Hekaheka za kibanda umiza

Peter Mwaihola

JF-Expert Member
Jun 23, 2022
227
333
Ni takriban kilomita 300 kutoka Iringa mjini kwenda Iringa vijijini tarafa ya Idodi.

Ni Tungamalenga, tulifika huko kwa ziara ya Siku mbili. Shoo inaanza ni mchezo wa ligi kuu Tanzania Bara siku ambayo Yanga alikula 3-mtungi pale Shamba la bibi dhidi ya Kagera Sugar ya wakata miwa na Mecky Mexime 2020.

Kila goli likifungwa mbu nao wanapiga mashambulizi, mara huyu kapiga shingoni, hujakaa sawa shavuni Mara paa! Miguuni.

Ilikuwa ni kasheshe na ugeni wa ule mji nilijuta kuingia kwenye kile kibanda, nikaanza kuwaza buku niliyoitoa Kama kiingilio, nikawaza kuhusu wenyeji wa lile eneo ambao nao walikuwemo kwenye kile kibanda wao hata hawajali wamekodoa macho kwenye Luninga Kama vile hakuna mbu waliokuwa wananisonga mimi.

Nikamuuliza jamaa yangu mmoja mmatengo, hawa mbu Wana Urafiki na wenyeji au damu ya wageni inajulikana? Akabaki anacheka tu.

Mwili ukaanza kusisimka ukahisi miwasho kwa ile sumu ya wale mbu waliosikika masikioni mwangu mithiri ya ndege za kivita zinazovuma kuelekea uwanja wa mapambano.

Nilitamani mpira uishe haraka nitoke zangu nirudi kambi tulikofikia, lakini mahaba yangu kwenye mpira wa miguu yakanisukuma niendelee kutazama ile mbungi mpaka kipyenga cha mwisho.

Nikawaza hata yasiyofikirika "Kwanini mmiliki asingefunga vyandarua kuzunguka hili banda la mbao, wahenga wa ukanda wa juu kusini huita "Mabanzi" nilijicheka mwenyewe kwa kuwaza ujinga.

Kipyenga pyeee! Wananchi wametota 3-0 nikatoka zangu, nikatema mate mlangoni Thee! Siwezi kurudi tena humu washenzi wamenyonya damu yangu.

1676257618379.jpg
 
Bange ya kuvutia chooni plus gongo na ulanzi wa juzi.
 
Nyasi GANZI
 
Back
Top Bottom