Heche: Stieglers Gorge itachukua miaka 10 kujengwa, Arab Contractors haijawahi kujenga bwawa

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
39,371
2,000
Naibu Spika wa Bunge, Dk Tulia Ackson amemtaka mbunge wa Tarime Vijijini (Chadema), John Heche kusitisha mjadala kuhusu mradi wa kufua umeme wa Bonde la Mto Rufiji, Stiegler's Gorge hadi hapo Serikali itakapoleta mkataba walioingia na mhandisi wa ujenzi wa mradi huo.

Naibu Spika ametoa kauli hiyo leo Jumatano Februari 6, 2019 wakati wabunge wakichangia taarifa ya Kamati ya Nishati na Madini.

Heche amesema kuna watu wamekuwa wakiimba kama kasuku kuhusu mradi huo bila kujua umeme wake utawaka mwaka 2027

Kauli hiyo ilimfanya mbunge wa Nkasi Kaskazini (CCM), Ally Keisy kuomba kuhusu utaratibu na kumtaka Heche kufuta kauli yake kwa sababu hakuna kasuku bungeni, jambo ambalo Heche alilikubali.

Akiendelea kuchangia, Heche amesema Serikali imetenga Sh700 bilioni katika bajeti yake lakini fedha zilizokwenda ni Sh26 bilioni tu.

Amesema ili kukamilisha ujenzi wa bwawa hilo zinahitajika Sh7.1trilioni na kwamba inahitajika miaka 10 ili kukamilika.

“Arab contractors inahusika kujenga nyumba na haijawahi kujenga bwawa kokote duniani na imeamua kusub contract kwa kutafuta kampuni nyingine kuipa asilimia 80,” amesema.

Hata hivyo, Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu alisimama kwa kutumia kanuni ya 64 (1) na kusema Heche amevunja kanuni hiyo kwa kusema uongo bungeni.

Subira amesema Heche alisema uongo kuwa kampuni ya Arab imetafuta mbia lakini ukweli ni kwamba kampuni hiyo ilikuja kwenye zabuni kwa ushirikiano.

Amesema hadi sasa hajatoa asilimia 80 ya kazi alizopewa na kwamba wanamkabidhi kazi mkandarasi huyo.
Subira alimtaka Heche kufuta kauli yake hiyo jambo ambalo lilimfanya mbunge wa Kigoma Mjini (ACT Wazalendo), Zitto Kabwe kuomba kuthibitisha badala ya Heche.

Hata hivyo, Dk Tulia alimtaka Heche kufuta kauli yake ya kwamba kampuni hiyo imetafuta mbia ambaye itampa asilimia 80 ya kazi hiyo.

Akijibu hoja hiyo, Heche amemtaka kutafuta kumbukumbu rasmi za Bunge ili kuona alichokisema.

“Nimesema kampuni ya Arab haina uwezo wa kujenga mabwawa, sitatoa neno langu. Kampuni inatafuta masub- contract kujenga bwawa hili. Siondoi maneno yangu,” amesema Heche.

Kauli hiyo ilimfanya Dk Tulia kutoa uamuzi kwa kumtaka Mgalu kuleta mkataba bungeni huku Heche akitakiwa kuthibitisha ukweli wa maneno yake mara utakapofika mkataba huo.

Pia amemtaka kutoendelea na mjadala huo tena hadi suala hilo litakapomalizwa.
  
 
samurai

JF-Expert Member
Oct 16, 2010
7,819
2,000
Google ipo hao wabunge siwagoogle tu waone kama kinachosemwa ni sahihi au la. Hydro-power plant tena ya 2000MW sio kitu cha masikhara tena hao wabunge wawe makini wanapojadili suala kama hili. Projects za namna hii zinahitaji sana makampuni yenye uzoefu na kazi husika na kampuni husika iwe na mtaji wa kutosha..
 
eddy

JF-Expert Member
Dec 26, 2007
13,581
2,000
Huyu heche kasomea ualimu wa history na Geography haya ya ujenzi anayatoa wapi? kwa akili yake kazi kubwa kama ile itafanya peke yake bila sub contractors? hata Dreamliner mifumo ya computer na tv imefungwa na Toshiba, hata SGR mifumo ya umeme inafungwa na Siemens na TV zitafungwa na Toshiba, umeme wa kuendesha reli utasimamiwa na General Electric. Suala sio kampuni kuwahi jenga ni wataalamu wake wanao weledi na ujuzi wakutekeleza mradi, tunaweza wapa kampuni iliyojenga akasomba dam au mtera dam kumbe wahandisi wote walishastaafu ikawa kazi bure.
 
Hata kashifa ya trilioni 1.5 mliipinga ila leo imezaa trilioni 2.4.
 
eddy

JF-Expert Member
Dec 26, 2007
13,581
2,000
Google ipo hao wabunge siwagoogle tu waone kama kinachosemwa ni sahihi au la. Hydro-power plant tena ya 2000MW sio kitu cha masikhara tena hao wabunge wawe makini wanapojadili suala kama hili. Projects za namna hii zinahitaji sana makampuni yenye uzoefu na kazi husika na kampuni husika iwe na mtaji wa kutosha..
Nadhani kinachohitajika ni weledi na ujuzi wa wataalamu wakazi husika, mfano ni kampuni ya konoike iliyojenga Morogoro road ni tofauti kabisa na konoike iliyojenga Bagamoyo road, hii kazi sio lelemama lazima mkandarasi akusanye wenzie duniani wakune vichwa namna gani watatekeleza hii kazi kwa ufanisi.
 
sheiza

JF-Expert Member
Sep 29, 2010
5,124

Sasa ndio madhara ya kupinga..hata airport ya terminal 3..sio kampuni moja imejenga..miradi mikubwa lazima ufanye kazi na wengine..inawezekana ni kampuni ndogo ila ina historia ya kutekeleza miradi mikubwa na kwa ufanisi huku ikipata asilimia chache..cha msingi sisi tumeingia mkataba na nani na condition zikoje..hayo mengine ni ya mkandarasi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
sheiza

JF-Expert Member
Sep 29, 2010
5,124
2,000
Watathubutu!!
Ukiletwa utahamisha hoja..ila hii serikali kiboko aisee..watu walishupalia tir 1.5 wakajua itawapeleka hadi kwenye kampeni 2020..ngoma imedunda..sasa wamehamia kwa mkandarasi wa stieglers gorge..kama wasingeelezwa mkandarasi wa ndege nae aligawa tenda kwa baadhi ya vitu kwa makampuni mengine, basi nayo wangekuja nayo kama hoja kuwa airbus kagawa tenda.
Inabidi wabunge wasome sana na kujiendeleza vitu vingi ili wasitie aibu..
Hivi mara ngapi tunaona vibao vya ujenzi vinavyoonyesha makampuni hata matatu..yapo ya umeme, yapo ya lift, yapo ya plumbing..ila mkandarasi mkuu unakuta ni mmoja

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Fursa Pesa

JF-Expert Member
May 30, 2012
3,485
2,000
Naibu Spika kama vile simwelewi vile.
Mkataba ni confidential sio wa kila mtu kuusoma,kuchambua au kunyofoa/kupiga picha na kusambaza atakavyo.
Mbona mikataba ya majenzi mengine haikupelekwa bungeni?
Jibu LA swali LA Mh.Heche lilikuwa rahisi tu "Ni kweli kuwa Arab Contractors nao wanatafuta Sub- Contractors katika ujenzi huo,hasa ukizingatia kuwa ujenzi ule unahusisha fani/field nyinginezo hadi kukamilika kwake"
"Lakini pia kwa mujibu wa mkataba Main contractor jukumu lake ni kukamilisha ujenzi ule kwa wakati,ubora/viwango na thamani ya fedha iliyotengwa,hivyo suala LA yeye kutafuta washirika/sub contractors liko ndani ya uwezo wake.Cha msingi ni Sisi kama Serikali kuthibitisha weledi wa yeyote atakaye jumuika katika ujenzi huo na KUHAKIKISHA ukamilifu wake unatekelezwa kwa mujibu wa Mkataba".
Ufafanuzi hapo juu usingelimwibua tena Mh.Mbunge kuuliza swali lingine la ziada.
 
Kifaurongo

JF-Expert Member
Jan 18, 2010
3,767
2,000
Sub contractors ni jambo la kawaida kwenye miradi mikubwa ya ujenzi, Mkandara anawajibika kwenye kuhakikisha ma injinia wake wanasimamia Specs na ubora wa kazi kama mkataba unavyotaka. Maelezo ya Heche ni kana kwamba Arab contructors wameuza mradi kwa faida ya 20%
 
vipik2

JF-Expert Member
Nov 24, 2011
2,265
2,000
Naibu Spika kama vile simwelewi vile.
Mkataba ni confidential sio wa kila mtu kuusoma,kuchambua au kunyofoa/kupiga picha na kusambaza atakavyo.
Mbona mikataba ya majenzi mengine haikupelekwa bungeni?
Jibu LA swali LA Mh.Heche lilikuwa rahisi tu "Ni kweli kuwa Arab Contractors nao wanatafuta Sub- Contractors katika ujenzi huo,hasa ukizingatia kuwa ujenzi ule unahusisha fani/field nyinginezo hadi kukamilika kwake"
"Lakini pia kwa mujibu wa mkataba Main contractor jukumu lake ni kukamilisha ujenzi ule kwa wakati,ubora/viwango na thamani ya fedha iliyotengwa,hivyo suala LA yeye kutafuta washirika/sub contractors liko ndani ya uwezo wake.Cha msingi ni Sisi kama Serikali kuthibitisha weledi wa yeyote atakaye jumuika katika ujenzi huo na KUHAKIKISHA ukamilifu wake unatekelezwa kwa mujibu wa Mkataba".
Ufafanuzi hapo juu usingelimwibua tena Mh.Mbunge kuuliza swali lingine la ziada.
Yote mnayosema ni kweli lakini tujiulize kwanini Heche ang'ang'anie alichosema na Serikali ing'ang'anie kuwa Heche ni mwongo? na alichosema Naibu Spika kuwa suala hilo lisizungumuzwe mpaka hapo mkataba utakapoletwa Bungeni je kuna dalili ya huu mkataba kuletwa Bungeni wakati kuna mikataba ya Gas, Migodi hadi leo ni holaaaa.
 
Jikombe

JF-Expert Member
May 13, 2010
352
250
Naibu speka yuko sahii. Mkataba ukiletwa bungeni na kusomwa, vitaoneka hivyo vipengere/ clause za sub-contracting and the limit (%) za subs.
Arabic Contractors anaweza kuwa hajawai fanya mradi kama huo ila anaweza kuwa na verified skilled personnel wa kutosha kuweza fanya such a project pia anaweza tumia mfumo wa management construction.: yaani anagawa kazi/ subs kwa wakandarasi mbalimbali naye ana fanya overall management

Sent using Jamii Forums mobile app
 
My Son drink water

JF-Expert Member
Nov 30, 2016
4,233
2,000
Huyu heche kasomea ualimu wa history na Geography haya ya ujenzi anayatoa wapi? kwa akili yake kazi kubwa kama ile itafanya peke yake bila sub contractors? hata Dreamliner mifumo ya computer na tv imefungwa na Toshiba, hata SGR mifumo ya umeme inafungwa na Siemens na TV zitafungwa na Toshiba, umeme wa kuendesha reli utasimamiwa na General Electric. Suala sio kampuni kuwahi jenga ni wataalamu wake wanao weledi na ujuzi wakutekeleza mradi, tunaweza wapa kampuni iliyojenga akasomba dam au mtera dam kumbe wahandisi wote walishastaafu ikawa kazi bure.
Wewe umesomea nini hadi ujue kuhusu ujenzi huo?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ngatele

JF-Expert Member
Jan 25, 2011
711
1,000
Naibu Spika kama vile simwelewi vile.
Mkataba ni confidential sio wa kila mtu kuusoma,kuchambua au kunyofoa/kupiga picha na kusambaza atakavyo.
Mbona mikataba ya majenzi mengine haikupelekwa bungeni?
Jibu LA swali LA Mh.Heche lilikuwa rahisi tu "Ni kweli kuwa Arab Contractors nao wanatafuta Sub- Contractors katika ujenzi huo,hasa ukizingatia kuwa ujenzi ule unahusisha fani/field nyinginezo hadi kukamilika kwake"
"Lakini pia kwa mujibu wa mkataba Main contractor jukumu lake ni kukamilisha ujenzi ule kwa wakati,ubora/viwango na thamani ya fedha iliyotengwa,hivyo suala LA yeye kutafuta washirika/sub contractors liko ndani ya uwezo wake.Cha msingi ni Sisi kama Serikali kuthibitisha weledi wa yeyote atakaye jumuika katika ujenzi huo na KUHAKIKISHA ukamilifu wake unatekelezwa kwa mujibu wa Mkataba".
Ufafanuzi hapo juu usingelimwibua tena Mh.Mbunge kuuliza swali lingine la ziada.
But kuna kiasi cha asilimia ambacho Mkandarasi anaruhusiwa ku-subcontract, mara nyingi inakuwa si zaidi ya 10%. Zaidi ya hapo inakuwa kutoka nje ya mkataba.
 
Kinyungu

JF-Expert Member
Apr 6, 2008
9,392
2,000
Huyu heche kasomea ualimu wa history na Geography haya ya ujenzi anayatoa wapi? kwa akili yake kazi kubwa kama ile itafanya peke yake bila sub contractors? hata Dreamliner mifumo ya computer na tv imefungwa na Toshiba, hata SGR mifumo ya umeme inafungwa na Siemens na TV zitafungwa na Toshiba, umeme wa kuendesha reli utasimamiwa na General Electric. Suala sio kampuni kuwahi jenga ni wataalamu wake wanao weledi na ujuzi wakutekeleza mradi, tunaweza wapa kampuni iliyojenga akasomba dam au mtera dam kumbe wahandisi wote walishastaafu ikawa kazi bure.
Usijifanye mjuaji. Heche ana point. Kama hao Arab wameshinda tenda tunategemea wao ndiyo wafanye sehemu kubwa ya hiyo kazi na siyo wa subcontract 80% ya kazi. Wao siyo kangomba wafanye kazi. Udalali kama huo hata Caspian wangeweza
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom