sekondari ambapo Jiji la Arusha likiwa limepitiliza lengo kwa kuwa na madawati ya ziada 180.
Pongezi kwa wananchi na wadau mbalimbali waliojitolea kwa hali na mali kuhakikisha madawati yanapatikana ili kuwezesha wanafunzi kusoma katika mazingira mazuri na katika viwango vinavyokubalika.
Pongezi za pekee pia kwa Rais Magufuli kwa kuweka tarehe ya kukamilisha mradi huo na kuhimiza viongozi kutumia kaulimbiu ya “Hapa Kazi Tu” ili kutekeleza kwa vitendo Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Ufanisi uliopatikana katika mkakati wa kuhakikisha kila shule inapata madawati ya kutosha umedhihirisha msemo wa Kiswahili kuwa penye nia pana njia! Baada ya kukamilika kwa mradi wa madawati, tunamuomba Rais atilie mkazo katika maeneo mengine hususan tatizo la ajira kwa vijana na uhaba wa zahanati katika kila kata ili kupunguza vifo vya wanawake na watoto wachanga vinavyotokana na uzazi.