Uncle Jei Jei
JF-Expert Member
- Jan 7, 2011
- 1,684
- 2,157
Wakristo tunasema "apumzike kwa Amani"
Naamini Kuna kundi la watu wanakereka kusikia habari za Magufuri, itabidi mzoee kiongozi huwa haishi kuongelewa
Binafsi niwe muwazi mapema tu, Mimi nimiongoni mwa waliosema, "Asante Mungu kwa kuitetea Tanzania" baada ya tangazo lile.
Alikuwa mtu fulani ambaye ni kama alitamani nchi yote hii aishi yeye na watu atakao watengeneza yeye wa kumuelewa na kufanana naye.
Aliongoza Taifa Kama familia yake tena yenye watoto under 18 ambao maamuzi yote watasubiri kwa Baba. Kwa mfano:-
1. Kujifanya yeye ndio mjuaji wa kila kitu na wengine wote hawajui chochote, wachache tu ndo wangemfurahia
2. Kuongea kwa dharau anapoongelea maslahi ya watu hasa watumishi wa umma, ni hakika alitufanya tutende dhambi ya kumchukia
3. Kuwaaminisha kundi la maskini kwamba yeye ndo mwema pekee na anatetea maslahi yao kwa kuwakomesha wanyang'anyi waliojimilikisha mali za Tanzania wakati huo huo pesa ikiondoka mtaani na kufungiwa kwenye vyumba anavyovifahamu yeye, wenye akili wasingemuelewa
4. Ubabe, dhihaka kwa viongozi wenzake, kufoka, matusi na kupenda kusikia mazuri tu, hili nalo halikupendeza machoni pa wengi
Hayo na mengine mengi yalimfanya ajiwekee madoa doa kwenye uongozi wake kwa makusudi kwani uwezo wa kutoyafanya na akafanikiwa alikuwa nao
Hata hivyo pamoja na mengi aliyofanya ambayo hayakuwapendeza waliowengi wakiwemo wasaidizi wake kwasababu za wazi na zisizowazi, najiuliza yafuatayo:-
1. Je, ndio sababu reli ya SGR isikamilishwe kwa wakati!?Wanamkomoa marehemu au Wananchi?
2. Bwawa la Nyerere tunasikia sio kipaumbele tena, kwani alikuwa anawajengea wanachato au Wananchi wote!?
3. Tunaona "wakoloni" waliopewa jina zuri la "wawekezaji"(Kwa kukopa maneno ya Professor mmoja mjumbe wa kigoda Cha Mwalimu Nyerere) wakimiminika kila Kona kwenye kila sekta huku wazawa wakiwekwa pembeni. Hapa napo tunalipiza kwa aliyofanya marehemu?
4. Bei za vyakula na bidhaa nyingine zinapanda kila baada ya dk kadhaa Kama zile biashara za kina Ontario za forex na utetezi umekuwa vita vya Ukraine na Urusi badala ya kusema ukweli vyakula tulivigawa kwa majirani zetu kwa bei chee Sasa tunahaha!
5. Ili kumkomoa, hatuoni taabu kupanda daladala "Europe" kwa safari ambayo ingeweza kuishia ubalozi uliopo nchini kwa kusaini kitabu Cha maombolezo japo na bendera ilishushwa nusu mlingoti. Bado hii haikutosha tutapigaje selfie na jeneza tusipoenda!?
6. Waliokuwa wanajinasifu kuwa watetezi wa wanyonge wameona Sasa wawanyonge wanyonge hao na kamba ya TOZO ilizongushwa kila Kona kiasi Cha kukosa pa kupumlia. Hapa napo wanamkomoa marehemu?
Hayo na mengine mengi wanayoendelea kufanya bila kufikiri vizuri, yanafuta taratibu madoa ambayo mwendazake alijiwekea mwenyewe na kwa kiasi kikubwa yakamchora Kama kiongozi aliyenyanyasa wenzake
Wakiendelea hivyo, the Late Magufuri ataibuka shujaa mioyoni mwa wote wenye akili na kulipenda Taifa letu.
Siku zote, ubaya alioutenda kiongozi kwa wananchi hufutwa na ubaya unafuatia kwa kiongozi mwingine!
Haya yanayoendelea Sasa yakiendelea hivi yanavyoendelea, the Late Magufuri ataonekana mwema na mtu aliyependa maendeleo machoni pa waliowengi kuliko mrithi wake wa sasa!
Time will tell