Heko JK kwa kwa Mswada mpya wa Madini changamoto ni HIFADHI YA MAZINGIRA | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Heko JK kwa kwa Mswada mpya wa Madini changamoto ni HIFADHI YA MAZINGIRA

Discussion in 'Tech, Gadgets & Science Forum' started by saggy, Jan 5, 2010.

 1. s

  saggy Senior Member

  #1
  Jan 5, 2010
  Joined: Nov 12, 2008
  Messages: 153
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Salamu sana wana jamii wote.

  Napenda kuchukua nafasi hii kumpongeza Rais wetu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kwa hatua ya kizalendo aliyoichukua kuunda Kamati ya kupitia mikataba ya madini ni matokeo yake ni Mswada mpya wa Madini ambao utapelekwa Bungeni mwezi April mwaka huu..Ukweli ni kwamba Raisi wetu amefanya kazi nzuri na anastahili pongezi,japo kunaweza kuwa na mapungufu mengi katika mswada wenyewe lakini ni hatua muhimu sana ya kuanzia kuwasadia watanzania wote tuweze KUFAIDI matunda ya Raslimali yetu ya madini.Heko JK !!!! fanya hivyo kwa:-

  1.TANESCO
  2.TRL

  Changamoto katika mswada MPYA wa Madini:

  HIFADHI YA MAZINGIRA
  Mswada haujuweka bayana vipengele vikali ambavyo vitawabana wawekezaji katika sector hii ya madini dhidi ya Uharibifu Mkubwa wa Mazingira wakati wa shughuli za uchimbaji wa Madini na tunaomba waheshimiwa wabunge mkalijadili hili kwa kina wakati wa mjadala wa mswada huu mpya ambao umewakuna sana MAMILION ya Watanzania.


  HEKO JK HUU NI MWANZO MZURI na Tunakuunga mkono kwa Juhudi hizo na usijali wasemayo watu wewe ni mwanadamu na hauwezi kukosa mapungufu na kumbuka hata ungetenda jema gani si rahisi watu wote wakupende ndivyo wanadamu tulivyo!


  HEKO JK heko MSWADA MPYA WA MADINI!
   
 2. Sophist

  Sophist JF-Expert Member

  #2
  Jan 5, 2010
  Joined: Mar 26, 2009
  Messages: 3,087
  Likes Received: 1,733
  Trophy Points: 280
  Kama hujatumwa ila unajipendekeza; pole!
  Na kama hujui uhusiano uliopo kati ya Bwana James Cynclaire, Kikwete na Madini ya Tanzania, pole nyingine.
  Ila kama umetumwa, sina la kusema maana uko kazini, ingawa kuwa kibaraka dhidi ya nchi yako ni kazi ya hovyo.
   
 3. m

  mjukuu2009 Member

  #3
  Jan 5, 2010
  Joined: Jul 6, 2009
  Messages: 91
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  ahaa ahaaa,
  Inabidi uka ulize kwanza ile nyumba waliopanga Kahama Mining(Barrick) pale masaki ni ya nani???????


  Alafu ndio uje tuendele na mada yetu,
   
Loading...