Haya wale wasikilizaji wa radio enzi hizo tukatane hapa tukumbushane baadhi ya vipindi

akilindefu

Member
Sep 5, 2020
69
63
Habari wana jukwaa.Leo nimeamua kulipanda jukwaa kwa kueleza na kukumbusha mengi wakati radio zikiwa zinavuma sana na nafahamu wengi tulikuwa wasikilizaji wazuri sana wa vipindi mbalimbali vya radio.

Binafsi mimi mi nililua mrahibu sana wa kusikiliza radio hilo lilipelekea baba yangu mzazi kuwa na tabia ya kunizawadia redio pale nlipokuwa nafanya vizuri kwenye mitihani ya shule kwangu mimi kuna watangazaji nawamisi sana baadhi yao ni Fredrick bundala(RFA) JUMA NKAMIA(TBC) JUMA BARAGAZA(RFA) na wengine wengi.niseme tu hawa ni kioo kwangu kufikia mpaka na mimi nikawa mtangazaji wa radio.

Haya na wewe tupe yako unayoyakumbuka kutokana na usikilizaji wa radio.Naomba kuwasilisha
 
Kuna kipindi kulikua usiku kwenye saa tatu RTD walikua wanachambua au wanatoa story ya wimbo
 
PM JM radio Tanzania nachingwea,
Leonard Mambo KBC taarifa ya habari na kombe la dunia 1998.
Halima Mchuka
Baragaza wa mambo mambo
Mambo ya elimu ,RTD kila siku saa nne
 
Bila shaka wewe mtoa mada ni msikilizaji mzuri wa DW na BBC maana maneno kama kulipanda jukwaa huwa nalisikia sana DW.​
Mraibu hahahaa umetisha sana.​
Kipindi cha Mambomambo RFA​
 
PM JM radio Tanzania nachingwea,
Leonard Mambo KBC taarifa ya habari na kombe la dunia 1998.
Halima Mchuka
Baragaza wa mambo mambo
Mambo ya elimu ,RTD kila siku saa nne
Kasoro KBC ila Leornad Mbotela nampata. Umenikumbusha hicho kipindi cha elimu rtd saa nne. Mzee alikuwa hataki kabisa kitupite.
 
Bila shaka wewe mtoa mada ni msikilizaji mzuri wa DW na BBC maana maneno kama kulipanda jukwaa huwa nalisikia sana DW.​
Mraibu hahahaa umetisha sana.​
Kipindi cha Mambomambo RFA​
hujakosea mkuu swadakta kabisa bila kumsahau sebastian ndege wa njia panda clouds
 
Tumbuizo Asilia, na Maiko Katembo. Wimbo wa outro anachomekea: Makondeeeee, Ngoma Juu, Manyanga Chini. Akasababisha msimu wa "Kubwaga Manyanga".
 
Habari wana jukwaa.Leo nimeamua kulipanda jukwaa kwa kueleza na kukumbusha mengi wakati radio zikiwa zinavuma sana na nafahamu wengi tulikuwa wasikilizaji wazuri sana wa vipindi mbalimbali vya radio.

Binafsi mimi mi nililua mrahibu sana wa kusikiliza radio hilo lilipelekea baba yangu mzazi kuwa na tabia ya kunizawadia redio pale nlipokuwa nafanya vizuri kwenye mitihani ya shule kwangu mimi kuna watangazaji nawamisi sana baadhi yao ni Fredrick bundala(RFA) JUMA NKAMIA(TBC) JUMA BARAGAZA(RFA) na wengine wengi.niseme tu hawa ni kioo kwangu kufikia mpaka na mimi nikawa mtangazaji wa radio.

Haya na wewe tupe yako unayoyakumbuka kutokana na usikilizaji wa radio.Naomba kuwasilisha
Dah! Mimi sichangii kabisa maana hawa unaowazungumzia wa jana tu! Mimi nalifikiri utamzungumzia Charlz Hillary anacheza mpira Uwanja wa Bora nyuma ya KIFUMA ukienda Polisi Mabatini pale Sinza au Marehemu Nyaisanga anabomu bia pale Vijana Social Hall!
 
RTD Pwagu na pwaguzi..
RTD malenga wetu..
RTD Mazungumzo baada ya habari.
RTD mahoka.
RTD Club raha Leo show.
RTD Kumekucha.
RTD shambani.
RTD Mchana mwema.
Kuna kipindi cha"'manenooo hayo" jamaa alikuw anajua kuchambua na sauti yake....RTD hatar
 
Back
Top Bottom