Macos
JF-Expert Member
- May 12, 2008
- 1,979
- 1,416
Wandugu huyu Mbunge ameonekana kituko.kituko kwa kutaka Diamond awekwe badala ya Picha ya askari nadhani ni utoto zaidi..Ila mimi nimeona hoja yake inaibua mjadala mpana kuhusu picha ile na Tanganyika.
Jee sanamu ile ni ya nini ?
Huyu mbunge ametufunua wengi kuhusu ile sanamu. Ni sanamu ya askari wa malkia wa UK alopigana kumuondoa mzungu mwenzie wa Kijerumani. Yule ni mwafrika , mwafrika alotumiwa na wakoloni hivyo nawwza kumwita alikua upande wa wakoloni wapo askari wabeba miziko au wapagazi walo andikwa katika placard ya pale. Lakini hawa sio mashujaa wa Tanganyika hata kama ni waafrika...hawa walipigana upande wa mkoloni muingereza dhidi ya mkoloni mjerumani hawa ni puppets sio wazalendo.
Naibua mjadala huu kwa makusudi na mbunge yule amechokonoa hoja ya msingi kabisa japo yeye kaleta uchepe.
Wafrika wa nchi hii walopambana na wakoloni ni Kinjekitile, Chief Mkwawa, Bushiri. Hawa walipoteza maisha yao kuilinda Tanganyika dhidi ya Ukoloni hawa wanastahiki kabisa stutue zao kusima pale tena za dhahabu ...na mtag ndugu yangu Mwanahistoria Mohamed Said aje nae atie mchango wake kuhusu hili
Wakoloni walitufanya wanaserere hata historia zetu tukazitia kwenye kapu na kutukuza za kwao.
Mwanzo ilikua picha ya askari wa kijerumani Major Hermann von Wissmann Waingereza waliindoa pamoja na Ya Bismack na Karls Peter
Sanamu Hii ya sasa , Ilizinduliwa Rasmi Dar es salaam hapo ilipo Mwaka 1927. Sanamu Hii imetengenezwa kwa shaba na imechongwa na James Alexander Stevenson.
Kabla haija letwa Dar es salaam iliwekwa kwa maonesho katika Royal Academy , London.
Tujaribu kusoma historia , kama hujui historia ya sanamu ile unakua saw ana huyo Mbunge . Hapa tunatakiwa kuijadili ile sanamu kama jee ibaki kama ilivo ambapo askari Puppet alo pigana upande wa Mfalme wa Uingereza dhidi ya Kals Peter wa Ujerumani ina maana yoyote Kwetu.
Jee si wakati mzuri wa kuwaenzi Kinjekitile, Abushiri na Mkwawa walopigana dhidi ya Ukoloni ? Hii ni hoja moto
Hii ni mada moto , hard talk kila mtu ajadili hili .