GE2025 Heche: Hatutajificha, tutashinda dhidi ya uovu

GE2025 Heche: Hatutajificha, tutashinda dhidi ya uovu

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
4,434
Reaction score
14,663
Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA John Heche, amesema yeye pamoja na na wenzake hawatojificha na kwamba Watashinda dhidi ya uovu unaopangwa dhidi yao.

1759587002608.png
Heche ameandika hayo leo baada ya kupokea taarifa kwamba Mahakama ya Tanzania imeombwa kutoa kibali cha kukamatwa kwa Viongozi saba wa CHADEMA na yeye akiwemo kwa madai ya kukaidi amri ya Mahakama iliyopiga marufuku mikutano ya kisiasa.

Katika maombi hayo yaliyofunguliwa na Wajumbe wa Bodi ya Wadhamini wa CHADEMA Zanzibar, Heche na wenzake wanadaiwa kuendelea kuendesha shughuli za Chama ikiwemo mikutano ya ndani na ya Waandishi wa Habari kinyume na amri iliyotolewa Juni 10, 2025.

Katika ombi hilo kwa Mahakama, Viongozi wengine wa Chama hicho waliotajwa mbali na Heche, ni John Mnyika, Rose Mayemba, Brenda Rupia, Hilda Newton, Twaha Mwaipaya na Gervas Lyenda.

Maombi hayo namba 70173 ya mwaka 2025 yamefunguliwa Mahakamani hapo na Wajumbe wawili wa Bodi ya Wadhamini CHADEMA Zanzibar, Ahmed Rashid Khamis na Maulida Anna Komu pamoja na Makamu Mwenyekiti Mstaafu, Said Issa Mohammed.
 
Back
Top Bottom