dalalitz
JF-Expert Member
- Sep 6, 2013
- 3,476
- 2,086
Awali ya yote ifahamike kuwa Mie sijabobea kwenye elimu ya Biblia.
Hata hivyo,
Ni muumini mzuri wa kuhitaji kuongeza taarifa na maarifa pale inaponiruhusu.
Ni kwa mukhtadha huo basi leo nikiwa napitia luninga tofauti tofauti nikakutana na kituo cha Channel Ten kikirusha filam ya Maisha na miujiza ya Bwn. Yesu.
Moja wapo ya tukio lililonifikirisha na ambalo ningeomba kwa yoyote mwenye ufahamu wa kutosha kunidadavulia mantiki,sababu/funzo au lengo la sehemu moja wapo inayoonekana katika filam hii, Tukio ambalo Sina Shaka litakuwa linao ufafanuzi kutoka kwa waliobobea.
Nalo ni pale ambapo Bwana Yesu,
Akiwa ametangulizana na wanafunzi wake katika harakati za kusambaza Neno;
Anafika sehemu (Ugenini),
Ikiwa taarifa juu yake zikiwa zimekwishafika,
Na akichukuliwa kama si mtu mwema,
Anatokea bwana mmoja akiwa na dhamira ya kuwadhuru Yesu na wenzake,
Lakini Yesu anajipeleka mbele ya huyu bwana, kimiujiza huyu bwana anaishiwa nguvu ghafla.
Lakini hapo hapo inaelezwa kuwa;
Yule bwana
(Aliekusudia kudhuru) alijawa na pepo wabaya na hivyo Bwana Yesu kwa uwezo aliokuwa nao aliweza kuwatoa wale Mapepo na kisha kuyatupa kwa Nguruwe (Kitimoto) ambao walikuwepo sehemu hiyo na wanaonekana 'Kitimoto' hao wakitawanyika (Na Mapepo yao, eti)
Huku Yule bwana akidai sasa kuona ukweli na akiapa kujiunga na harakati za Yesu za kusambaza Neno.
Nimefuatilia hadi mwisho wa filam hiyo sijaona mahali 'Kitimoto' hao tena Wala wakitolewa (kuopolewa) dhidi
Ya yale Mapepo.
Sasa najiuliza;
Kitimoto ni Mapepo?
Au
Si Mapepo lakini wanamapepo?
Na je,
Anaekula-je?
Ufafanuzi kwa ajuae tafadhali.