MWITA BUGONGO
Member
- Jun 5, 2014
- 19
- 8
Tuko Dodoma kula
posho tu - Mjumbe
Rasimu ya Katiba Mpya
Na Habel Chidawali, Mwananchi
Posted Ijumaa,Agosti22 2014 saa 11:7 AM
KWA UFUPI
Nawakumbusha watu kufuta matumaini ya
kupata Katiba Mpya, kinachojadiliwa hapa ni
mambo ya kulazimishana kila upande, sisi
wengine tunaona bora ya Ukawa waliotoka nje
kuliko mambo ya humu ndani, alisema Juma
na kuongeza:
Dodoma. Katibu Mkuu wa Chama cha
Ukombozi wa Umma (Chaumma), Alli
Omari Juma amefuta matumaini ya
Watanzania kuhusu kupatikana kwa Katiba
mpya, badala yake akabainisha kuwa
wajumbe wako Dodoma kwa ajili ya kula
posho tu.
Nawakumbusha watu kufuta matumaini ya
kupata Katiba Mpya, kinachojadiliwa hapa
ni mambo ya kulazimishana kila upande,
sisi wengine tunaona bora ya Ukawa
waliotoka nje kuliko mambo ya humu
ndani, alisema Juma na kuongeza:
..Hata wale Wapemba waliokwenda Umoja
wa Mataifa kudai haki ya kujitenga , naona
walikuwa halali kwani hapa bungeni
hakuna mwakilishi hata mmoja kutoka
huko wakati tunaambiwa kuwa itakuwa
Katiba ya wote, ni kudanganyana.
Mjumbe huyo alisema kuwa Rasimu ya
Warioba imetupwa na wajumbe wa Chama
Cha Mapinduzi kiasi cha kuwafanya
wengine waone kuwa kinachotengenezwa ni
marekebisho ya Katiba ya 1977.
Alisema kuwa suala la akidi pia litakuwa ni
moja ya vikwazo vitakavyosababisha
kutopatikana kwa Katiba, akitolea mfano
kutoka kwenye kamati yake Namba 4.
Alisema ndani ya kamati hiyo mambo
mengi yanachakachuliwa kwani wajumbe
wanaotakiwa kutoka Zanzibar ni 14 lakini
waliopo ni 12 tu, ambao baadhi
hawakubaliani na mawazo ya CCM lakini
wanaambiwa mambo ni mazuri.
Ukawa walitoka kwa uhalali kabisa nami
nawaunga mkono, sisi tuliobaki humu
ndani tulikuja kwa makusudi ya kuangalia
kinachoendelea na sasa tunaona mambo ni
ovyo, alisema.
Kwa upande mwingine alimlaumu
Mwenyekiti wa Bunge Maalumu Samuel
Sitta kwamba amekuwa ni kinara wa
kuvuruga kanuni kila wakati na kutaka
mambo yake mwenyewe.
Jumba ambaye ni mtaalamu wa sheria,
aliwatupia lawama pia viongozi wa
Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kwamba
nao wanapaswa kulaumiwa kwa kushindwa
kuwaweka Wazanzibar pamoja ili wajue
wanataka nini.
Kwa mujibu wa Juma, kila maeneo
wanayojadili wanafanya kazi hiyo kwa
kuboresha maslahi ya CCM kwani
wanawasaidia kuwaandikia Ilani yao.
Alimtaka rais Jakaya Kikwete kukubaliana
na maoni ya watu mbalimbali kwamba
bunge la Katiba lisitishwe mara moja kuliko
kuendelea kujadili misimamo mikali ya
CCM.
posho tu - Mjumbe
Rasimu ya Katiba Mpya
Na Habel Chidawali, Mwananchi
Posted Ijumaa,Agosti22 2014 saa 11:7 AM
KWA UFUPI
Nawakumbusha watu kufuta matumaini ya
kupata Katiba Mpya, kinachojadiliwa hapa ni
mambo ya kulazimishana kila upande, sisi
wengine tunaona bora ya Ukawa waliotoka nje
kuliko mambo ya humu ndani, alisema Juma
na kuongeza:
Dodoma. Katibu Mkuu wa Chama cha
Ukombozi wa Umma (Chaumma), Alli
Omari Juma amefuta matumaini ya
Watanzania kuhusu kupatikana kwa Katiba
mpya, badala yake akabainisha kuwa
wajumbe wako Dodoma kwa ajili ya kula
posho tu.
Nawakumbusha watu kufuta matumaini ya
kupata Katiba Mpya, kinachojadiliwa hapa
ni mambo ya kulazimishana kila upande,
sisi wengine tunaona bora ya Ukawa
waliotoka nje kuliko mambo ya humu
ndani, alisema Juma na kuongeza:
..Hata wale Wapemba waliokwenda Umoja
wa Mataifa kudai haki ya kujitenga , naona
walikuwa halali kwani hapa bungeni
hakuna mwakilishi hata mmoja kutoka
huko wakati tunaambiwa kuwa itakuwa
Katiba ya wote, ni kudanganyana.
Mjumbe huyo alisema kuwa Rasimu ya
Warioba imetupwa na wajumbe wa Chama
Cha Mapinduzi kiasi cha kuwafanya
wengine waone kuwa kinachotengenezwa ni
marekebisho ya Katiba ya 1977.
Alisema kuwa suala la akidi pia litakuwa ni
moja ya vikwazo vitakavyosababisha
kutopatikana kwa Katiba, akitolea mfano
kutoka kwenye kamati yake Namba 4.
Alisema ndani ya kamati hiyo mambo
mengi yanachakachuliwa kwani wajumbe
wanaotakiwa kutoka Zanzibar ni 14 lakini
waliopo ni 12 tu, ambao baadhi
hawakubaliani na mawazo ya CCM lakini
wanaambiwa mambo ni mazuri.
Ukawa walitoka kwa uhalali kabisa nami
nawaunga mkono, sisi tuliobaki humu
ndani tulikuja kwa makusudi ya kuangalia
kinachoendelea na sasa tunaona mambo ni
ovyo, alisema.
Kwa upande mwingine alimlaumu
Mwenyekiti wa Bunge Maalumu Samuel
Sitta kwamba amekuwa ni kinara wa
kuvuruga kanuni kila wakati na kutaka
mambo yake mwenyewe.
Jumba ambaye ni mtaalamu wa sheria,
aliwatupia lawama pia viongozi wa
Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kwamba
nao wanapaswa kulaumiwa kwa kushindwa
kuwaweka Wazanzibar pamoja ili wajue
wanataka nini.
Kwa mujibu wa Juma, kila maeneo
wanayojadili wanafanya kazi hiyo kwa
kuboresha maslahi ya CCM kwani
wanawasaidia kuwaandikia Ilani yao.
Alimtaka rais Jakaya Kikwete kukubaliana
na maoni ya watu mbalimbali kwamba
bunge la Katiba lisitishwe mara moja kuliko
kuendelea kujadili misimamo mikali ya
CCM.