Haya Nyerere alishayakataa, si yake...!

Rapkatuni

Member
Sep 27, 2011
29
5
LEO hii tunapokumbuka nini tulichokipoteza miaka kumi na mbiliiliyopita katika taifa hili lenye makabila 126 na dini zaidi ya tatu,niwazi tunamkumbuka shujaa tuliyemtambua kama JK wa kwanza. Marehemu J.KNYERERE baba wa taifa hili lijulikanalo kama TANZANIA. Hakika hii nifursa ya kurejea na kupitia busara, hekima na ufanisi wa kiongozi huyuambaye alikuwa ni dira katika taifa hili..

Kiongozi im...arana mwenye heshima kubwa duniani ni wazi kuwa tunatakiwa tujiulizetunamuenzi vipi ili kwa kumuenzi huku wapatikane viongozi wengine hapombele watakao fanana na yeye katika mtazamo na utendaji. Ni wazi kuwakatika wakati wa sasa nikimaanisha upepo huu tulionao katika siasa hivisasa ni wazi kuwa tunawahitaji akina NYERERE wengi ipasavyo ilikurudisha hali katika hali yake.

Hii ni kwa sababu kuu ya kwamba katikasiasa za leo ndani ya tanzania kuna watu ambao tayari kwa makusudi nakwa dhamira ambazo hazina chembe ya wema kwa watanzania wanapotosha nakuvuruga muelekeo na mwenendo wa siasa za tanzania kwa kuyafanyayaleyale ambayo hapo nyuma tuliyapiga vita na kuyakemea katika jamiiyetu kwani si tu kuwa hayakuwa na faida kwetu bali pia hayana asili yajamii yetu.

Baba wa taifa alikuwa ndio kiongozi namba moja wa vita hiikatika ardhi ya Tanzania,ni vita ambayo ilipiganwa kuhakikisha kuwaudini na ukabila havipati nafasi katika mioyo na mitazamo yawatanzania,kwani tulifahamu kuwa vitu hivyo viwili ni adui mkubwa kwamaendeleo yetu sisi kama taifa na baba wa taifa alifahamu haya naakasimamia katika kuepusha hayo yasitokee kwetu.

Lakini ni miaka kumina miwili tu tangu kufariki kwa kiongozi wa vita hii tayari kuna watuwameshaibuka wakilitangaza,kulipandikiza na kulishabikia hili la udinina ukabila. Tunapolizungumzia suala la udini katika uongozi na siasa zandani ya tanzania hivi sasa ni vitu vyenye kukua na kupanuka kwa kasiya ajabu yenye kushinda kasi ya ukuajia wa kitu chochote chakimaendeleo chenye kuijenga jamii hii ya watanzania.

Ama kwa hakikahatutakuwa tukijitokeza mbele na kumtaja kiongozi huyu wa watanzaniakama kiigizo chetu ikiwa ndani ya mioyo yetu tumewekaubaguzi,udini,ufisadi,ukabila na rushwa. Tanzania ya leo imeshamirimambo haya hata ikafika kipindi watu wakasahau utaifa na ipi nidhamu yautaifa huo na vipi wautunze na kuuimarisha.

Sitaki kuitabiria mabayaTanzania wala sina nia mbaya juu ya utaifa wa mtanzania bali najaribukusema uhalisia wa mambo yalivyo katika siasa zetu leo hii kuwa kamatutaendelea hivi basi yale tuliyokuwa nayo kama misingi ya utaifa yetuyatavurugwa na kutokomezwa kabisa na badala yake yatakuja kutokea yaleambayo leo tunasimuliana na tunayaona kutokea kwa jirani zetu kamaSomalia, Congo, na kwingineko.

Haiwi sawa kwa watu walio na falsafa ya usawa, kuwa mmoja awe yuko juu ya mwingine tena akimbagua nakumkandamiza wa chini yake si kwa sababu nyingine yeyote lakini ni kwa sababu tu huyo ni wa kabila Fulani, dini Fulani, chama Fulani au wa eneo Fulani. Imefika wakati sasa kwa watanzania kujitambua kuwa wao ni watu wa jamii gani, wenye misingi gani na asili yao ni nini, ni wakati wa kutambua nini wanakihitaji na nini hawakihitaji na ni vipi watapata kile wanachookihitaji na pia vipi wataondokana na kile ambacho hawakihitaji.

Ni wakati wakufahamu yupi ni adui,yupi ni mnafiki na yupini rafiki wa kweli. Na kwa hakika hatutaweza kuyafahamu haya mpakaturudi na kujikagua upya kwa kuzingatia asili yetu na misingituliojiwekea baada ya uhuru wetu kawa watu wa taifa la Tanzania, nilazima turudi katika misingi ya usawa, amani, umoja na mshikamano.

MUNGU IBARIKI TANZANIA.,MUNGU IBARIKI AFRIKA….!
 
Back
Top Bottom