Good Father
JF-Expert Member
- Feb 28, 2014
- 10,275
- 18,352
Habari za wakati huu.
Niende kwenye mada moja kwa moja.
Jana nikiwa katika kijiwe flani hapa jijini kwa Makonda nilisikia watu wazima wakitoa malalamiko makubwa ambayo kiukweli yalinitisha.
Hoja zao zilihusu hospitali ya Mloganzila (ile branch ya Muhimbili National Hospital) iliyoko Kibamba, wale wazee walikua wakisikitika kuhusu ubora wa huduma za pale na gharama za matibabu kuwa ghari sana.
Wanasema ukipelekwa pale unaumwa uwezekano wa kupona unakua mdogo sana, ukinusurika kufa basi utakua unadaiwa mamilioni ya fedha, waliendelea kusema kwamba madaktari wa pale wengi ni wanafunzi (internship) hawana care kubwa wala uzoefu mkubwa hali inayopelekea cases nyingi kushindikana na wagonjwa kufa.
Hayo yalikua na mazungumzo ya wale wazee, nilisikiliza mazungumzo yao bila kuchangia wala kuonesha kama nawasikiliza stori zao lakini nilikua nafatilia kwa makini sana kutokana na unyeti wa suala lenyewe.
Mimi sijawahi kufika hospitali ya Mloganzila naishia kuona kibao chake pale barabarani tu, mliowahi kwenda kupata huduma au mlipeleka ndugu zenu hebu wekeni ukweli tusiojua tujue maana sisi sote ni wagonjwa watarajiwa.