DuaZaMama
JF-Expert Member
- Jun 2, 2025
- 1,882
- 4,129
Oktoba 4, 2025, Makamu Mwenyekiti wa Chadema (Bara), John Heche alizungumza na wananchi wa Kijiji cha Bukokwa kilichopo Halmashauri ya Buchosa, mkoani Mwanza, katika mkutano wa hadhara uliohusu kampeni ya “No Reforms, No Election”. Katika hotuba yake, Heche alisisitiza kuwa chama chake hakitaogopa vitisho vya kukamatwa, kesi au kifungo gerezani katika harakati za kudai mabadiliko ya sheria na mfumo wa uchaguzi nchini.