Haya ndo yalonikumba `Me too' kwenye LOVE CONNECT!

Status
Not open for further replies.

Me too

JF-Expert Member
Feb 9, 2015
7,377
9,297
Nikatoa bango langu likionesha vigezo na masharti kuzingatiwa. Akatokea Q dini tupo sawia maana kitaa yupo ila dini inagoma kabisa ie. Muslim vs Christian.

Sikujali Q aajiriwe au asiajiriwe mradi naweza kuitafta 500 ya mafuta ya kupaka na kusuka twende kilioni, ila ajue majukumu ya baba. Mapambano ya hapa na pale hayakosi ila msimamo wangu ni kupima HIV mara 3 na kuto kudo mpaka tujulikane hadharani hasa kwa wazazi.

Miezi imesonga, kuona nakazania msimamo wangu akaja na style ya "Am Busy". Calls asipokee kumbe ananikwepa na masharti yangu wakati huo nilimpa makusudi kama mume wa mtu hatoyaweza.

Mwezi wa 3 nikamtext kama kawaida yetu, kumbe simu kashika mkewe. Si akanipgia na kulalamika kuwa Q ni mumewe. Nikamwambia mbona kanambia hajaoa? Dada yule kalalamika nikamwambia kama ni mumeo nisamehe sikujua ila sasa nimeshajua sitakukwaza tena ila muonye mmeo kwa tabia ya uongo.

Dada akaridhika nami nikataka kuongea na Q, alichodakia unanijua wewe, namba yangu umeipata wapi?, kuanzia leo usitumie namba yangu usije vunja ndoa yangu bure!!!!

Ndo ukawa mwanzo wa kufunga file la JF.
 
Duu muandiko wako mzuri dada mwee jaman Ila masharti ndio yaliomkimbiza vizuri sana Ila namini mwisho utafanikiwa
 
jifunze hata wew kuwa na mashart hasa ukimtoa GIZANI km jf la cvo utaangukia MME/MKE wa mtu, au kulala na majini.

Mashart lazima nakubali lakini kwa ulimwengu wa sasa mambo ya kutogegeda kweli sii balaa.
Wewe watu wenyewe sio mabikra labda mie nina mtazamo tofauti lakini kwangu mie sifa kubwa ya kuwa mume au mke mwema ni kuwa bikra...kwa sasa kulitegemea hilo ni kujidanganya.
 
Ni wachache sana wenye kukubali hayo mashariti yako. Na ungekuwa hivyo tokea unazaliwa sidhani kama ungekuwa na mwanaume mpaka leo.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom