Haya ndio mapenzi ya siku hizi!

Haya ndio mapenzi ya siku hizi!

kaka9

JF-Expert Member
Joined
Jul 16, 2017
Posts
280
Reaction score
113
Mahusiano mengi ya mapenzi siku hizi,yamekuwa ni ya maigizo(Drama)sana kuna baadhi ya watu wanakuwa katika mahusiano na watu flani kwa sababu ya "show off" na kuwa "impress" watu wengine,unakuta msichana anajisifia mbele za watu "Eti boyfriend wake ni Branch manager wa bank flani/msanii maarufu au Kiongozi flani mkubwa.

Serikalini,lakini ni mara chache sana ukakuta msichana anajisifia mbele za watu kuwa boyfriend wake ni "mchamungu,mstarabu na mwenye Upendo mkubwa",Hiyo inaashiria nini? wanawake wengi siku hizi wanajali sana Mali na umaarufu kuliko utu

Lakini minawakumbusha kitu kimoja wasichana, cheo au Kazi ya boyfriend wako sio yako ni ya kwake,akiwa boss ni yeye sio wewe usijifu kwa nafasi yake au umarufu wake, halafu unatakiwa ujiulize umaarufu/Kazi yake ndivyo vinavyoweza kukupa wewe furaha au matendo yake?

kama umempenda mwanaume kwa sababu ya umarufu wake nakushauri ni bora ubaki kuwa shabiki wake tu na kama umempenda mwanaume kwa sababu ya Kazi yake nakushauri ni bora ubaki kuwa mteja wake tu,kwa sababu umaarufu na Kazi sio vitu vya kudumu lakini Upendo wa kweli hudumu milele,mwanamke mvivu huvutiwa na pesa za mwanaume lakini mwanamke mchapakazi huvutiwa na matendo na Hekima ya mwanaume.

Utajiri wa kweli ni kuwa na vitu ambavyo pesa haiwezi kununua "upendo,heshima na Busara" ,pesa inatupatia mahitaji tu lakini hauwezi kutupatia Upendo wa kweli.

Nawatakieni siku njema!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mtoa mada,
Siku hizi ukweli hawasikilizi tena. Utapigwa bure risasi ukiwa msema kweli.
Najua utashambuliwa sana, lakini ukweli utajisoma kwenye akili zao.

Tupambane tu na kutafuta Pesa za kuwatunza wake zetu na familia

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom