Haya ya kufanyiwa kazi haraka Simba SC kabla ya kuanza Ligi Kuu na michuano ya CAF

Nimeishia uliposema ALIDHARAU... HIVI UNA AKILI KICHWANI?? NANI ALIWAHI KUDHARAU MECHI???
 
Kanoute alikuja vema mpaka kuna Uzi yeye na Sakho nikiwaelezea lakini sasa kuna kitu hakiko sawa upande wake, ana rafu ambazo si lazima kufanya.

Kwahivyo kwenye michezo kama hii ukimtoa Kanoute, mbadala (anayeingia) anatakiwa kuwa kama yeye au zaidi yake tutaendelea kujiuliza kwanini Akpan hakucheza ndo maana nikasema Kocha Zaron Maki alizidiwa mbinu ya Kocha Nabi.
Alizarau mechi kocha wa simba huwezi ukamuanzisha mzungu kwenye derby kama zile wakati hata pre season hakuwa na team.
 
Simba hii inasikitisha sna, Babra team imemshinda huyu, nakumbuka wenzake waliijenga team akairithi ikiwa nzuri il alipoingia tu project ya kwanza ikawa kuuza key players chama na Luis, alaf akasajili watt wakina Banda, nyoni sjui wakwap.

Nilidhan dirisha hili tungekuwa very aggressive cha kushangaza licha ya usajili ila bado team inategemea Mzamiru na Mkude, Boko wakupe positive results.

Mara unasajili Kyombo kweli ndo awe mkombozi? Hata Sopu hatukumuona? Jamn hii Simba hapa kuna tatizo kubwa.
Duh! Unajua kukatisha tamaa wenzako.
 
Kwa msimu huu viongozi wa Simba SC wamejitahidi sana usajili, licha ya kumkosa Adebayor na Lobi Manzoki

Kocha Zaron anaweza kuchagua Kikosi chake cha ushindi na kuacha kujaribu Wachezaji na Sub yake ambayo imegharimu timu, nina imani Simba itakuwa moto sana na hasa wakipata Defensive Midfielder, aanze sasa kusoma mbinu za wapinzani wake na hizi Derby namna ya kupambana nazo.

Lengo ni kufanya vizuri Ligi na michuano CAF, hawa Yanga wameshtua nini la kufanya kwa msimu ujao.
Hana muda mrefu sana kwenye timu taratibu ataipata best eleven yake
 
Kipindi cha Kwanza Yanga walikuwa tumewakamata, Kitendo cha kumtoa mbunifu wa pasi za Magoli yaani Chama na Mkabaji asiyepewa heshima yaani Kanoute ili mkosti Kocha, nafikiri suala la Kocha msaidizi lifikiliwe upya ikiwezekana aondolewe kama tulivyofanya kwa Djuma basi Matola naye amshe tu.
CHAMA AMETOLEWA DK YA NGAPI NA MATOKEO YALIKUWAJE MUDA HUO??
 
simba hata turudiane na Yanga kesho tutafungwa tu... Tuseme ukweli ile formation yao ya Morrison Mayele Azizi Moloko ni beki gani wanaweza kuwatuliza hawa watu..? Yanga ukiikaba kushoto katikati inakufunga, ukiikaba katikati basi Morrison au Azizi hakuachi salama... Mkitaka tuifunge Yanga basi yule beki wao Mwamnyeto acheze dakika 90 halafu Bangala asicheze... Simba hatuna forward za kutisha
Wasipoelewa hapa basi waache.
 
Nilipoona tu yumo Kibu, Kanoute, Mkude na Kyombo nikajua hapa leo hatutoboi.

Kanoute aliniprove wrong, lakini hao wengine hakuna walichokifanya.
 
Kanoute anauwezo wa kucheza DM tena kwa kiwango kikubwa sana, game na Yanga kirumba kipindi cha pili dk ya 70 alisimama kama DM na alicheza kwa ufanis mkubwa sana licha ya kua ni Box to box kocha amshift acheze DM maana ana sifa za DM
 
Nimeishia uliposema ALIDHARAU... HIVI UNA AKILI KICHWANI?? NANI ALIWAHI KUDHARAU MECHI???
Kwangu siwezi kuwa na akili kama yako..Wote wameleta maoni yao kwa mtazamo wao.

Kama unaweza kusema eti umeishia niliposema sijui nini inakuhusu nini wewe Pimbi? Umeitwa

Baada ya game Kocha Zaron amekiri kuzidiwa mbinu na kusababisha kupoteza game, sasa wewe ni zaidi ya Kocha?

Halafu unaleta bhah bhah zako hapa.
 
Akizungumza kwenye Pre-Meeting ya Watani wa Jadi Simba SC na Yanga SC, Kocha Zaron Maki alisema kuwa amekutana na derby nyingi, huku akiamini kuwa ubora wa wachezaji ndo unaamua mechi kushinda na sio ubora wa mbinu ndani ya uwanja, kwani game kubwa huamuliwa na mambo kama Kona au Free Kick.

Kwangu Ghazwat, hili lilikuwa kosa kubwa sana alifanya Zaron Maki, kwani hapa ni dhahiri ameshindwa kumuheshimu mpinzani wake, ameleta dharau na ndo maana aliamua kuingia na kikosi cha kawaida mno na kufanya Sub yake ambayo imegharimu timu hali iliyosababisha kufungwa kizembe na ndo kilikuwa Kiini hasa cha matokeo.

Kwahivyo ili kuweza kufikia malengo ya timu, Viongozi wa Simba wamwambie Kocha abadilike kabla ya Ligi Kuu na michuano CAF kuanza, aache dharau na kukariri na mambo ya Morocco, Sudan na Angola, na kwa game dhidi ya Yanga, Nabi ndo ameonekana kuzijua zaidi game za Derby, na amekumbushwa la kufanya.

April 30 2022, niliandika Uzi kuhusu Kocha Pablo Flanco Martin kuwa ni Kocha nzuri sana ila anahitaji wachezaji Quality, hapa ni wachache sana walielewa hii Nukta akiwepo Pettymagambo na Goguryeo asanteni sana nyie Wanamsimbazi

Pablo Flanco ni kocha aliyemsumbua sana Nabi kimbinu ingawa alikuwa na wachezaji wa kawaida, tofauti na sasa, Kocha Nabi ili aweze kumfunga Pablo ilikuwa lazima baadhi ya wachezaji katika kikosi cha Simba kuwa majeruhi, na pia alifanya vizuri Kimataifa kwa matokeo ya ndani na nje hasa game dhidi ya Orlando Pirates.

Kuelekea msimu wa Ligi Kuu na michuano CAF, Simba SC wanahitaji Defensive Midfielder, (DM) na siku zote hakuna mabeki wazuri kama hakuna Defensive Midfielder, Simba SC inahitaji Proper Replacement ya Prime Kanoute.

Haya ndo mambo yakufanya kabla ya Ligi Kuu na michuano CAF, ili kubaki na mwendo wa ngiri tu meno nje, naona baadhi wengine wamesusa na wakafika mbali zaidi kwamba viongozi waache ngazi, mashabiki waache kwenda uwanjani haya yote sidhani kama ni sahihi kwa sasa, na si afya kwenye medani ya soka, hii ni Simba yetu Nguvu Moja.

Kulitaka Mwana Kulipewa Mwana
Sasa hao unaowashauri hivi ni kama mang*ombe tu hayaelewi na wala hakuna watakachofanya zaidi ya ujinga tu walete mzunguu....mlete mzunguu..
 
Style ya kocha ..timu inacheza vizuri posesive game..
Katikati simba bado la shida..hatuna kiungo ambaye ni fast na nguvu ( ona Khalid aucho )..
Bado naangalia Quattara speed yake..

Bt Simba haukuzidia sana , ila second half subs
 
Simba hawataki kocha wa mbinu kama kishingo na pablo wao wanataka pira biriani dakika 90 ila wale kina pablo na sven walikuwa technical coach.
Kwani kishingo aliondokaje Simba ?

Pablo alikuwa na football philosophy tofauti na club ulitaka timu iendelee kucheza mpira usioeleweka ?
 
Kocha Zaron Maki alimuhitaji zaidi Mohamed Ouattara kuliko Herve Ngomo ambapo kamati ya usajili walimtaka.

Lakini rejea kwenye Uzi, hakuna beki bora kama hakuna Defensive Midfielder
Lakini ngomo ana offer viwili beki wa kati na kiungo mkabaji
 
Najibu hoja mbili 4 na 5 hapo kwenye Uzi

Kuhusu mashabiki nimesema kuwa kuna mashabiki wanasusia Timu na kutaka uongozi uachie ngazi, hapo sioni kosa la viongozi maadamu wametimiza wajibu wao kwenye usajili.

Kiungo Defensive Midfielder kwa kumtegemea Mkude na Mzamiru endapo Kanoute akiwa low ni kujidanganya.

Kuna mdau ametoa maoni yake kuwa ikiwa kusajili DM ni ngumu kama kuna Mchezaji anaweza kutengenezwa akawa DM imara, kutafuta mbadala si lazima kusajili, kama Kocha anaona Akpan hatoshi ni kiasi cha kumuweka sawa.
Ni kweli mashabiki wengi wasiofahamu mpira kiundani wanataka lazima Simba isajili kiungo mkabaji mwenye weledi wa Lwanga au Fraga. Lakini narudia tena sio lazima Simba wasajili bali benchi la ufundi kama ni mahiri wanaweza kumtengeneza ndani ya kundi la wachezaji 30 waliosajiliwa na sio lazima afanye kazi hiyo kwa 100%. Bali atakuwa wa mpito tu mpaka dirisha dogo watakapopata mtu mwenye kazi yake. Kwa kuwasaidia Simba kiufundi zaidi Akpan na Outara wanaweza kuifanya hiyo kazi kwa ufanisi sana. Na ikishindikana hao hata Kapama atengenezwe ila huyu ni kisaikolojia zaidi na itahitaji muda zaidi vinginevyo akifanyiwa haraka atapotea kama alivyopotea mwenzie Abdulswamad.

Na hili sio geni kabisa. Kwa wanaofuatilia mpira muda mrefu na wenye kumbu kumbu nzuri watamkubuka kocha mmoja wa Simba aliyekuwa anaitwa Lenchatre ambaye alimtengeneza Kapombe halafu akamuhamisha toka pembeni na kumuingiza kati kucheza kiungo mkabaji na 6 na wakati mwingine namba 8 kutegemea mahitaji ya timu kutokana na mechi husika. Na Kapombe alimpa Lechantre alichohitaji kwa wakati ule. Sasa benchi la ufundi la sasa hivi kumbadilisha Mkude kucheza "aggressive" kama kiungo mkabaji haliwezi lakini hata kutengeza mchezaji mwingine wa kubeba hayo majukumu limeshindwa ndani ya wiki tatu za pre season Misri.
 
Ni kweli mashabiki wengi wasiofahamu mpira kiundani wanataka lazima Simba isajili kiungo mkabaji mwenye weledi wa Lwanga au Fraga. Lakini narudia tena sio lazima Simba wasajili bali benchi la ufundi kama ni mahiri wanaweza kumtengeneza ndani ya kundi la wachezaji 30 waliosajiliwa na sio lazima afanye kazi hiyo kwa 100%. Bali atakuwa wa mpito tu mpaka dirisha dogo watakapopata mtu mwenye kazi yake. Kwa kuwasaidia Simba kiufundi zaidi Akpan na Outara wanaweza kuifanya hiyo kazi kwa ufanisi sana. Na ikishindikana hao hata Kapama atengenezwe ila huyu ni kisaikolojia zaidi na itahitaji muda zaidi vinginevyo akifanyiwa haraka atapotea kama alivyopotea mwenzie Abdulswamad.

Na hili sio geni kabisa. Kwa wanaofuatilia mpira muda mrefu na wenye kumbu kumbu nzuri watamkubuka kocha mmoja wa Simba aliyekuwa anaitwa Lenchatre ambaye alimtengeneza Kapombe halafu akamuhamisha toka pembeni na kumuingiza kati kucheza kiungo mkabaji na 6 na wakati mwingine namba 8 kutegemea mahitaji ya timu kutokana na mechi husika. Na Kapombe alimpa Lechantre alichohitaji kwa wakati ule. Sasa benchi la ufundi la sasa hivi kumbadilisha Mkude kucheza "aggressive" kama kiungo mkabaji haliwezi lakini hata kutengeza mchezaji mwingine wa kubeba hayo majukumu limeshindwa ndani ya wiki tatu za pre season Misri.
Kapombe ni versatile toka muda mrefu hivyo hakukuwa na kutengeneza chochote pale
 
Back
Top Bottom