VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,135
- 17,802
Msiba umetukumba watanzania. Aliyekuwa Rais wa Zanzibar na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Tanzania,Hayati Aboud Jumbe Mwinyi ametutoka. Ametangulia mbele ya haki. Alale mahali pema peponi,Amina.
Jumbe,aliyezaliwa tarehe 14/6/1920 huko Juba,Sudan Kusini(wakati huo ikiitwa Anglo Egyptian Sudan),amewahi pia kuwa Makamu Mwenyekiti wa CCM Taifa. Amepata kuwa Rais wa Zanzibar kuanzia tarehe 7/4/1972 hadi tarehe 30/1/1984.
Mwaka 1984,mwezi Januari,Hayati Jumbe alitoka Zanzibar na kwenda Dodoma kuwajibika kama kiongozi wa chama tawala na Serikali. Akapoteza nyadhifa zake zote za kiserikali na kichama. Hayati Jumbe 'hakuruhusiwa' kurejea Zanzibar. Badala yake aliishi Mjimwema,Kigamboni Dar es Salaam tangu mwaka huo hadi mauti yanamkuta mwaka huu.
Kwa miaka zaidi ya 32,Hayati Jumbe ameiacha Zanzibar yake. Hakwenda wala kuiona tena.Amerejeshwa huko kwenda kuzikwa. Hakuwa kama alivyotoka. Ndiyo maana nasema,ametoka kwenda kuwajibika na amerudi kupumzika. Chamani na Serikalini,Hayati Jumbe alikuwa mzazi wetu,kiongozi wetu,mshauri wetu na mfano wetu. Hoja zake zitaishi daima!
Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam