Haya wale wasikilizaji wa radio enzi hizo tukatane hapa tukumbushane baadhi ya vipindi

Kwa kweli tuliosikiliza redio zamani kwa sasa hakuna redio ya kusikiliza. Watangazaji wa sasa hawana ubunifu na wamekuwa kama kasuku.

Enzi hizo mtu unapata maarifa ya kutosha tena sana kupitia redio. Leo hii kuna redio huwezi kusikiliza na watoto au wazazi wako, ni full matusi na lugha zisizo na staha.
 
Kipindi cha twende na wakati igizo nlikuw sikosi RTD,kilikuw kikizungumzia vijana ,pamoja na changamoto wanazokutana nazo.hasa Magonjwa ya zinaa,madawa ya kulevya ,ulevi wa kupindukia ,kwa kweli Akina Tunu nakumbuka mbali sana
Na wale vijana machachari kibuyu na kidude
 
Na wale vijana machachari kibuyu na kidude
Ilikuw good Sana ,hasa ka Melody na wimbo kabla ya igizo.heli niwe peke yangu.......hell niwe nasubira ........hell niwe na mmoja ....ukimwi watisha /waniua us kipenzi ,waniua ua mamaee ×2 maneno yako matamu waniua ua ...***** waniua ua kipenzi waniuauamtu ulikuw unaji fill Kama unajanga vile
 
Maneno hayoo!!, Michezo mtangazaji Ezekiel Malongo, Majira watoaji taarifa Restituta Bukori radio Tanzania....... Jamboo!! Asubuhi daaah
 
Fredirick bundala--sitasahau(RFA)
Glory robinson--showtime(RFA)
Swed mwinyi --- ligi kuu matangazo(TBC)
Juma nkamia-- ligi kuu matangazo(TBC)
Wambula mtani--je huu ni uungwana?(RFA)


Radio free africa kipindi kile ilikuwa ni moto wa kuotea mbali.
 
RTD Pwagu na pwaguzi..
RTD malenga wetu..
RTD Mazungumzo baada ya habari.
RTD mahoka.
RTD Club raha Leo show.
RTD Kumekucha.
RTD shambani.
RTD Mchana mwema.
RTD mazungumzo baada ya habari ,mtangazaji- Berni Kiko kama sijakosea
 
"Wakati umewadia wa salamu kwa wagonjwa hospitalini tunawapa pole"hicho ni kibwagizo cha wimbo katika kipindi cha SALAMU KWA WAGONJWA siku ya jumapili asubuhi!
 
Kipindi cha twende na wakati igizo nlikuw sikosi RTD,kilikuw kikizungumzia vijana ,pamoja na changamoto wanazokutana nazo.hasa Magonjwa ya zinaa,madawa ya kulevya ,ulevi wa kupindukia ,kwa kweli Akina Tunu nakumbuka mbali sana
Haha unamkumbuka Tila? Tunu je? Na yule mume wao alikuwa anaitwa nani vile?
 
Back
Top Bottom