Haya ndio majina matatu ya wanachama wa CCM wanaoweza kupambana na Lissu jino kwa jino bandika bandua akimwaga mboga anamwaga ugali

Bezecky

Senior Member
Apr 28, 2024
136
146
Lissu ni kijana wa mjini na amefanya siasa nyingi za hoja na za hovyo akiwa Bungeni na sasa majukwaani.

Kwa mtazamo wangu haya ndio majina ya wanachama 3 wa CCM wanaoweza kupambana na Lissu jino kwa jino bandika bandua.

Anahitaji kujibiwa vile anavyokuja akija kihuni anajibiwa kihuni akija kisomi anajibiwa kisomi.

1. Prof Palamagamba Kabudi

2. Hamprey Polepole

3. David Kafulila
 
L
Hakuna hapo. Labda kwa mbali Prof Kabudi kwa sababu na yeye anaijua vizuri historia kama Tundu Lissu

Hao wengine vilaza tu
 
Yes kafulila anaweza kucheza miguu yote Kwa hoja nzito, hapo ccm waliokota kichwa hasa
 

Kafulila pumzika Wacha mahangaiko
 
Yes kafulila anaweza kucheza miguu yote Kwa hoja nzito, hapo ccm waliokota kichwa hasa
Hakuna mwana CCM anayeweza kuleta majibu yanayoelewa na kukubaliwa na wengi kuwa ni majibu kwenye issue ya Muungano.

Nielewe nikisema hakuna. Issue ya Muungano hata tumkodi Malaika kutujibia hawezi akaeleweka.

Wewe tu ukiulizwa kwa nini Mzanzibar anakuwa Mkuu wa Wilaya Tanganyika na mtanganyika hawezi kuwa mkuu wa Wilaya Zanzibar unaweza kujibu?

Hapo halijawekwa suala la umiliki wa ardhi!
 
Wewe ni muungwana..hivi kuna uongo au chumvi kwenye issue ya muungano anavyoisema Lissu kiasi kwamba kuna mambo hayafahamiki na hivyo Kafulila au Kabudi ndiye anaweza yaelezea..
Ni kweli hata aje malaika hakuna kipya atafafanua kuhusu muungano!
 
Acha kuota mchana
Professor hapo nani?
Hakuna wa kumshinda Lissu na hoja amini hivyo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…