Ahsante mwalimu, kwa darasa hili maridhawa la Upendo............... Sina cha kuongeza, umemaliza mkuuTangu tumezaliwa tumesikia neno UPENDO,mimi binafsi wazazi wala shule sikuwahi kuambiwa maana ya hili neno!Nilikuja kulitafuta mwenyewe!Nakumbuka kwenye mafundisho ya dini tulikua tunaambiwa tupendane,nyumbani hivyohivyo.Nilipokua nikajua kuna kumpenda mwanamke,hawa walionieleza kuhusu upendo hawakuwahi kunifafanulia,nikajiuliza kuna tofauti kati ya kumpenda mama yangu na jirani yangu pia vipi kuhusu mwanamke?Nilibaki mtupu!Lakini niliamua kutafuta maana na nimepata tafsiri hii;Upendo ni kumkubali mtu bila masharti.Yaani kama ni mwanao sio mpaka afaulu mtihani ndo apendwe,kama ni jirani rio mpaka awe na pesa ndo apendwe,upendo ni kutoa tu bila kujali unaempenda anakurudishia nini,yaani wewe ni kutoa tu,na ukiwa hivi hautaona shida kuishi na mke/mume mkorofi.ANGALIZO,kwenye ndoa ni hatari kuishi na mtu mwenye tabia za hatari kama kupiga,kufuja,kudhalilisha n.k,hapa unatakiwa usitishe haya mahusiano,kufanya hivi haimaanishi unamchukia.Unaweza ukatengana nae lakini mkawa pamoja kwenye mambo mengine.Sasa kama niko sahihi,kuna upendo siku hizi?Na kama siko sahihi,tafsiri yako ni muhimu hapa,tuambie......
Upo kwa tafsiri ipi?Yako au yangu?
Upo kwa tafsiri ipi?Yako au yangu?
Dada Asha,u hali gani?,.....Upendo halisi haushuki wala hauishi,unaoisha ni ule upendo wa "kutegemea something in return"it means kwamba kama hujanifanyia hiki au kile sitakupenda,huu ni upendo wa masharti,na pia sio upendo!Tena hali hii kwenye uhusiano ndo kubwa,kiukweli hii ni mihemko ambayo hukujia baada ya mtu kukutendea jambo fulani au mtu kuwa na mtazamo/muonekano fulani[makalio,miguu ya bia,sauti,mrefu,mtanashati n.k]mihemko inayotokana na hali hizi huisha pale unapokinai kilichokuvuta au kinapotoweka!Upendo hauna masharti haya,haujali kama unarudisha matusi,au chuchu saa sita zimelala baada ya kunyonywa na mtoto.Mwenye upendo anaangalia ubinadamu tu.
Upo kwa tafsiri ipi?Yako au yangu?
Upendo ni kumkubali mtu bila masharti.
ANGALIZO, kwenye ndoa ni hatari kuishi na mtu mwenye tabia za hatari kama kupiga,kufuja,kudhalilisha n.k,hapa unatakiwa usitishe haya mahusiano,kufanya hivi haimaanishi unamchukia.
Kama tutaangalia kwenye dondoo hizi mbili, kuna mambo yanachanganya - kumpenda mtu bila masharti na upendo wa kutegemmea something in return". Nahisi tusijidanganye, mwenye tabia chafu hapendeki (kama zilizotajwa hapo juu kwenye ndoa, au kwa rafiki mwongo, virungu, mbea, mchonganishi n.k, au mtoto mwizi, mwivu, mlevi n.k.) Anayependa katika mahusiano yoyote, iwe baina ya wapenzi, rafiki au familia, hutegemea kurejeshewa upendo, ikiwa atachokuwa anavuna ni maudhi na maumivu upendo hupungua na pengine huisha kabisa......Upendo halisi haushuki wala hauishi,unaoisha ni ule upendo wa "kutegemea something in return"it means kwamba kama hujanifanyia hiki au kile sitakupenda.