Mgambilwa ni mntu
JF-Expert Member
- May 30, 2017
- 2,869
- 3,188
Real Madrid chini ya Bilionea na Mwenyekiti wao, Florentina Peres ilileta mapinduzi makubwa sana ya Soko la usajili wa wachezaji ghali duniani kuanzia Msimu wa 2000 - 2007. Timu hiyo ilitaka mafanikio ya haraka baada ya kuwa imechukua Champions League mwaka 1998 baada ya kusubiri zaidi ya miaka 32. Hivyo, haikutaka kusubiri tena ndipo ikaanza kununua Wachezaji wa bei mbaya: Luis Figo, Zidane, Ronaldo na Beckham.
.
Katika kumbukumbu za kihistoria, haijawahi kutokea wakati wa amani kwa Chama kilicho madarakani kufanikiwa kupata wanachama wengi wenye ushawishi kutoka kwenye vyama vya upinzani. Hali hii ya mshangao imetokea Tanzania katika Zama za CCM ya Dk. John Pombe Magufuli, kiongozi aliyetokea kuteka hisia za Waafrika wengi ambao wamekuwa wakimuona kama mfano mpya wa kuigwa barani Afrika (refer to Profesa Patrick Lumumba).
Tangu ichaguliwe tena mwaka 2015, CCM mpya imefanikiwa kuwasajili wanasiasa wengi maarufu nchini, kuanzia Wabunge, Madiwani na Viongozi wa Vyama vya Upinzani. Baadhi ya Vigogo kutoka Upinzani, ni:
Hongera Magufuli na Polepole kwa kufanikisha usajili wa majina makubwa na muhimu kwa ajili ya kupambana katika ligi ya siasa.
Naona Galacticos ya CCM ikivifyeka Vyama vingine come 2020 Election.

- Prof. Kitila Mkumbo (Mshauri Mkuu wa ACT)
- Samson Mwigamba (M/kiti Kamati ya Uchaguzi ACT)
- Albert Msando (Mwanasheria wa ACT)
- Anna Mghwira (M/kiti wa ACT na Mgombea urais 2015)
- David Kafulila (aliyekuwa Mbunge wa Kigoma Kusini - NCCR Mageuzi)
- Patrobas Katambi (aliyekuwa M/kiti BAVICHA Taifa)
- Mwita Waitara (Mbunge wa Ukonga - CHADEMA)
- Godwin Mollel (Mbunge wa Siha - CHADEMA)
- Julius Mtatiro (M/kitu was Kamati ya Uongozi ya CUF - Maalim)
- Julius Kalanga (Mbunge wa Monduli - CHADEMA)
- James Lembeli (aliyekuwa Mbunge wa Kahama - CCM)
- Maulid Mtulia (Mbunge wa Kinondoni - CUF).
- Zuberi Kuchauka (Mbunge wa Liwale - CUF)
Hongera Magufuli na Polepole kwa kufanikisha usajili wa majina makubwa na muhimu kwa ajili ya kupambana katika ligi ya siasa.
Naona Galacticos ya CCM ikivifyeka Vyama vingine come 2020 Election.