PreGE2025 Heche: Msimamo wetu wa kulinda rasilimali mpaka mwisho uko pale pale, wakimfunga Lissu wengine tutasonga mbele

PreGE2025 Heche: Msimamo wetu wa kulinda rasilimali mpaka mwisho uko pale pale, wakimfunga Lissu wengine tutasonga mbele

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Cute Wife

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2023
Posts
2,786
Reaction score
7,567
Makamu Mwenyekitu CHDAEMA, John Heche akiwa anaongea na waandishi wa habari April 12, 2025 ikiwa ni baada ya kutangazwa rasmi kuwa CHADEMA kwa kutofika kusaidi kanuni za maadili ya uchaguzi wamejiondoa rasmi katika kushiriki uchaguzi mkuu 2025 ametoa msimao wa chama, ambapo amesema;




"Msimamo wetu wa kulinda rasilimali za nchi yetu za kuzipigania kwa tone la mwisho la damu yetu upo pale pale na hatutoyumba.

"Akiongeza kuwa tunaishi kwenye nchi yenye rasimili nyingi lakini watu wake ni masilikini kwa sababu ya viongozi ambao wamejigeuza kuwa miungu watu na majambazi huku wakilindwa na vyombo vya dola huku wale wanaokemea wasifanye ujambazi huo wanashughulikiwa na vyombo vya dola!"

"Heche amesema kama walidhani wakimkamata Lissu watakwenda kuomboleza, Lissu atakaa ndani wengine watasonga mbele, na wakimkata yeye (Heche) wengine wataobaki wanatakiwa kusonga mbele, na kama wakiwapiga risasi watakaobaki wasonge mbele , na kwamba hawataweza kuiua CHADEMA" - Heche Makamu Mwenyekiti CHADEMA leo Aprili 12, 2025 Mkoani Mbeya.
 
Hongereni sana wananchama wa CHADEMA kwa kuwachagua wazalendo kama hawa, kuipigania nchi yao.

Hakika sisi wazalendo wenzao na pia wapenda mabadiliko tulio wengi, tutawaunga mkono mpaka pale mkoloni mweusi atakapo tolewa madarakani! Hata ikibidi kwa nguvu ya umma.
 
Back
Top Bottom