Haya ya Uingereza kuzuia bunge ikoje?

Zawadini

JF-Expert Member
Feb 2, 2012
2,213
1,638
Tuliona na kusikia wakati ule Waingereza walipopiga kura kwa hiari yao kuamua kujitoa uanachama wa Umoja wa Ulaya baada ya Serikali kuridhia jambo hilo chini ya uwaziri Mkuu wa wakati ule. Hili la kuridhia kura ya maoni ipigwe wakati ule huenda lilitokana na uzoefu uliotangulia ambapo nchini Scotland wananchi wa kule walipiga kura kuamua ama kujitoa au kubaki katika Muungano wa Ufalme (UK) na hivyo wananchi kwa hiari yao wakaona ulazima wa kubakia katika Muungano huo kwa kujua athari ambayo ingeweza kutokea kwa kujitoa. Hili, nadhani, ndilo lilimdanganya Waziri Mkuu wa wakati ule kukubali kura ipigwe, akiamini wananchi watakataa kujitoa kama ilivyotokea Scotland. Kwa bahati mbaya matokeo yakawa tofauti, kwani Waingereza wakaamua kujitoa EU.
Baada ya kura ile uchambuzi wa kisiasa ukafanywa, nadhani, kuona athari ya jambo lile la kjujitoa. Ikitokea kwamba hili la kufanya utafiti lilifanywa baada ya uamuzi wa wapiga kura kutolewa, itakuwa Waingereza walipitikiwa/walijisahau au waliamini kura hiyo itaamua kutokujitoa jumuiani.
Kwamba sasa Waingereza ndio wanaamka kutoka usingizini wakitaka kubadili msimamo, kwangu mimi naona kama hawajiamini hivi! Kuanzia jana wananchi wa huko wameanza maandamano, na nadhani yataendelea, ya kupinga kujitoa kwa Uingereza bila masharti – wenyewe wanaita no deal Brexit. Kitendo hiki kwangu kimenifanya nijiulize kulikoni? Ni kwamba wanajielewa mno au hawajielewi? Kwamba zile kura zilizopigwa wakati ule zilikuwa za maruhani? Natarajia istilahi hii ya kura za maruhani sio ngeni sana Tanzania. Kwamba Waziri Mkuu wa sasa ameamua kuzuia vikao vya bunge ili lisipitishe uamuzi/azimio la kuchelewesha jambo hilo ni la busara au imekaaje? Nawasilisha.
 
Sarakasi kila sehemu, ingekuwa nchi ndogo weshaikemea zamani ......

Similar Discussions

Back
Top Bottom