Hazina ya Tanzania imefilisika, Rais aseme tu ukweli

Zero Hours

JF-Expert Member
Apr 1, 2011
12,942
18,669
UPDATE: Sept 2019

Zitto afunguka:



===========
Previously:

Maji yameanza kufika shingoni. Matumizi yamezidi mapato. Kama serikali ingekuwa inaweka wazi kuwa hazina imebakiza kiasi gani kwa sasa, basi watanzania wengi wangepata mshituko mkubwa.

Financial sources za nje nazo zimebuma. Mapato ya TRA yamebuma nayo. Zile mbwebwe za kutangaza mapato zilidumu kwa miezi mitano tu. Sasa tunaelekea mwezi wa tatu hawajatangaza mapato ya TRA. Yani tumefikia hatua hata Fine za barabarani nazo kuonekana kama chanzo cha pato kubwa sana hapa nchini.
ccdc3ada503331d4ece4c2d69367c6c1.jpg

Tuna 40% budget deficit. Average domestic income ni Trilion moja kwa mwezi. Miezi 12 maana yake ni 12 trillion. Hapa kuna deficit ya 5trillion from projected domestic income ya 17 trillion. 12trillion ilitegemewa kutoka hasa kwenye mikopo na misaada. Misaada sasa imebuma. Na mwanzoni walikuwa na mbwembwe kweli. Eti 70% ya pato itakuwa inalipa deni la taifa!!!!!!!! Sijui mpaka sasa imelipa kiasi gani!

Sasa serikali imepata kiwewe. Walianza na kupiga panga pesa za mikopo kwa wanavyuo, wakapiga zile za kagera, wanaosoma nje nao wakanyimwa mikopo, bila kusahau panga la ajira hasa walimu. sasa posho za madiwani zimefutwa, zitafata za wabunge, mawaziri, na hata watumishi wa serikali.

"Hii sio kubana matumizi bali ni kupunguza matumizi ili kuendana na hali mbaya ya uchumi."

Kinachoniuma ni pale wanakanusha na kusema hali ya uchumi ni nzuri na inaimalika. Wanatoka hapo wanajisahau na kusema hali ya uchumi imelega sababu ya wapiga dili wamebanwa. Ama kweli njia ya muongo ni fupi.

Wanatumia nguvu kweli kuwasingizia wapiga dili. Uongo tu huu kweupe kabisa. Wataiba nini kwenye serikali iliyofilisika? Ni sawa na ukute masikini hana chochote analala mlango wazi akijisifu kuwa hakuna wezi. Unakuta mtu kama Mwakyembe anasema eti wapigadili wamebanwa. Jamani jamani !!!! Muwe mnamuogopa hata Mungu. Mseme tu ukweli serikali haina pesa tunaihurumia hata kuiibia.
fa9b1477e5a6716f29dbbe3dbaf6f0dd.jpg


2015 walikuwa wanajinadi kuwa nchi ni tajiri. Sisi ndyo tuwe tunatoa mikopo nchi nyingine. MCC waametunyima pesa tuliwakejeli sana. Wapo waliosema hatuhitaji pesa sa misada tunaweza kujiendeleza wenyewe. Leo wanatangatanga kutafuta mikopo. Apo msisingizie riba. Semeni ukweli kuwa tunanyimwa sababu ya malimbikizo makubwa ya madeni. Tanzania hatulipagi madeni.

Hakuna anayefurahia hii hali tunakoelekea nikubaya. Kila mtu inamuumiza. Personaly mimi ni muajiri. Wafanyakazi wangu nimewapiga panga la 20% ya mishahara yao asiyetaka aache kazi. Hii sasa ni kila sehemu. Private secta zinapunguza waajiri kama sio kuwapunguza mishahara ili kwendana na hali ya uchumu. Serikali ilijiwai mapema kuwakata wajiriwa wapya wa mwaka 2015.

Tanzania hatujawai kuwa na uchumi mzuri lakini hii hari ni bora ya jana.

Viongozi wenyewe hata hawaeleweki wanamkakati gani wa kuokoa jahazi zaidi ya kutoa matamko na kusingizia wapiga dili. Wao wanasema hali ni nzuri. Na ni kweli wanachokisema. Hata kwenye nyuso zao utatambua kuwa hali ni nzuri kwao kwa jinsi wanavyopendeza na kuzidi kunawili kiafya. Watakuwa wanafiki wakisema hali ni mbya wakati wananenepa na sura kungara. Walivyokuwa kabla hawana madaraka 2015 si sawa na sasa.

a7a74563abe760431c89fc43910e6944.jpg


Yani serikali ya magufuli naifananisha kama mmiliki wa ngombe anayekamua ngombe zake ila hazipeleki malishoni. Maziwa anakunywa yeye na familia yake. Hafikirii keshokutwa kuwa ngombe watashindwa kutoa maziwa. Kwa wamasai wanafikiaga hata hatua ya kuwanyonya damu.

Watanzania wanapinda kweli kulipa kodi ila zinaishia kwao kulipana mishahara na kuimalisha
Usalama wao na familia zao .

Ningependa kumfikishia huu ujumbe Magufuli.
" He Can Cheat Tanzanians, but not Economic Principles, and if he likes the milk let him feed the cow too" Over.
 
Lugumi ndio mgombea urais wa chadema 2020 Dj akibadili gia za angani.

Bavicha msimtukane sana itakuja kuwapa shida kumsafisha ,kama ilivyowapa shida kumsafisha Lowasa
Naanza kupata mashaka na hawa watu wa lumumba. Hivi nyie ni binadamu au CCM misukule? Sasa nani kaongelea Lugumi hapa.

Kuna kitu CCM inawafanya nyie sio bure
 
Lugumi ndio mgombea urais wa chadema 2020 Dj akibadili gia za angani.

Bavicha msimtukane sana itakuja kuwapa shida kumsafisha ,kama ilivyowapa shida kumsafisha Lowasa
discuss fact iliopo mezani acha kuwa msomi-ta.hi.ra sasa lowassa anaingiaje kwenye hiyo mada hapo.mi nadhani ungemkosoa kwa kuleta data kuwa hizo data anazozisema si kweli
 
Back
Top Bottom