Martin BM
Member
- Jul 2, 2020
- 16
- 22
1. Watu wenye Mafanikio na Ufanisi huwa na sifa mbili midomoni mwao: Tabasamu na Ukimya. Tabasamu husaidia kutanzua matatizo, vile Ukimya husaidia kuepuka matatizo.
2. Unaweza kuchanganya Sukari na Chumvi pamoja. Ila sisimizi huchkua Sukari tu, na kuondoka nayo, na kuacha Chumvi. Chagua marafiki wema, katika maisha yako, ili uyaboreshe na kuyaona kuwa ni matamu.
3. Ukishindwa kufanikisha ndoto zako, badilisha mbinu, usibadilishe Mola wako.
4. Kumbuka daima! Miti hupukutisha majani yake, ili istawi zaidi. Haibadilishi mizizi yake!
5. Hutafika uendako, iwapo utakatisha safari ili umrushie jiwe kila mbwa anayekubwekea njiani!
6. Wenye kukuchukia, hawatakosa la kusema! Hata wakuone unatembea juu ya bahari, watasema ni kwa sababu hujui kuogelea! Hata kama utacheza ngoma juu ya Bahari, basi watakushutumu kuwa unawarushia vumbi!
7. Panga kuishi kwa Amani na Utulivu; kwa kushughulikia mambo yako, kwa nguvu zako mwenyewe; hutakuwa mtumwa wa mtu!
8. Kumbuka daima! Usitiane miereka na nguruwe; mtachafuka nyote wawili. Ila nguruwe atafurahi na kuona raha!
9. Kumbuka, daima usibishane na mjinga! Hata werevu watashindwa kutofautisha nani ni mjinga kati yenu!