Hebu tu-rewind mkanda..Wema Sepetu na marehemu Steven Kanumba..(R.I.P)

queenkami, nakupenda bure shosti.
Achana na hao wanaokupa ushauri hewa.
Wameona wema kawazidi.
Hahaha!
 
Last edited by a moderator:
Y kuhamisha private life kuipeleka kwenye public ndio ushamba hasa alofanya domokaya. Alasfu eti anamshauri amshauri kwanza domo ndo aje kwa Wema.

wema unachekesha leo unamwita diamond domokaya wakati kakunyonya na kukula kabang vya kutosha, kweli wema we hatari...btw naitamani sana 0713 yako usipime kila nikiona kabang yako moyo badunda dunda...
 
Wema mi nakufagi sana nilishangaa yaan we domokaya ndo linakukosesha amani? we ni mrembo unavutia achana na sen*ge hilo linatabia za kiumbea kama jike.kula maisha mamii kwa raha zako mashabik wako tupo.kwanza cjui kwa nn hilo domokaja wala huendan nalo lisikupe mikosi achana nalo.
 
Baada ya kusoma ujumbe wa wema wa instagram kuwa watu wamuonee huruma kwa kweli nilipata huruma,ila baada ya kutafakari kidogo niliona huyu dada yeye mwenyewe ndiye anayehitaji kujionea huruma maana yote yanayomtokea ni mazao ya mbegu alizopanda mwenyewe.

Watu wengi tunaonekana kumtukana Diamond sababu ya yeye kumrekodi Wema lakini hakuna anayejiuliza imekuaje hadi Diamond kufikia kuchukua uamuzi huo.Watu wanaonekana kumchukia Diamond kwa kitendo cha kumrekodi Wema ambaye ni EX wake lakini wamesahau kuwa marehemu Steven Kanumba (Pumzika kwa AMani) baada ya kuchoshwa na vituko alivyokua akifanyiwa na wema alifikia hatua ya kumpeleka Wema Sepetu Selo ambako alilala kwa wiki nzima sijui siku mbili(sikumbuki vizuri).Wakati huo nao wema alikua ni EX wa marehemu Steven.

Iweje mwanamke huyo huyo mmoja yeye tu ndiye anakua na matatizo na ma-ex wake?Mbona Diamond hajawarekodi hao ma-ex wake wengine tunaosikia alitoka nao akawaacha?au mbona kanumba hakuwapeleka lupango ma-ex wake wengine aje kumpeleka huyu wema tu?.

Katika maisha kabla yakumhukumu mtu vibaya kutokana na kitendo alichofanya ni vizuri kujiuliza kwanza kwanini mtu huyo akafanya kitu alichofanya.Mfano watu wanamsengenya Diamond kwa kitendo cha kukataa hela za wema ktk show ya diamonds are forever.Kumbukeni Diamond ana nafasi ya kujua mambo mengi ya Wema ambayo mimi na wewe hatuwezi kuyajua.Hivi kwanini mtu usijiambie kwamba labda diamond anajua kwamba labda Wema´s money stinks ndo maana akazikataa.Mfano kama wema anatembea na vibabu halafu likabumburuka magazetini na wakati huo huo Diamond anafurahia kutuzwa hela na wema si haters wake watamtungia jina na mario?Au tunajuaje kuwa labda diamond anajua kuwa njia ambazo wema anapatia pesa zake ni njia chafu kiasi kwamba mkono wake ulishindwa kunyanyuka kupokea hizo pesa.Au hamjui kwamba kuna wanadamu wanafanyishwa mambo ya ajabu kiasi kwamba ukiyajua wanayofanya kupata pesa zao hata wakikununulia soda huwezi kunywa.Hivyo tusimlaumu tu Diamond kisa tunachukia mafanikio yake.
Sisemi kwamba wema anapata pesa zake kwa njia njafu nimetoa tu mfano.

Mimi nafikiri kumtukana Diamond hakusaidii,kinachotakiwa ni kumshauri wema na kumweleza ukweli.Sana sana mkimtukana Diamond mjue kila tusi mnalomtukana Diamond linarudi mara tatu kwa wema kwa sababu nyie mnaomtukana Diamond nyie ndio mnaomuona mshamba,limbukeni sijui hivi na vile ila sasa huyo mrembo wenu yeye hakuyaona hayo yoote mnayomkosoa ex wake.Sasa limbukeni na mshamba na anayempenda limbukeni na mshamba ni nani kati yao ni limbukeni na mshamba zaidi.

Classy ladies date classy gentlemen na trashy ladies date trashy gents.Ndege wa rangi moja huruka pamoja kwa hiyo Wema hana umaana wowote wa kumshinda Diamond.Mkitaka kumfanya Wema wa maana automaticaly inabidi na Diamond nae mkubali tu kuwa ni wa maana na mkitaka kumfanya diamond aonekane ni takataka inabidi tu mkubali kuwa hata wema ni takataka.Tena hiyo mnayoiona takataka ilimvalisha hadi pete na akaikubali,angekua anajitambua ni wa maana si angeikataa!Takataka hupendana na takataka nyenzao na wa maana huwa na wa maana wenzao.Tuko lini nzi akapeperuka kwenye kundi la vipepeo jamani.

Jamani tuache kumshambulia kijana mwenzetu Diamond tuangalie huku na huku maana watu wamefikia hatua ya kuhamasisha watu wasiende kwenye concert zake,sio vizuri huko ni kutaka kumharibia kijana mwenzetu maisha yake bila sababu.

Pia wanaosema eti wema kampa jina na umaarufu Diamond sio kweli,maana kila mtu anajua kuwa wema anapenda kutoka na watu maarufu sasa angemjulia wapi Diamond kama Diamond angekua sio maarufu tayari?

Na nyie mnaosema eti Wema ana nyota kali kiasi kwamba ukitoka nae lazima uwe juu ndio hamjui kabisa mnachoongea.Wema alitoka na TID,MR BLUE,JUMBE na yule chalz nini sijui wa twanga pepeta.Sasa kama huyo wema ana nguvu za kungarisha watu mbona hao ma-ex wake wote wamejichokea maskini ya mungu hata hawajulikani wanapumulia wapi.

Msururu wa wasanii wengi waliotoka na wema wamejichokea majina yao yamekufa kwa hiyo mtu mwingine anaweza kusema wema ana mkosi ndio maana wasanii wengi waliotoka nae majina yao yamekufa.

Na nyie mnaodai wema ndo kampa jina Diamond ina maana basi kuwa hata Kanumba alifika pale alipofika sababu alitembea na wema?Sababu ninachokumbuka mimi kanumba ndie aliyemrudisha wema kwenye msimamo.

Mimi siamini katika mambo ya nyota,hivyo siamini kuwa wema ana nyota kali inayoweza kumpa mtu umaarufu na wala siamini kuwa wema ana mikosi inayoweza kupoteza jina la msanii.Mimi ninaamini msanii kama Diamond anapata mafanikio kutokana na juhudi,ubunifu na kipaji alichopewa na Mungu na waliopoteza majina wamepoteza sababu wamekua wazembe katika kazi zao.

Naona watu wamerogwa na wema kisa alitoa 13M kumsaidia Kajala.Hata mimi nilifurahishwa sana na utu ambao wema alionesha,kwa hili sitaacha kumsifia dada wa watu maana wapo wengi wenye mahela lakini wasingeweza kufanya wema na ubinadamu alioufanya wema.

Mimi ninampenda Wema na movie zake nitaendelea kuangalia na Diamond vile vile ninampenda na nyimbo zake sitaacha kusikiliza.
Hata hivyo naona watanzania wenzangu tunashabikia tu kuwa wema ana mihela..wema ana mihela..ndio ni kweli mwenzetu siku za hivi karibuni amekua akijitahidi sana kutuonesha kuwa ana mihela.Swali ni je anazipata wapi?Najua watu watasema ni umbea na kumind business za watu kutaka kujua anakopatia pesa.ni sawa..na sio sawa kutegemea na ubongo wa mtu.

Wema ni kioo ch jamii,wasichana wengi wataweza hata kuacha shule ili waingie bongo movie ili wawe tajiri kama wema,lakini ukweli ni kwamba bongo movie haina uwezo wa kumfanya msanii amiliki nyumba ya 400m, 13M ya Kajala,kampuni ya zaidi ya 70m,movie premier ya over 30m,nguo za mbwa za 6m,kugawa mihela kwenye sherehe,kubadilisha magari na mambo mengine kede wa kede ya kutumia pesa nyingi.

Anapoyatoa mahela yake atajijua mwenyewe, kama anatoka na vibabu,kama anauza unga au kufanya vitu vingine haramu ipo siku nguvu ya dola itafanya kazi yake na sisi tutasoma magazetini kama tulivyosoma habari za yule mume wa model Jack cliff.Kama ni bongo movie ndio inayomlipa hivyo basi ni vizuri na ninampa hongera na ninamtakia kila la heri na aelekeze nguvu zaidi kwenye sanaa yake ili apate mafanikio zaidi ya hayo.

Mimi sishabikii kitendo cha Diamond ila Wema ni wakati wa yeye kujiheshimu kama mwanamke.Mimi kama mwanamke mwenzio nimeona nikupe ukweli wako,sababu nina kupenda na ninataka kuona ukifanya mambo makubwa zaidi ndio maana sijataka kukupa misifa isiyo na mbele wala nyuma wakati naona kabisa usipoambiwa ukweli mwisho wako utakua mbaya.

Angekua anajiheshimu kama kina Jokate sidhani kama huyo Diamond angemfanyia dharau ya kiasi hicho,mwanamke gani kila siku wewe tu ufanye vitu vyakufanya wanawake wote tuonekane akili zetu za panzi!!?? Maana mara leo uoneshe makalio yako,wewe upigwe picha ukiliwa denda,wewe upelekwe selo,makalio yako yako wazii mitandaoni,kila mtanzania mkubwa kwa mdogo anajua makalio yako yakoje in nudity form,wewe hivi leo wewe vile jana halafu utake tukuonee huruma,ndio unatia huruma ila anza kujihurumia mwenyewe then ndio utake dunia ikihurumie maana usipojihurumia kwa kuanza kujiheshimu ipo siku utakutana na mwanaume mwehu zaidi ya Diamond na Kanumba akufanye kitu ambayo ku-recover itakua nguvu.

KIROHO SAFI TU.
Wewe Dada akili zako ni ndogo sawa na huyu Domo Chapati. Attention seeker.

[h=5]



Diamond"Ni kweli Nilimrecodi Wema ila Sioni kosa Langu Siwezi Mwomba Msamaha"





Skendo iliyokuwa ikiendelea mtaani kuhusu msanii Diamond na tuhuma za kumrekodi aliyekuwa mpenzi wake wa zamani mwanadada Wema Sepetu, msanii huyo amekir kuwa ni kweli alifanya tuhuma hizo kwaajili ya kulinda penzi lake.





“Hivi karibuni Wema amekuwa akinipakazia mbovu kwa mpenzi wangu Penny akiwa na leno la kutaka kuni haribia juu ya mimi na mpenzi wangu, nilichukia sana kwahiyo siku alivyoamua kunipigia simu ndipo niliamua kumrekodi ili kumsikilizisha Penny ambaye alikuwa haniamoni kabisa” Alifunguka Diamond.





Sauti hiyo ambayo ilitoka kwa Wema Sepetu ikiwa inambembeleza Diamond waweze kurudiana pamoja kwakuwa bado anampenda, Diamond amekiri kuirekodi hiyo sauti lakini amekana kuisambaza mitaani na hajui nani kafanya hivyo.





“Lengo langu kubwa ilikuwa ni kurekodi sauti hiyo na kumsikilizisha Penny, sasa ambaye aliichukua na kuisambaza mitaani sijui ni nani, lakini hata mi sikujisikia vizuri nilipoisikia mitaani maana sikupenda hali iwe hivyo lakini ndo sina jinsi” aliongeza Diamond.





Baada ya kukiri kujutia, Diamond aliambiwa aombe msamaha Live ili Wema asikie ila alikataa na kusema hawezi kumuomba msamaha maana haoni kosa lake.

[/h]
 
wema unachekesha leo unamwita diamond domokaya wakati kakunyonya na kukula kabang vya kutosha, kweli wema we hatari...btw naitamani sana 0713 yako usipime kila nikiona kabang yako moyo badunda dunda...
Ukiambiwa una akili kama za Diamond ni tusi kubwa, na ukiambiwa una Domo kama la Diamond pigana mpaka ufe.

Sasa naanza kuamini si bure, kwa 100% hili Domo linatumia jina la Wema Sepetu kujipigia Promo. huyu ni Falla tu.
 
diamond piga kazi na nenda kny ibada umuombe mungu akuepushe na hawa wakorofi wa mtandaoni,roho mbaya tu......eti tusiende kny show yake,WOMAN WHO THE HELL DO YOU THINK YOU ARE???show ya diamond tunaenda na VITENGE VYAKO HATUNUNUI.....pumbafu kabisa
 
diamond piga kazi na nenda kny ibada umuombe mungu akuepushe na hawa wakorofi wa mtandaoni,roho mbaya tu......eti tusiende kny show yake,WOMAN WHO THE HELL DO YOU THINK YOU ARE???show ya diamond tunaenda na VITENGE VYAKO HATUNUNUI.....pumbafu kabisa
Labda kwenye ibada za majini na Mungu wa Lucifer.
 
Tunashukuru kwa kutu riwaindia mkanda wa kanimba na wema

ila nahisi it was supposed to be" mkanda wa Wema na daimond" na siyo Kanumba
 
mmmmmmmmmmh tunashukuru kwa kutu rewaindia mkanda

lakini mkanda uliotakiwa kuu rewind nahisi ulitakiwa uwe wa diamond na wema.....

kanumba ungem mention tu ka kina jumbe
 
Mimi nafikiri kumtukana Diamond hakusaidii,kinachotakiwa ni kumshauri wema na kumweleza ukweli.Sana sana mkimtukana Diamond mjue kila tusi mnalomtukana Diamond linarudi mara tatu kwa wema kwa sababu nyie mnaomtukana Diamond nyie ndio mnaomuona mshamba,limbukeni sijui hivi na vile ila sasa huyo mrembo wenu yeye hakuyaona hayo yoote mnayomkosoa ex wake.Sasa limbukeni na mshamba na anayempenda limbukeni na mshamba ni nani kati yao ni limbukeni na mshamba zaidi.

Classy ladies date classy gentlemen na trashy ladies date trashy gents.Ndege wa rangi moja huruka pamoja kwa hiyo Wema hana umaana wowote wa kumshinda Diamond.Mkitaka kumfanya Wema wa maana automaticaly inabidi na Diamond nae mkubali tu kuwa ni wa maana na mkitaka kumfanya diamond aonekane ni takataka inabidi tu mkubali kuwa hata wema ni takataka.Tena hiyo mnayoiona takataka ilimvalisha hadi pete na akaikubali,angekua anajitambua ni wa maana si angeikataa!Takataka hupendana na takataka nyenzao na wa maana huwa na wa maana wenzao.Tuko lini nzi akapeperuka kwenye kundi la vipepeo jamani.

KIROHO SAFI TU.

hakika nimependa haya maneno.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom