Hoja kama hizi ni nzuri. Zinayufundisha na kutupa fursa za kutafakari. Hoja hizi zinapanua mawazo.
Mfano mzuri umetoa. Je, Tanzania inajiendesha inavyotakiwa nchi kujiendesha?
Mfumo wa Uongozi halisi.
Chama kilitakiwa kiwe peke yake
Serikali ilitakiwa iwe peke yake.
Sawa na hardware na software.
Lakini Tanzania yetu kumekuwa na mseto. Software ndio hiyo hardware, na hardware ndio hiyo operating system na ndio hiyo hiyo pia anti virus. Itawezekana kweli na ndio maana tunajikuta kwenye hali ngumu.
Tumeona "Hamu Binafsi" ndizo zinaweza kuwa Sera zitakazo tawala nchi yetu.
Hatuwezi kwenda kwenye kiwanda kinachotengeneza dawa tukataka kujitibu Ugonjwa. Kuna Hospitali, kuna Dakitari, Kuna Mahabara, kila Ugonjwa na dawa yake na pia kuna wauguzi. Leo hii Kiwanda cha dawa ndio Hospitali, Ndio Maabara, ndio Dakitari, ndio Wauguzi, mgonjwa (mwananchi) atapona?
Wakati Wazungu wametumia sayansi na teknolojia kundundua dawa ya Ukwimu na Kisukari, sisi tunakimbilia kikombe cha Babu.
Kwenye karne ya 21?
Hapa hatukosoi, hapa tunakumbushana na kuelimishana.
Kuna mfano bora wa Uongozi zaidi ya ule tutakaojifundisha kutoka SADC, kwa wakati huu?
Kwanini turudi na tusiegemee huko?
Tumejikita, kushindania au kufuata mifano au kutaka kuwa kama nchi za maziwa makuu, nchi zenye historia ya migogoro na zisizokuwa na nidhamu au mifano mizuri ya Uongozi. Nchi zisizothamini utu na thamani ya Ubinaadamu.
Tusisahau Azimio 2076 la Baraza kuu la Usalama la Umoja wa Mataifa, ndio lililoidhinisha kupeleka wanajeshi wetu Congo kulinda amani. Wanajeshi wetu hawakwenda kujenga viwanda vya Ice Cream huko.
Tumeisahau Pretoria "Economical Giant" wa bara hili. Na Pretoria ndio iko madarakani leo kupitia Ubarikio wetu na mchango wetu wa awali.
Pretoria ni watu safi, Waaminifu, Kiuchumi, Kiusalama, Kisiasa na hata katika sanaa na utamaduni wa Mwafrika. Ni sehemu Mwafrika anaweza kutimiza ndoto yake. Ni watu wanatupenda na kutuelewa.
Mcheza kwao hutunzwa.