Haya ni mawazo potofu sana

Haya ni mawazo potofu sana

Mr Equalizer

JF-Expert Member
Joined
Dec 14, 2013
Posts
611
Reaction score
727
Kuna watu wanashangaza sana.

Baadhi yao wanadhani wako juu ya sheria. Kwamba wanaweza kufanya chochote bila mkono wa sheria kuwagusu.
Kwamba wanaweza kumpiga huyu kisha wakamsukuma yule bila ya sheria kukata upande wao.
Kwamba wanaweza kumpiga mtu kwa marungu hata kumvunja viungo vyake bila mkono wa sheria kuwaona.

Vitendo hivi hufanywa katika nchi ambazo watu wake bado wamejikita katika mawazo ya kunyanyasana.
Hizi ni tabia za kitumwa na utwana.

Hapa Afrika tabia hizi zililetwa na Wazungu .Hawa jamaa weupe waliwatumia Waafrika kunyanyasa Waafrika wenzao.

Sasa hivi hawa wazungu wameshabadilika , wameachana na tabia hizi za kitumwa .Tumebaki sisi watu weusi tunaoendekeza tabia hizi za kinyama , tabia za msituni , wanakoishi Simba Tembo Nyumbu na wengineo.

Huko msituni hakuna sheria , mwenye mabavu ndio mwenye haki , wanyonge hawana chao huko.

Huu ni wakati wa kuachana na tabia hizi za wanyama , sisi ni binadamu ambao Mungu ametuumba kwa mfano wake , lazima tujifunze kuwa na tabia za Mungu ambaye ni baba yetu.

Sisi mbona tunafanya makosa mengi tu na Mungu hutupigi marungu?

Hivi Mungu angekuwa anapiga Marungu nani angekuwa hai leo?

Tubadilike tuache unyama tuwe binadamu.



Sent using Jamii Forums mobile app
 
kweli tabia za ajabu ajabu za uonevu bila kufuata sheria tuziache
 
Mwamuzi wa mwisho ni hakimu/ Jaji, tuvute subra muda utaongea
 
Back
Top Bottom