Haya ni yangu kutoka moyoni mwangu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Haya ni yangu kutoka moyoni mwangu

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by muislamsafi, Jun 18, 2012.

 1. m

  muislamsafi Member

  #1
  Jun 18, 2012
  Joined: Jan 25, 2012
  Messages: 78
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ni rahisi sana kusema mtufulani anatawaliwa na mkewe au mama mkwe au mtufulani ni mmbea lakini ni ngumu sana kusema mimi natawaliwa na mke wangu. ndicho hichi kinacho nifanya nishindwe kuchangia humu ndani kwenye mada zinazo fanana na ile ya kuchoma makanisa na nyingine nyingi za udini.

  Naona kabisa tunafanya makosa makubwa nasikia aibu na uzuni moyoni kwani mimi mwenyewe nimelelewa na familia ya mzee jacob na mkewe sara kilimanjaro moshi majengo kwamtei baada ya mzee kufariki na mama (ambaye sasa ni marehemu pia) akaona marafiki wake wa karibu ni hawa. hakujali kama mwanae anaishi na wakristo alijua tu kuwa kamkabidhisha mtoto wake kwa marafiki zake wa kweli na alijua hivyo kutoka moyoni mwake.

  Nilinunuliwa kanzu nzuri na zakutosha nikapewa na misaafu na vitabu vya dini yangu. na mama aliye nilea (sara) alikuwa ananiambia mama yako anapenda sana uijue dini yako vizuri hatanilipo litamani kanisa labda kwasababu ya utoto na niliishi mazingira ya wakristo wengi mama aliniambia ukisha kuwa mkubwa utaenda kanisani lakini kwa sasa jifunze kwanza hili ambalo mama yako mzazi ameniomba ni kuongoze.

  Sasa naona aibu kujiita muislamu natamani familia ya jacob inge nibadilisha tangu zamani na kuwa mkristo. kwani naamini mungu hakutuumba kwaajili ya jehanam, bali pepo. nikisikia watu wanachoma makanisa mabanda yanguruwe yanachomwa zanzibar wakristo wanaishi kwa mashaka wakati mimi nimelelewa na wakristo na wakaniongoza kama mapenzi ya dini yangu yanavyo taka na moyo wangu ukarizika nami nikawapenda nakuwaeshimu kama wazazi wangu!

  Inauma sana kuona watu waimani yako wanafanya haya inachoma sana nikisikia nguruwe za mzee jacob zilizo tumika kuninunulia mavazi malazi na chakula zimechomwa moto etikwa sababu dini yangu hairuhusu.nguruwe ambazo mimi zimenifikisha chuo kikuu na kunipa na kunilea pale mlimani kwa miaka mitatu.

  Huu niupumbavu wa hali yajuu. kamatunaitaji nchi ya kiislamu tukatengeneze ya kwetu angani hatuwezi hata siku moja kaulazimisha maji ya tiririke kupanda mlima, nchi iliyo jaa wakristo na waislamu halafu unataka kulazimisha sheria za kiislamu zitumike hii inamaanisha unawalazimisha wakristo kufuata sheria za kiislam, vipi na waikristo wakiamua sheria zao za dini yao zitumike au na wao walazimishe katiba itambue sheria zao.

  Nafahamu wazi kuwa asilimia kubwa ya waislam walio soma zamani walisoma seminary za wakristo ikiwa ni pamoja na raisi wetu kikwete. Natambua kuwa nyerere hakujenga shule kwa miaka mingi sana ya utawala wake, alizibadilisha shule na hospitali za wakristo kuwa za serikali, sasa sisi ni kinanani na tuna roho gani ambayo hata shukrani haina, nyerere asingelizibadilisha shule zile sisi tungelikuwa tumepiga hatua gani kwenye elimu. kama kikwete angezuiliwa kusoma seminary labda hata sasa asingelikuwa raisi wa hii nchi.

  natamani mtume wa mungu angeshuka na kushuhudia maneno yangu na kuupooza moyo wangu
  mimi narudia tena mimi nawapenda sana ndugu zangu wakristo na asanteni kwa msaada wenu kwangu na kwa ndugu zangu pia
   
 2. IGWE

  IGWE JF-Expert Member

  #2
  Jun 18, 2012
  Joined: Feb 3, 2011
  Messages: 7,753
  Likes Received: 1,326
  Trophy Points: 280
  Maneno yenye wingi wa hekima haya.
   
 3. Las Mas Bobos

  Las Mas Bobos JF-Expert Member

  #3
  Jun 18, 2012
  Joined: Jun 15, 2012
  Messages: 993
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Sasa kakufanyaje mjinga? Kwako wewe kuchoma kanisa ni sahihi?
   
 4. F

  Froida JF-Expert Member

  #4
  Jun 18, 2012
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 7,900
  Likes Received: 1,328
  Trophy Points: 280
  ushuhuda unagusa moyo,kweli tuendelee kufundishana sisi wote ni waja wake hakuna dini bora hapa duniani
   
 5. Ngorunde

  Ngorunde JF-Expert Member

  #5
  Jun 18, 2012
  Joined: Nov 17, 2006
  Messages: 1,128
  Likes Received: 735
  Trophy Points: 280
  Watakuita mnafiki kwa hii kauli yako ya neno UPENDO. Ila sishangai sana kwa hii taarifa yako baada ya kuona elimu yako.
   
 6. m

  muislamsafi Member

  #6
  Jun 18, 2012
  Joined: Jan 25, 2012
  Messages: 78
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  F.W mawazo yako ni sawa tu na ya wapuuzi wanaoichafua Dini na hayata fanikiwa kamwe
  uislam na maadili yake havita poromoka kamwe
   
 7. Akthoo

  Akthoo JF-Expert Member

  #7
  Jun 18, 2012
  Joined: Nov 5, 2007
  Messages: 587
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 60
  Mtumikie Kafiri Upate ujira wako!
   
 8. palalisote

  palalisote JF-Expert Member

  #8
  Jun 18, 2012
  Joined: Aug 4, 2010
  Messages: 8,352
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 0
  muislam safi hawezi kuandika hiki ulicholeta hapa.
   
 9. m

  muislamsafi Member

  #9
  Jun 18, 2012
  Joined: Jan 25, 2012
  Messages: 78
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  haisaidii kunikashifu jaribu kufikiri na kufanya maamuzi ya busara ilituishi kwa amani tanzania
   
 10. kibol

  kibol JF-Expert Member

  #10
  Jun 18, 2012
  Joined: Apr 24, 2012
  Messages: 3,141
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  muislamu safi anaandikaje?
   
 11. G

  GALIMA JF-Expert Member

  #11
  Jun 18, 2012
  Joined: Jun 29, 2011
  Messages: 275
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  ww hujielewi wapi uliposimama.do u think wote wanahuruma??nafikiri umechukua tabia za hao waliokulea ukageneralise.tabia haina dini.PIA ACHENI KUENEZA UDINI WATZ WENYEWE MASKINI MNAONGEZA JANGA LA UDINI.
   
 12. kibol

  kibol JF-Expert Member

  #12
  Jun 18, 2012
  Joined: Apr 24, 2012
  Messages: 3,141
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  kaka wala usiwaze sana,kwasababu nilichojifunza humu jf mpaka sasa hivi ni kuwa inapoletwa mada ya kidini humu ndani,watu akili zao zinawaruka kwa muda na kuongozwa na hisia na mapenzi kwa dini zao,wanasahau kuwa dini zote mbili za ukristo na uislamu zilikuja zikakuta watu hawa wanaabudu na wanaishi kwa upendo na amani.tuendelea kuishi kwa upendo na amani kama watoto wa Mungu mmoja despite of our differences.
   
 13. m

  mmteule JF-Expert Member

  #13
  Jun 19, 2012
  Joined: Oct 3, 2011
  Messages: 1,004
  Likes Received: 619
  Trophy Points: 280
  waafrika ndivyo tulivyo...ukristo na uislamu vya kuja tuuuu. dini za mababu zetu za kuabudu mizimu saaaaafi........ wala kusingekuwa na mpasuko wa umoja wa taifa letu. naipenda afrika naupenda uafrika... nauchukia uarabu nauchukia uzungu. full stop.msituletee utumwa wenu wa mawazo.....shit.... udin udin kil KONA tutampa kingunge madaraka tuone sasa!
   
Loading...