Leo katika pitapita zangu nikatokea mitaa ya Temeke hospital ng'ambo ya pili,lengo langu nifike wailes .wakati natafuta kichocholo cha kupita nikaona watu wanatokezea kichocholo flani hivi nami nikavutika kupita hapo,kwanza kichocholo chenyewe ni lazima upite kiubavu tena mmoja mmoja ukimuona mwenzio kwa mbali anakuja inabidi usubilie.
Ilipofika zamu yangu kupita baada ya kumaliza tu hicho kichocholo nikawakuta wadada wamekaa nje mlangoni kwenye sturi karibu vyumba arobaini hivi ,cha ajabu kulikuwa na pilikapilika nyingi sana eneo hilo wanaume walikuwa wanapitapita na wengine wanaingia ndani na wengine wanatoka .
Nilipouliza kwani kuna nini maeneo haya jamaa mmoja akanijibu hapo kuna huduma ya ngono maarufu kwa WAHAYA da kwakweli nimechoka
Sent from my BlackBerry 9700 using Jamii Forums