hebu tutafakari haya..... katika elimu yetu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

hebu tutafakari haya..... katika elimu yetu

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by gfsonwin, May 25, 2012.

 1. gfsonwin

  gfsonwin JF-Expert Member

  #1
  May 25, 2012
  Joined: Apr 12, 2012
  Messages: 16,943
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Asalam aleykum wana jf wote,

  Leo naomba kuja na hili japo kuwa ni baya lakin tulijadili tu labda litatupa nafasi wengine ya kujua tujipange vipi katka maisha. Nimekuwa nawaza sana juu ya elim ya Tz na inakoelekea. Siku kwa siku ufaulu wa wanafunzi umeshuka sana wengi wana faulu kwa daraja la 3&4 and yet tunasema kiwango kimeongezeka. Kibaya zaid waalim wa voda fasta hawawez hata kidogo ku coup na wanafunzi hawa wasio na maadili na wale ambao ni slow learners.

  Hali hii imefika mahali wazazi wenye hela zao wanapekleka watoto wao st schools na wasio nazo wanapelekwa st halmashauri. Waalim wamepoteza mvuto si tu kwa serikali hii bali hata kwa raia wenyewe kias kwamba wamekata tamaa na kazi yao.

  kibaya zaid sisi tulio na moyo wa kazi ambao bado tunadhani ualim ni kazi nzuri hatukutani na mazingira pendwa yanayokufanya uifurahie kazi.

  sasa je wewe kama mwana jf unatoa ushauri gani kwa waalimu wa hili taifa?
  na je unafikiri taifa lijalo litajengwa na watu wa aina gani kama hatuwez kuzalisha wataalam sisi wenyewe?
  je ungeishauri nini serikali ambayo mpaka sasa inajua kuwa mtaalam yeyote anatengenezwa akifikia chuo kiasi kwamba huku chini hali inaachwa ijiendeshe yenyewe?

  Naomba tujadili haya kwa hali ya kutafakari zaid kuliko kunyoosheana vidole na ushauri wako utasaidia sana katika kubadili hali hii.
  mods tafadhali kama mtaona uzi huu haufit hapa basi uhamishieni kwenye jukwaa la elim pasi kuharibu maana halisi.

  Mwalimu
   
 2. Kimbori

  Kimbori JF-Expert Member

  #2
  May 25, 2012
  Joined: Feb 21, 2012
  Messages: 2,724
  Likes Received: 347
  Trophy Points: 180
  Kutakana na Takwimu, ufaulu uweshuka.
  UKIANGALIA KWA KINA: kiwango cha ufaulu hakijashuka! Kilichotokea ni kwamba; kutokana na pupa za serikali, serikali imelegeza masharti kiasi kwamba waalimu na wanafunzi wasio na uwezo wanaingia shule za sekondari. Mfano Mwalimu aliyefeli kuruhusiwa kufundisha, mwanafunzi asiyejua kusoma na kuandika kuingia sekondari, ambako anafundishwa na mwalimu aliefeli, mwalimu aliyefeli anapewa darasa lenye wanafunzi 70+ ili awafundishe.

  Miaka ya nyuma ilikuwa yeyote anayeingia sekondari anastahili, hivyo wengi walikuwa wanafaulu.
  Tunakoelekea: tunaelekea nyakati ambazo kutakuwa na kundi kubwa wa wahitimu (takribani kijiji kizima) waliofeli sekondari i.e Form IV. Hivyo thamani ya elimu ya sekondari kuwa kama elimu ya darasa la saba.
  Suluhu ipo ila kunahitajika utashi wahali ya juu katika kuutekeleza ipasavyo. majibu yapo ila hakuna ujasiri wa kutekeleza.
   
 3. gfsonwin

  gfsonwin JF-Expert Member

  #3
  May 25, 2012
  Joined: Apr 12, 2012
  Messages: 16,943
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Wilguy kwanza kabisa unaposema kiwango cha elim hakija shuka unamaanisha nini? takwimu tunazosomewa na ndalichako zina incluide wanafunzi wote hata waliopata 4 ambao wanaweza kupata academic certificate hawa mara nyingi ndio wanao kwendaga vyuo vya ualim au unesi. pia wanafunzi wanaopata daraja la 1 ni wachache ukilinganisha na miaka ya nyuma na hii inathibitika unapoangalia idadi ya wahitimu with respect to daraja husika. pia siku hizi div 3 scoreres ni wengi sana kuliko 1&2.

  sasa wewe unamshauri nini hapa?
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 4. mshamu

  mshamu JF-Expert Member

  #4
  May 25, 2012
  Joined: Aug 5, 2011
  Messages: 391
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 45
  Hoja nzuri sana hii nami tu niseme kuwa serikali imeshindwa kuboresha sekta ya elimu baada ya kupeleka walimu wasio na uwezo katika shule za msingi na wanafunzi wengi kufeli wakabadili mfumo wa mitihani wakaleta maswali ya kuchagua mpaka hesabu sasa hapo wameboresha au wameboronga. Tena tusubiri na sekondari sasa hivi watafanya maswali ya kuchagua. Elimu ya msingi siyo msingi tena bali ni bora liende zamani darasa la saba angekuwa polisi au nesi sasa darasa la saba hajui kusoma na kuandika.
   
 5. gfsonwin

  gfsonwin JF-Expert Member

  #5
  May 25, 2012
  Joined: Apr 12, 2012
  Messages: 16,943
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  mshamu nafikir kuna haja ya dhat ya kujadili mustakabali wa elimu ya tz na ifanyiwe ufumbuzi mapema sana vinginevyo, hili taifa litakwisha kabisa. Tz will become an extinct nation very soon.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 6. Msambaa mkweli

  Msambaa mkweli Senior Member

  #6
  May 25, 2012
  Joined: Dec 31, 2011
  Messages: 193
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Swala la wanafunzi kufeli huu ni mkakati wa serikali, kidato cha pili wanasubiri kwanza waone matokeo, na wakiona drop out ni kubwa wanasema waendelee kdt cha 3, Je unatengemea nini matokeo ya kidato cha 4? Mwaka 2012 kdt cha kwanza inchi nzima wasiojua kusoma na kuandika idadi ni 5000 (source Mwananchi) lakini mpaka leo hakuna hatua iliyochukuliwa, wakifeli kdt cha 2 mwaka 2012 je ni nani alaumiwe? Swala la kufeli wanafunzi kwa div 3,4 na zero ni mkakati wa serikali.
   
 7. Aikasa

  Aikasa Member

  #7
  May 25, 2012
  Joined: Apr 11, 2012
  Messages: 37
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  Jamani, naomba nami niongee haya machache! Shule nyingi zinazofanya vizuri ni zile za st., ambazo walimu malipo yao mazuri na zile zinazozalisha 3 & 4 na 0 ni zile za serikali na nyingi za KATA ambazo walimu malipo yao hayaendani na hali ya maisha!
   
 8. Aikasa

  Aikasa Member

  #8
  May 25, 2012
  Joined: Apr 11, 2012
  Messages: 37
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  serikali, kama haitawathamini walimu kila siku matokeo kwa xcul za goverment yatakuwa mabaya hadi mwisho wa dunia....Hebu, linganisha malipo ya mbunge na mwalimu, kuna uwiano?
   
 9. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #9
  May 25, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Wadau mimi ni mwalim,,,,nipo sekta binafsi,,,labda niseme kwamba suala la elimu yetu kusuasua linahusisha wadau kadhaa,,,
  -serikali yenyewe,imeshindwa kuboresha mazingira ya kazi kwakweli,haitoi vifaa na hata miundombinu pia mibovu,(madawati,ofis za walim na mengineyo).
  -wazaz wanahusika kabisaaaa,,,,angalia hili la watoto kumaliza shule pasipo kujua kusoma na kuandika,hivi mtoto asiyejua kusoma na kuandika utamjua akiwa amemaliza std VII????SASA hawa wazaz huwa wanawakagua kweli watoto wao????
  Nna mwanafunz ambae namfundisha baba yake hajui anasoma shule gani,kidato gani na combination gani???je mzaz wa namna hii atajua nin maana ya elimu???,kuna wazaz tangu mwaka jana hawajaja kuchukua report za maendeleo ya watoto wao..
  -Lakini hawa watawala wetu hawaguswi kabisaaaa,maana wao watoto wao weng hawasomi hapa,kwa sasa wengi wanasomesha watoto wao Malaysia,singapore na south afrika,
  -wanafunzi wenyewe:kila mtu anakujua kizaz cha sasa,anajua kilivobadilika,,,kinakabiliwa na mambo mengi na changamoto nyingi sana,watoto wanajua na kufatikia mambo yasiyo na msingi kwao zaid ya shule,watoto wanaharibikia home na shuleni pia,nilisimamia mtihan wa taifa wa kidato cha IV mwaka jana,mwanafunz wa hapahapa mjini hawez kuchora raman ya east afrika,akachora korosho(sitanii),lakini mmoja akaniuliza,nikamuuliza:HUJAWAH KUANGALIA EASTAFRIKA TV????AU habari za afrika mashariki on itv???yupo kwenye chumba cha mtihan hapo....
   
 10. Rweye

  Rweye JF-Expert Member

  #10
  May 25, 2012
  Joined: Mar 16, 2011
  Messages: 15,029
  Likes Received: 3,052
  Trophy Points: 280
  Nitoe tu mfano,kwanini siku hizi watoto wa maraisi,mawaziri,makatibu,wakurugenzi,wabunge,wakuu wa vyuo,wakuu wa mikoa na wilaya,maras na madas hawasomi shule zetu na watoto wetu kama ilivyokuwa henzi za Mwalimu?

  Likirudi hili ndo siku elimu ya watoto wetu itakuwa nzuri na bora na mambo yote kama vitabu,waalimu na maabara vitapatikana pia.Vinginevyo hamna shortcut katika hili.
   
 11. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #11
  May 25, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  uwiano hakuna,,,,ila sasa siasa inalipa,hata magufuli alikua mwalim
   
 12. gfsonwin

  gfsonwin JF-Expert Member

  #12
  May 26, 2012
  Joined: Apr 12, 2012
  Messages: 16,943
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Bajabri mwl mwenzangu, nakubalina sana na wewew juu ya hili na binfsi naona mwanafunzi haitaj lawama bali mzazi mwl na serikali tu.
  jamani ukienda marking ndipo utajionea vituko vya mwaka manake mwanafunzi hata comprehension ina mshinda na huyu unakuta ni wa form 6. ukiangalia kwa makini utakuta form4 alinunuliwa mtihan, na mzazi yuko happy to him anajali afaulu tu hata kama hawez kutafakazri au kupambanua mambo.

  nashauri wazazi waanza mikakati ya lazima ya kuhakikisha watoto wao wanakuwa na uwezo wa kufikiri na kupambanua mambo.
  pia serikali iwekeze katika elimu kwa dhati, bajeti ya elimu iongezwe jamani na pale inapaowezekana hawa waalim hata teaching allowance tupewe.

  mashuleni nazungumzia (govt) siku hizi vitabu ni vya sayansi na hivi ni vichache sana vya masomo kama geography shule yenye wanafunz 945 unakuta kitabu 2 au 4 kwa form jamani. manafunzi atasoma geog bila geography room ama histry pasi archive? sijawahi kuona nchi iliyoendelea bila kuweka mkakati wa kutengeneza wataalamu wao wenyewe. kama hatutaweza kutengeneza wataalam wetu tujue kabisa kuwa elimu hii tunaiua natural death.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 13. gfsonwin

  gfsonwin JF-Expert Member

  #13
  May 26, 2012
  Joined: Apr 12, 2012
  Messages: 16,943
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Aikasa hayo unayosema ni kweli kabisa lakn je tutasomesha bila miundombinu mizuri na yenye tija? mathali sidhan kama kuna shue zenye archives au geography room kwa siku za leo.sioni kama mashuleni kuna library furnished, agriculture rooms hakuna, maabara za sayans zipo kwa uchache sana na vifaa hakuna vitabu hakuna hata kama utapewa mshahara milion 8 kwa mwezi utawezaje kupandisha uelewa wa wanafunzi hali vitenea kazi hakuna?
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 14. E

  Eno New Member

  #14
  May 26, 2012
  Joined: Mar 26, 2012
  Messages: 2
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Jamani sisi walimu wanafunzi tunateseka sana sijui serikali iko wapi! Leo tumefunga chuo lakini barua yamatumizi inazid kiwango cha ada wanachuo 789 tuna takiwa kutoa milion 70 kwa ajili ya miundo mbinu na matibabu hali yakuwa chuo nimali ya serikali na wengi wetu watoto wawa kulima mbaya zaid ukisema unatishiwa kufukuswa jamani tusaidieni, butimba mwanza huku.
   
Loading...