Haya tena! Mgombea udiwani wa Chadema achomewa nyumba!

Haya tena! Mgombea udiwani wa Chadema achomewa nyumba!

Mag3

Platinum Member
Joined
May 31, 2008
Posts
13,602
Reaction score
23,986
NEWS ALERT: MGOMBEA UDIWANI CHADEMA ACHOMEWA NYUMBA - Kwa hisani ya CHADEMA DIASPORA

Mgombea udiwani kwa tiketi ya CHADEMA kata ya Ubagwe wilaya ya Ushetu mkoani Shinyanga Bwana Adam Ahmad Ngoma amechomewa nyumba yake usiku wa kuamkia leo na wanao hisiwa kuwa ni vijana wa Greenguard.

Kata ya Ubagwe ni miongoni mwa kata zenye ushindani mkubwa katika kipindi hiki cha kampeni za uchaguzi mdogo, ni kata ambayo CHADEMA imetokea kuku
balika kwa kasi sana na mgombea wa udiwani kwa tiketi ya CHADEMA amekuwa akipokea vitisho kutokana na misimamo yake ya kutetea na kusimamia haki.

Alishatishiwa na vijana wa Greenguard mara kadhaa kuwa atachomewa nyumba hasa baada ya pingamizi dhidi yake alililowekewa na CCM kukwama.

Kutokea kwa tukio hilo kuna tafsirika kwamba ni ahadi iliyotimia kutoka kwa vijana hao waliokuwa wanamtishia maisha ikiwa ni pamoja na kumchomea nyumba.

Kwa sasa yuko polisi akiandikisha maelezo akiwa na makamanda wa CHADEMA alioambatana nao.

Tutazidi kujuzana.
 
......kwakweli inasikitisha, maslahi binafsi ya kisiasa yanaacha familia patupu!!! Mungu atalipa tu.
 
Pole sana kamanda tupo nyuma yako mpaka kieleweke. Waliofanya hicho kitendo wakamatwe wapelekwe mbele ya sheria
 
Ukimya wa wenye haki si silaha tosha kwa waovu.

Kila siku likitokea tukio kama hili twaishia kusema .......ipo siku....., so what?
 
nani wa kuwapeleka mbele ya sheria? hawa ndo huwa wanateuliwa kuwa viongozi wa greenguard
Pole sana kamanda tupo nyuma
yako mpaka kieleweke. Waliofanya hicho kitendo wakamatwe wapelekwe mbele
ya sheria
 
2015 hawa ccm tutalpza kisasi chetu kwakweli inasikitisha
 
Ccm ukiwazidi kwenye jukwaa wako tayari kukuua, ccm ni mashetwani hawafai hata kidogo, huo ni udiwani tu, je ubunge na urais itakuwaje?
 
Pole kamanda. Ndio gharama za ukombozi hizo...
 
Huyo kajichomea mwenyewe nyumba ili apate udiwani kwa huruma, kweli hiki chama cha mashetani.
mgombea mwanywa gongo unategemea nini?
 
watuhumiwa watafutwe, wakamatwe na kufikishwa mbele ya chombo cha kutoa haki.

Pole Mgombea kwa kunguliwa na nyumba.
 
Wafanyacho CCM sasa sicho ndo maana mwenyekiti wao kawakemea
 
Itajengwa nyingine tuu..mwambie achukue ushindi halfu kapu lipite..?Keshaingia ktk histori aya ukombozi
 
Waliohusika kuchoma nyumba ya huyo kamanda watafutwe,halafu wanyongwe hadharani au wapigwe risasi za moto mchana kweupe.
 
Hivi bado hao green guard wapo? Jamani si msajili wa vyama mstaafu alisema ni kinyume na sheria vyama kuwa na vijikundi vya kijeshi? Au ilikuwa ni kwa ajili ya CDM tu!
 
Back
Top Bottom