Kwisaro
Member
- Mar 28, 2018
- 30
- 45
Nafkr mambo yanayoendelea ya wabunge na madiwani kuachia nyadhifa zao kisa tu kuwa na mahaba na mkuu wa kaya inabidi ujiulize!! Ni kweli ni haki kikatiba mtu anao uhuru wa kuhamia chama chochote akitakacho.Lkn inaathari kwa sisi walipa kodi pesa ambazo zingeenda kwenye maendeleo ya taifa hili ambalo lina changamoto kibao leo zinarudia uchanguzi tena kwa viongozi walewale waliojiuzuru nafasi zao. Kuna umuhimu wa kuirudisha rasmi ya katiba ya jaji warioba mezani ili kuepusha mambo kama haya yasiendelee.