Hebu sikieni haya ya Mlima K'njaro | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hebu sikieni haya ya Mlima K'njaro

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by EPA TZ, Jan 17, 2012.

 1. EPA TZ

  EPA TZ Member

  #1
  Jan 17, 2012
  Joined: Jan 16, 2012
  Messages: 32
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ANGALIA MAJIBU YA HAO VIGOGO WA KINAPA/TANAPA

  Na Restuta James, aliyekuwa Moshi

  JEURI na hujuma zinazofanywa na askari wanaolinda mlima Kilimanjaro zinahatarisha maliasili hiyo kutokana na uhalifu mkubwa wa upasuaji wa mbao na ukataji wa miti unaofanyika ndani ya hifadhi ya msitu wa mlima huo.


  Uchunguzi wa NIPASHE uliofanywa kwa wiki moja kuanzia Januari 3, mwaka huu umebaini kwamba upasuaji huo wa mbao unafanyika mchana na usiku; kilometa chache kutoka kwenye geti la askari wa Mamlaka ya Hifadhi ya Mlima Kilimanjaro (Kinapa), katika kila njia rasmi zinazoingia mlimani.

  Mbali ya upasuaji wa mbao, wananchi wa vijiji vya karibu wanachunga mifugo yao ndani ya hifadhi, wakiwamo ng'ombe na mbuzi ambao hula hata miti midogo inayoanza kuchipua.

  NIPASHE ilishuhudia sehemu kubwa ya msitu wa hifadhi hiyo ukiwa umebaki vichaka na maeneo ya wazi badala ya miti kama ilivyokuwa imezoeleka miaka ya nyuma.

  Pia NIPASHE ambayo iliingia kwenye hifadhi hiyo, ilishuhudia ukataji wa miti na upasuaji wa mbao ukifanywa nyakati hizo; na katika maeneo mengine, wahalifu hao walikimbia walipohisi kuona watu wasiowafahamu.

  Baadhi ya wananchi wanaoishi katika vijiji vinavyopakana na msitu ambao walizungumza na NIPASHE walieleza kwamba wahalifu wanaovuna miti na kupasua mbao katikati ya hifadhi wanafahamika, lakini wanalindwa na askari wanaolinda hifadhi hiyo.

  Mkazi wa Kijiji cha Kifuni, Kata ya Kibosho Magharibi, Wilaya ya Moshi Vijijini, ambaye hakutaka jina lake liandikwe gazetini, aliliambia NIPASHE kwamba, baadhi ya watuhumiwa ni viongozi wa kijiji ambao ni marafiki wa karibu wa askari hao.

  Alisema wananchi wamekuwa wakitoa taarifa za uhalifu huo kwa askari, lakini watuhumiwa hawachukuliwi hatua zozote.

  Alisema hali hiyo imesababisha uharibifu mkubwa wa vyanzo vya maji na kusababisha mito mingi kukauka hivyo kuathiri shughuli za kiuchumi kijijini hapo.

  Januari 3, mwaka huu, NIPASHE ilifika kwenye geti la kuingia katika mlima huo la Umbwe saa 6.00 mchana baada ya kufanya uchunguzi ndani ya hifadhi.

  Ilikutana na askari wawili ambao walikanusha kuwapo uharibifu huo na kuwazuia waandishi kuingia kwenye hifadhi hadi watakapopata kibali cha Kinapa.

  “Hatusemi kwamba kuna upasuaji unaofanyika. Huo ni uvumi tu, watu wanawaletea. Lakini kama mnataka kuingia msituni inabidi mpate kibali cha Kinapa na wao ndio wanaweza kusema kama kweli kuna kitu kama hicho hapa,” alisema askari aliyetambulika kama mkuu wa kituo hicho bila kutaja jina lake.

  Askari huyo alimtaka mwandishi wa habari hizi awasiliane na Kinapa ama Mamlaka ya Hifadhi za Taifa (Tanapa) kwa ufafanuzi zaidi.

  Kutokana na hali hiyo, NIPASHE ililazimika kwenda kwa Diwani wa Kata ya Kibosho Magharibi (CCM), Claud Olomi, ambaye alithibitisha kuwapo uharibifu huo, lakini akaeleza kwamba Kinapa ilishafunga msitu huo siku nyingi.

  “Wiki kama mbili hivi zilizopita Kinapa walifanya msako na kukamata mbao na mabanzi katika nyumba kadhaa katika kijiji cha jirani hapo Kiwei. Upasuaji mnaousikia unafanyika usiku na sio mchana,” alisema.

  Kauli ya diwani huyo ni tofauti na hali, ambayo NIPASHE ilishuhudia kwa kuwa upasuaji ulikuwa unafanyika mchana wa siku hiyo.

  Hata hivyo, alisema kumekuwa na jitihada kubwa za upandaji wa miti ndani na nje ya msitu wa hifadhi kwa lengo la kuokoa mazingira.

  “Tulikuwa na mito minne na mifereji isiyo na hesabu lakini yote imekauka, mto Umbwe ambao ni mkubwa ndio umebakia na maji kidogo kabisa, hali hii ni hatari,” alisema.

  Olomi alisema mbali ya uharibifu ndani ya hifadhi, katika kipindi cha nyuma wananchi walikuwa wakikata miti kwenye mashamba yao hivyo kuongeza hali ya 'jangwa'.

  Pamoja na maelezo ya diwani huyo, NIPASHE ilishuhudia uchimbaji wa mchanga katika mto Umbwe hali inayochangia zaidi uharibifu wa mazingira.

  Alisema katika mkakati wa upandaji wa miti, wananchi kwa kushirikiana na asasi ya kiraia ya Lepaje, imekwishapanda miti 4,000 ndani na nje ya hifadhi hiyo.

  “Uchimbaji wa mchanga unaathiri sana mazingira na tunawazuia japokuwa sio moja kwa moja kwa sababu wapo wazazi wengine wanasomesha watoto wao kwa biashara hiyo,” alisema Olomi.

  NIPASHE pia ilizungumza na Mhifadhi Mkuu wa Kinapa, Nyamakumbati Mafuru, kuhusiana na uharibifu huo, lakini alijibu kwa jazba kwamba: “Wewe si Mtanzania? Kama ni hivyo, basi ujue unalo jukumu la kulinda mlima Kilimanjaro.”


  “Kama umeona mtu anapasua mbao si ungemkamata? au unataka tu kuichafua Kinapa? Lazima tujue kwamba hili ni jukumu letu sote. Kwanza mimi siruhusiwi kusema chochote. Mtafute Shelutete (Pascal), ambaye ni msemaji wa Tanapa, atakuwa na majibu ya kina,” alisema Mafuru.

  Aliongeza: “Utaratibu ni kwamba unatakiwa kuandika maswali, uyapeleke Tanapa Arusha. Halafu kama wakikujibu sawa au wakiniambia nizungumze na wewe nitafanya hivyo. Niache kwa sasa nina majukumu makubwa ya kiofisi natakiwa kufanya...huu sio muda wa kuongea na waandishi wa habari.”

  NIPASHE ilipomtafuta Shelutete na kumweleza hali hiyo, alijibu kwamba yupo likizo hivyo asingeweza kusema chochote.  Mwandishi wa habari hizi alimwomba Shelutete amwelekeze kwa mtu, ambaye angeweza kutoa ufafanuzi wa suala hilo kwa niaba yake, lakini alikataa kwa madai kwamba hakumwachia mtu yeyote nafasi yake.


  Wakati wakubwa hao wa Tanapa na Kinapa wakieleza hayo, katika eneo la Uru inadaiwa kwamba ndiko hasa biashara ya mbao inafanyika, ambako mnunuzi huagiza mbao asubuhi akiwa Moshi mjini na analetewa 'mzigo' usiku ambapo pia analipia.

  “Kama uko serious unataka mbao sema ni kiasi gani na uelekeze unakotaka zishukie; jioni nakuletea mzigo wako, lakini utaletewa mbao mchanganyiko yaani za miti mbalimbali,” alisema mfanyabiashara mmoja ambaye hakutaja jina lake.

  Katika eneo hilo, uharibifu ni mkubwa na unafanana na vijiji vingine vinavyopakana na hifadhi hiyo.

  Wilayani Hai, ambako kuna geti la Machame, ukiwa ndani ya msitu huwezi kuona tofauti ya msitu na mashamba ya kawaida ya wananchi kwa kuwa kumebakia viwanja na vichaka vidogovidogo.

  NIPASHE iliingia ndani ya msitu huo kupitia kijiji cha Nkuu Ndoo, kilichopo Kitongoji cha Nkweshoo, Kata ya Machame Mashariki na kushuhudia uharibifu mkubwa, ikiwamo ng'ombe na mbuzi kupata malisho ndani ya msitu.

  Mzee Sindanaeli Kileo (71), ambaye shamba lake linapakana na hifadhi ya mlima, alisema: “Miaka mitano ijayo huu msitu utakuwa umeisha. Mimi nilishapeleka hadi majina ya wanaopasua mbao kwa askari, lakini upasuaji unaendelea.”

  “Miezi miwili iliyopita niliwaeleza watu wa Kinapa kuhusiana na hii hali wakaniambia nisiwaelekeze kazi kwa sababu wanalinda mlima sio msitu. Ndio maana unaona msitu unaendelea kuteketea,” alisema Mzee Kileo ambaye pia aliwahi kuwa Mwenyekiti wa Kitongoji cha Nkweshoo.

  Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Kitongoji hicho ambaye pia ni mwanaharakati wa masuala ya mazingira kijijini hapo, Twalib Mallya, alisema inasikitisha kwamba wananchi wenye mapenzi mema wanapanda miti, lakini wahalifu wachache wanakata miti na kuchunga ng'ombe kwenye hifadhi bila kuchukuliwa hatua.

  “Kutoka hapa hadi hapo getini hakuna umbali wowote, lakini unaweza kuona jinsi watu wanavyopasua mbao wakati wowote tena bila wasiwasi,” alisema.

  Alisema kitongoji hicho kinakusudia kutunga sheria ndogondogo ili watakapomkuta mhalifu akikata mti ndani ya hifadhi wanamkamata na kumpeleka kituo kikuu cha polisi mjini Moshi badala ya sasa wanavyomkabidhi kwa askari wa Kinapa na kuachiwa.

  “Sisi hatuna imani kabisa na Kinapa kwa sababu hawachukui hatua zozote kudhibiti hali hii,” alisema.

  Diwani wa Machame Mashariki (CCM), Rajab Nkya, alikiri kuwapo kwa hali hiyo na kueleza kuwa: “Nasikia tu kuna Kinapa na Tanapa. Sina hakika kama wapo. Maana sioni wanachofanya. Kwa sababu sisi wananchi wa kawaida tunaona watu wanapasua mbao, lakini Kinapa haijafanikiwa kuwaona."

  Aliongeza: “Nafikiri kama msitu ungekuwa mali ya mtu binafsi miti isingekatwa mbona ndizi huku shambani haziibwi? nimeshakamata fuso mbili zikiwa zimesheheni mbao nikapeleka polisi na nyingine serikali ya kijiji lakini wahalifu wapo na Kinapa hawachukui hatua zozote."

  Alisema juhudi za kupambana na uhalifu huo unakwama kwa sababu wapasuaji wakubwa wa mbao ni baadhi ya viongozi wa vijiji ambao wanalindwa na askari wa Kinapa.

  Alisema hali hiyo imesababisha kukauka kwa mito Waramu, Makoa na Weruweru pamoja na mifereji yote iliyokuwa ikitumiwa na wananchi kumwagilia mashamba wakati wa kiangazi.

  Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Leonidas Gama, alipoulizwa kuhusiana na hali hiyo, alionyesha kusikitishwa na kuahidi kufuatilia kwa kina ili kuona namna ya kulitatua.

  SOURCE: NIPASHE
   
 2. feis buku

  feis buku JF-Expert Member

  #2
  Jan 17, 2012
  Joined: Aug 29, 2011
  Messages: 2,371
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Too long!!!
   
 3. MNYISANZU

  MNYISANZU JF-Expert Member

  #3
  Jan 17, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 7,056
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Askari wanalinda mlima na sio msitu! Nimeipenda hii
   
 4. p

  punainen-red JF-Expert Member

  #4
  Jan 17, 2012
  Joined: Nov 18, 2010
  Messages: 1,735
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Kichwa legelege, idara zote legelege, Kichwa punguani, viungo vingine vyote vitafanya matendo ya kipunguani... Kiongozi mkuu mwizi, viongozi wengine wote lazima wawe vibaka... Kama dege la kiarabu linakomba wanyama hai sembuse hao vibaka wa mbao...
   
 5. M

  Mchomamoto Senior Member

  #5
  Jan 17, 2012
  Joined: Aug 19, 2011
  Messages: 169
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  ha ha ha ha ha ha sisi watz tuna mambo!!??jamani WF- nchi hii imeshaharibika ndugu zangu maana hata kwenye mambo yasiyohitaji siasa sisi tunaleta siasa.Viongozi wetu wanaleta siasa kwenye uhifadhi wa "viumbe pori" sasa kwa kutumia uwezo mdogo tu wakufikiri unategemea askari na viongozi wa KINAPA wafanye nn??? serikali haitaki kufanya uhifadhi ubaki kuwa uhifadhi na si kuchanganya na siasa, pesa hakuna, vifaa hakuna, miundo mbinu mibovu, na mengine mengi;sasa unategemea askari gani atakuwa hayawani wa kuacha fedha kutoka kwa wafanyabiashara wa mbao alinde msitu!!acha wale tuu!!anaiba baba Rizi na washkaji zake sembuse askari!! kwani nn bwana sawa tu.
   
Loading...