Hebu acheni hii mambo

Hebu acheni hii mambo

Socratic

JF-Expert Member
Joined
Dec 18, 2014
Posts
568
Reaction score
308
Unakuta mtu amefariki. Watoto, wanafamilia, ndugu jamaa na marafiki wanalia na kuomboleza. Anatokea mtu anatoa nasaha kuhusu marehemu na mwisho anamalizia kwa kusema "Sisi tulimpenda Lakini Mungu alimpenda zaidi". najua ni kauli inayolenga kuleta faraja lakini tumeshafikiri kwa jicho la tatu kuhusu kauli hii?

Fikiria unamwambia mtoto mdogo ambaye mzazi wake aliyempenda sana amefariki kisha anaambiwa "Mungu alimpenda zaidi (Ndio maana amemchukua), tunajua hii inaleta fikra gani kwa yule mtoto? Na hata kwa watu wazima, ni kweli kuwa Mungu anawachukua wale anaowapenda zaidi? Ni kweli wanaofariki leo wamependwa zaidi na Mungu?

Hii misemo mingine inachanganya sana na pengine kupotosha.
 
mbona uishie njian fafanua zaid ili wana jamvi wakuelewe jarb hata kutoa maoni yako juu ya kauli yako.
 
mtoto mdogo anapoambiwa Mungu amemchukua mtu kwa sababu alimpenda zaidi kisaikolojia inamwongezea msongo kwa vile hufikiri ni kwa vile hakumpenda sana mzazi wake ndio maana Mungu ambaye amempenda zaidi amemchukua. Kama yeye (mtoto) angempenda zaid Mungu asingemchukua. Hii inaleta guilty conscious kwa mtoto na hivi kumzidishia machungu. na hata kwa tafsiri ya watu wazima si kweli kwamba Mungu huwachukua wale anaowapenda zaidi ina maana waliopo duniani hawapendwi zaidi na Mungu? je majambazi wanaouawa kwa kuchomwa moto wanakufa kwa sababu Mungu aliwapenda zaidi? maoni yangu ni kuwa tuache misemo ambayo haina tija.
 
UHURU WA MAONI;Wewe unadhani misemo ipi itumike ili kuleta mantiki nzuri??.
 
Kweli hii kauli sio nzuri hata kidogo huwezi fiwa halafu ukaambiwa aliyekufa mungu alipenda zaidi ina maana nyie ambao mpo kwenye msiba mungu hawapendi
 
duuh. kazi. kweli kweli yani kiswahili ndo lugha ya taifa
 
Ukifka mahali ukakuta msba unatakiwa umwambie aliyefiwa kwamba amuombe mungu nayeye afe amfuate
 
ttzo mnaleta mzaha kwenye misiba na kuwakosesha walio hai kutafakar kwamba nao watakufa wajiandae kwa kutenda yalio mema
 
Unakuta mtu amefariki. Watoto, wanafamilia, ndugu jamaa na marafiki wanalia na kuomboleza. Anatokea mtu anatoa nasaha kuhusu marehemu na mwisho anamalizia kwa kusema "Sisi tulimpenda Lakini Mungu alimpenda zaidi". najua ni kauli inayolenga kuleta faraja lakini tumeshafikiri kwa jicho la tatu kuhusu kauli hii?

Fikiria unamwambia mtoto mdogo ambaye mzazi wake aliyempenda sana amefariki kisha anaambiwa "Mungu alimpenda zaidi (Ndio maana amemchukua), tunajua hii inaleta fikra gani kwa yule mtoto? Na hata kwa watu wazima, ni kweli kuwa Mungu anawachukua wale anaowapenda zaidi? Ni kweli wanaofariki leo wamependwa zaidi na Mungu?

Hii misemo mingine inachanganya sana na pengine kupotosha.
ni kauli ya kufariji, ila siipendi, mungu anawapenda watu wema wote,ila kufa si kwakua umependwa
 
Back
Top Bottom